2956; Viwango, Fokasi na Kasi.
Rafiki yangu mpendwa,
Kama unataka kujenga biashara yenye mafanikio makubwa sana, unapaswa kufanyia kazi kwa uhakika maeneo hayo matatu.
Unapaswa kuweka viwango vya juu sana kisha kuhakikisha watu wote wanafikia viwango hivyo.
Biashara nyingi hazifanikiwi kwa sababu hakuna viwango vilivyowekwa.
Biashara inakuwa haina msimamo wowote.
Kila wakati inabadilika ili kuendana na kila mtu.
Mwishowe inakuwa ni biashara isiyoeleweka inalenga watu gani na kusimamia nini.
Biashara inapaswa kuwa na fokasi, kwa umakini wote kupelekwa kwenye vitu vichache ambavyo ndiyo muhimu zaidi.
Biashara nyingi hazifanikiwi kwa sababu kila wakati zinakimbizana na vitu vipya vinavyojitokeza.
Kila wakati kuna fursa mpya inayokuwa inafanyiwa kazi.
Fursa zinaweza kuwa nzuri, lakini kama haziwekewi umakini na kufanyiwa kazi kwa muda mrefu, zinakosa maana.
Unapaswa kujua kusudi la biashara yako kisha kuweka malengo ya kufika kwenye kusudi hilo.
Baada ya hapo kuachana na mengi yanayokujia kila wakati na kuweka fokasi yako yote kwenye yale yaliyo muhimu zaidi.
Biashara inapaswa kuendeshwa kwa kasi kubwa.
Maamuzi yanapaswa kufikiwa na kufanyiwa kazi haraka.
Biashara nyingi hazifanikiwi kwa sababu ya mambo kwenda taratibu.
Mambo muhimu yanachelewa kufanyiwa maamuzi na hata baada ya kuamuliwa bado utekelezaji unakuwa wa kusua sua.
Unapaswa kuwa na kasi kubwa kwenye kuamua na kutekeleza mipango ya kibiashara.
Ushindani ni mkali, ukizubaa unaachwa nyuma.
Ni viwango gani umeweka kwenye biashara yako? Watu wanaisifia biashara hiyo kwa vitu gani vya kipekee?
Ni fokasi gani uliyonayo kibiashara? Ni mambo gani pekee unayofanya na kupuuza mengine yote?
Una kasi kiasi gani kwenye kuamua na kutekeleza? Inachukua muda mrefu kiasi gani kuamua na kufanya?
Jikague maeneo hayo matatu kibiashara na utaona kuna fursa ya kuboresha zaidi ili uweze kukuza biashara yako zaidi.
Kila biashara ina wigo wa kuboreshwa zaidi kwa kukuza viwango, kuwa na fokasi na kuongeza kasi ya kuamua na kutekeleza.
Wewe kiongozi wa biashara ndiye unayeweza kuwa kikwazo kwa ukuaji wa biashara kwa kupuuza maeneo hayo matatu muhimu ya ukuaji wa biashara.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Mambo haya matatu ni muhimu sana na naenda kuyafanyia kazi.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ahsante sana
1. Watu wanaisifia biashara yangu kwa kuwai kufungua.
2. Focus- ipo kwenye
# kujenga timu
# kukuza mauzo.
Biashara ni vita na adui hana huruma.
LikeLike
Safi sana,
Linda sifa hiyo kwa gharama yoyote ile.
Peleka juhudi kwenye yao maeneo ya kufokasi.
LikeLike
Asante sana Kocha, ni kweli bila ya kuwa na fokasi pamoja na kasi kwenye biashara au kazi zetu hatutafanikiwa. Siku hizi mambo ni mengi, bila kuweka umakini kwenye biashara haiwezi kukua kwa haraka na kasi inayotakiwa.
LikeLike
Kweli kabisa, usumbufu ni mwingi mno na unahadaa kubwa.
Usipokuwa na fokasi, haukuachi salama.
LikeLike
Ahsnate sana kocha
1. Mimi biashara yangu wanaisifia kwakuwa na ufuatiliaji mzuri pale mtu anapoanza dozi.
2. Focus sasa ni kuhakikisha najenga timu ili isiwe inanitegemea mimi kwa nyakati zote.
LikeLike
Vizuri kabisa, linda sifa hiyo ili biashara iendelee kuaminika.
LikeLike
Biashara yenye mafanikio:
I. Viwango vya juu kwenye bidhaa/huduma, wafanyakazi na kuvisimamia kikamilifu.
2. Focus: umakini mkubwa, maono makubwa, ukuaji daima.
3. Kasi katika kuamua na kutekeleza. Kuacha ukiritimba.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Yusuph.
Ntahakikisha biashara yangu inakaa humo-Viwango,Fokasi na Kasi.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kwenye biashara yangu nachagua kupandisha na kusimamia viwango vya juu kila mara, sitashudha viwango ilibkupata watu ila nitasimamia viwango vyangu Hadi nipate wale watakaoweza kwenda na viwango vilivyowekwa.
Naweka umakini katika machache muhimu na kuachana na fursa mpya za kila siku.
Naweka focus eneo moja Hadi likamilike then naenda kwenye lingine kwani kufanya mambo mengi Kwa wakati mmoja huchosha zaidi, kupunguza ufanisi na mengi huishia njiani (nusunusu) hakuna la maana litakalokamilika Kwa ufanisi mkubwa kama hakuna focus
LikeLike
Vizuri, kamilisha haya ili kujenga biashara bora.
LikeLike
Hakika ni vita na vitani hakuna mazoea au comfort zone.
LikeLike
Vita ni kufa na kupona, lazima uwe makini sana.
LikeLike
Hakika ni vita na vitani hakuna mazoea au comfort zone, ni kuweka fokasi muda wote
LikeLike
Viwango, fokasi na kasi ni vitu muhimu sana kuvizingatia katika kazi na biashara. Asante sana kocha kwa kutukumbusha haha.
LikeLike
Karibu Basil.
LikeLike
Asante Kocha
1. Biashara yangu inasifika kwa ubora wa maarifa
2. Focus ni maarifa ya AMSHA UWEZO kuwafikia wengi kisha watu kupata mafanikio wanayostahili
3. Kasi siyo kubwa sana, nalipambania
LikeLike
Vizuri sana.
Kaa humo.
LikeLike
Asante Sana kocha kwa makala hii lakini kwa msisitizo ktk vipindi vya BIT,kuwa na viwango,kufokus kwenye vitu vichache nakuwa na sipidi ktk kufanya yale uliyoyapanga.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Biashara ni viwango,focus na kasi
Asante
LikeLike
Tukae humo.
LikeLike
Fokas ,viwango, kas.
Daima nitavismamia
LikeLike
Visimamie hasa bila kuyumba.
LikeLike
Standard Focus and speed. Ujumbe mirua kabisa huu. Ninkweli tunapenda kuweka Viwango, na speed Ila sisi viongozi tunakuwa vikwazo kwa tuliyoyaweka wenyewe. Hatuwi Mfano Bora katika kusimamia maamuzi na Viwango tunavyovitaka. Mfano mtu anasema nataka tudhibiti matumizi na hakuna mtu kuchukua bidhaa bila kufata utaratibu. Ila Kiongozi ndiyo mstari wa mbele kuingia kwneye drop na kuchota hela au bidhaa kuitumia bila kufata utaratibu. Hii inachelewesha mikakati na kukwaza Viwango vilivyoweka.
Weka Viwango na visimamie kwa speed kubwa ukiweka umakini wako kwenye lengo mama.
Asante
LikeLike
Watu wanaisifia biashara yangu Kwa namna ninavyotoa huduma Bora
LikeLike
Vizuri, simamia utoaji wa huduma bora kabisa bila kuyumba.
LikeLike
Tutapiga kelele sana, lakini watu wanaiga tunachofanya na siyo kusikia tunachosema.
Kuna funzo kubwa hapo.
LikeLike
Asante kocha nitakuwa na focus , kufanya maamuzi na kuyatekeleza
LikeLike
Kila la kheri katika kutekeleza haya.
LikeLike
Asante sana kocha kwa ujumbe mzuri,
Standards + focus + Speed lazima Zizingatiwe
Tena kwa MSIMAMO BILA KUACHA…
LikeLike
KWA MSIMAMO MKALI….
LikeLike
Viwango, Fokasi & Kasi ndio vitu nahakikisha biashara yangu ita zingatia. Asante sana Kocha
LikeLike
Vizuri kabisa.
Tukae humo.
LikeLike
Mara zote fokasi
LikeLike
MARA ZOTE…
LikeLike
Nitahakikisha naweka viwango,fokasi na kasi kubwa ili kukuza biashara yangu.
LikeLike
Tekeleza hilo.
LikeLike
Asante kocha
Viwango,fokasi na kasi hivi ndivyo vitu navyopaswa kuvisimamia ili kukuza biashara yangu
LikeLike
Vizuri, visimamie hasa.
LikeLike
nakaa kwenye viwango ,fokasi mbali sana na kuweka KASI kubwa nifanyalo
LikeLike
Tekeleza hili kwa uaminifu mkubwa.
LikeLike
_Kila mmiliki anaweza kuipandisha biashara yake na ikawa ktk viwango vya juu kabisa vya ubora kama ataamua kupeleka umakini wake wote kwenye biashara
Hiyo tuu. Na vile vile Kama atakuwa na Kasi ya kufanya maamuzi muhimu ktk biashara yake hiyo. Asante Sana kocha kwa pakegi hiyo . Yaani
1. Kuweka viwango vya juu
2. Focus
3. Kasi
LikeLike
Mara zote napaswa kuzingatia maeneo hayo matatu kwenye biashara;kufokasi,viwango,kasi.
LikeLike
Kasi yangu ya maamuzi ni ndogo nahitaji kuongeza kasi.
LikeLike
Mara zote napaswa kuzingatia maeneo hayo matatu kwenye biashara;kufokasi,viwango,kasi. Asante Kocha.
LikeLike
Kasi yangu ya maamuzi ni ndogo nahitaji kuongeza kasi na ubora.
LikeLike
Ahsante sana kocha kwa tafakari
LikeLike
Dawa ni kuwa na Viwango, kuFokasi na kuwa na Kasi.
Ahsante Kocha.
LikeLike
Wewe kiongozi wa biashara ndiye unayeweza kuwa kikwazo kwa ukuaji wa biashara kwa kupuuza maeneo hayo matatu muhimu ya ukuaji wa biashara.
LikeLike