2957; Utatu wa umasikini.
Rafiki yangu mpendwa,
Umasikini ni mbaya sana.
Kuna vitu vingi sana tunavyokutana navyo ambavyo vinadhihirisha umasikini na madhara yake kwetu.
Aliyekuwa raisi wa kwanza wa Tanzania, Mwl. J. K. Nyerere alichagua maadui wakubwa watatu ambao alishawishi kila mwananchi kupambana nao.
Maadui hao walikuwa ni Ujinga, Maradhi na Umasikini.
Pamoja na miaka mingi kupita tangu Nyerere kuainisha maadui hao, bado wameendelea kuwa mzigo kwa watu wengi.
Ukiwaangalia vizuri maadui hao watatu ambao Nyerere aliwaainisha, utaona kuna adui mkuu mmoja ambaye ni umasikini.
Ukiwa masikini, ujinga na maradhi vinakuwa na nguvu kubwa zaidi ya kukutikisa.
Ujinga na maradhi vinachangia sana kwenye umasikini, lakini pia ni zao la umasikini ambao watu wanakuwa nao.
Umasikini, ambaye tunaweza kumwita adui mkuu, unasababishwa na vitu vingi.
Lakini kuna vitu vikuu vitatu ambavyo huwa vinaambatana sana na umasikini.
Yaani popote penye umasikini, vitu hivyo vitatu huwa vinajidhihirisha wazi.
Kitu cha kwanza ni uvivu.
Tunaweza kusema uvivu na umasikini ni mapacha wa kufanana ambao wanaambatana pamoja kwenye kila jambo.
Masikini wana uvivu mkubwa sana ndani yao.
Wengine kwa nje wanaweza kuonekana kama ni wachapa kazi, lakini ni maonyesho tu.
Ndani yao hawapendi kile wanachofanya na wanatafuta kila sababu ya kutokufanya kazi.
Kitu cha pili ni kutokujiweza au kwa maneno rahisi uzembe.
Hapa watu wanakuwa hawana uwezo wowote wanaoweza kuuonyesha kwa wengine na wakaaminika.
Watu wanaweza kuonekana wanachapa kazi sana, lakini mambo wanayofanyia kazi ni ya kawaida sana, hakuna kinachowatofautisha na wengine.
Kwa kifupi masikini huwa wana uwezo mdogo sana wa kufanya mambo makubwa na ya tofauti.
Hawapendi kujaribu vitu vipya na vya tofauti.
Hivyo kwa kukosa uwezo wa kujitofautisha na wengine, masikini wanajikuta katikati ya kundi kubwa lenye ushindani mkali sana.
Kitu cha tatu ni ujinga.
Na huu ni tofauti na ule ujinga ambao Nyerere aliutaja. Nyerere alitaja ujinga wa kutokujua kusoma na kuandika, na ndiyo maana elimu ya watu wazima ilishamiri zama hizo.
Lakini kwa zama hizi, karibu kila mtu anajua kusoma na kuandika.
Ujinga wa zama hizi ni watu kukosa maarifa ya nini wafanye na wafanye kwa kiwango gani ili waweze kutoka kwenye umasikini.
Ukiangalia kwa umakini, unaona masikini wakiwa ndiyo wanajiona wajuaji wakubwa.
Waambie wajifunze kwa kusoma vitabu na hatua nyingine muhimu na watakujibu hawana muda, au fedha. Kwa vyovyote wataashiria kujitunza siyo kipaumbele kwao.
Lakini wale wanaopiga hatua kubwa kwenye maisha yao na kuushinda umasikini huwa ni wanyenyekevu na wenye utayari wa kujifunza.
Wanapojifunza wanachukua hatua mara moja kwenye yale waliyojifunza, kitu kinachowapa matokeo ya tofauti.
Rafiki yangu mpendwa, mambo hayo matatu; Uvivu (Laziness), Uzembe (Incompetence) na Ujinga (Ignorance) ndiyo utatu mkuu wa umasikini, ambayo ukiwa nayo, hakuna namna unaweza kutoboa kutoka kwenye umasikini.
Utahangaika sana, lakini kama hutayavunja hayo matatu, utaishia pale ulipoanzia.
Ni mpaka uvunje utatu huo na kuusambaratisha ndiyo utaweza kupiga hatua kubwa unazotaka kupiga.
Kataa uvivu kwa kuwa mchapa kazi, jijengee nidhamu kali ya kazi na isimamie mara zote.
Ondokana na uzembe kwa kujijengea uwezo wa kipekee unaokutofautisha na wengine.
Na muige Socrates, mtu mwenye hekima sana kuwahi kupita hapa duniani, ambaye aliwahi kusema, kitu kipekee ninachojua ni kwamba sijui, hivyo kuwa tayari kujifunza. Ondokana na ujuaji, jifunze na chukua hatua ili kuyaboresha maisha yako.
Watu huusema sana umasikini, kwamba ni laana na mengine mengi.
Lakini utatu huu uliojifunza hapa ndiyo mzizi mkuu wa umasikini.
Yeyote anayeweza kuyavunja, hakuna namna anaweza kubaki kwenye umasikini.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Nitapambaba kuvunja uvivu,uzembe na ujinga ili kutobaki kwenye hali ya umaskini.Asante Makirita kwa kutukumbusha hili.
LikeLike
Nakataa kuwa MTU w kawaida. Nakataa kuwa masikini. Mimi ni bilionea mafunzoni
Ninachapa kazi kwa bidii. Sizembei kazini na mara zote najifunza
LikeLike
Ukiweza kuvunja uzembe, ujinga na uvivu utakua mtu wa tofauti sana.
LikeLike
Uvivu, uzembe na ujinga ni vitu ambavyo havipaswi kuvumiliwa wala kuendekezwa ktk maisha yetu. Asante sana Kocha 🙏🏽
LikeLike
Nitapambana na kusambakatisha uvivu, uzembe na ujinga kwa nguvu zangu zote!
LikeLike
Najua sijui, siku zote nitakuwa mnyenyekevu kujifunza.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
usijenge urafiki na uvivu,uzembe,ujinga.Kuondokana na hayo nitafanya haya
uvivu=nitajituma sana kuweka kazi
uzembe=kufanya vitu kwa utofauti na si ukawaida.
ujinga=kujifunza na kuchukua hatua sahihi baada ya maarifa.
LikeLike
Ahsante sana Kocha.
Naukataa na kuupinga umasikini mara zote kwa kuweka kipaumbele cha kazi kuwa mbele siku zote.
✅✍️👏👏
LikeLike
Uzembe uvivu na ujinga ndio maaadui naopaswa kupambana nao kwa kila namna ili kutokua maskini.Asante kocha kwa kuendelea kufungua akili zetu.
LikeLike
Kitu pekee ninachojua ni kwamba sikijui kitu,hivyo nakuwa tayari kujifunza. Asante sana Kocha.
LikeLike
Nitapambana na utatu wa umasikini ambao ni uvivu,uzembe na ujinga mchana na usiku ili kumshinda adui yetu mkuu ambaye ni umasikini.
LikeLike
Asante sana Kocha kweli Uvivu, Uzembe na umasikini ni tatizo kubwa sana kwenye zama hizi tunazoishi
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Uvivu,uzembe na ujinga ndio utatu wa umaskini tukiviondoa hivi lazima tutatoboa
Asante sana
LikeLike
Uvivu ,uzembe,ujinga ni utatu wa umaskini tukiviondoa hivi lazima tutoboe
Asante sana
LikeLike
Lowassa alisema hakuna faraja yoyote katika umaskini.
LikeLike
“Cowardness” ni hali inayochangia sana umaskini.
LikeLike
Ukiweza kuondokana na hivi vitu vitatu ;Uvivu, uzembe na ujinga lazima tutoboe.
LikeLike
Ni jambo bora kupambana na utatu huu wa umaskini ili kuwa na maisha yenye maana kwenye jamii zetu: kwa kuepuka hivi vitu vitatu vinapalilia umaskini mafanikio ni jambo la lazima kulifikia
LikeLike
Imekaa vzur sana
LikeLike
Ni Bora ukutane uso kwa uso na Simba mwenye njaa kuliko kuruhusu uvivu , uzembe , na ujinga vikutawale,
Asante Sana kacha .
LikeLike
Umasikini sio utakatifu lazima tukubali kuondokana nao
LikeLike
Tuuchukie kabisa.
LikeLike
Utatu wa umaskini ni UVIVU, UZEMBE naUJINGA. Asante Sana kocha na kama ni lasna, basi ni lasna ambazo mtu anajilaani mwenyewe kwa kutokuwajiibika.
Kama mtu amejilaani mwenyewe anatakiwa avunje mwenyewe
LikeLike
Kabisa, hakuna wa kumlaumu.
LikeLike
ahsante kocha, nitavunja uvivu , uzembe na ujinga
LikeLike
Asante kocha nitapambana kuepuka uzembe,uvivu na ujinga hasa kupitia kujifunza.
LikeLike
Dawa ni kuvunja Uvivu, Uzembe na Ujinga.
Ahsante Kocha.
LikeLike