2959; Kisima kitupu.
Rafiki yangu mpendwa,
Kama una bomba la maji ambalo linatokea kwenye kisima, lakini halitoi maji, siyo kwamba maji hakuna kabisa, bali ni kisima ndiyo kitupu.
Kama kisima kingekuwa na maji, ni dhahiri bomba lingetoa maji.
Unaweza kulalamika hakuna wateja kwenye biashara yako, lakini huo siyo ukweli. Wateja wapo na wananunua, tatizo lako ni una wateja tarajiwa wachache unaowafuatilia.
Kama una wateja tarajiwa wawili tu unaowafuatilia na wote wakawa hawapo tayari kununua, utaona hakuna wateja.
Vipi kama utakuwa na wateja tarajiwa 100 ambao unawafuatilia? Kwa hakika kuna ambao watakuwa tayari kununua.
Kwa hiyo unajionea hapo, tatizo siyo maji (wateja), tatizo ni kisima (orodha ya wateja tarajiwa unaowafuatilia).
Kwa kuongeza idadi ya wateja tarajiwa unaowafuatilia, unaongeza nafasi ya kupata wateja zaidi.
Kadhalika kwa wafanyakazi unaowatafuta uwaajiri. Unapokosa wafanyakazi bora siyo kwa sababu hawapo, ila kwa sababu kuna wachache sana unaowafuatilia. Kama hao wachache wasipokuwa sahihi, unaishia kukosa wafanyakazi. Lakini kama ungekuwa na wengi ambao unawafuatilia, kati ya hao unakuwa na nafasi kubwa ya kupata walio bora.
Mara nyingi tunajikwamisha kwenye maisha kwa sababu ya namba ndogo tunayokuwa tunafanyia kazi. Namba hiyo ndogo inaposhindikana, tunakwama na kuona mambo hayawezekani.
Lakini kama tutakuwa na namba kubwa tunayofanyia kazi, uwezekano wa kupata tunachotaka unakuwa mkubwa zaidi.
Kwenye kila eneo la maisha yako, kuwa na namba kubwa unayoifanyia kazi. Hiyo ndiyo ndani yake utaweza kupata kile unachotaka.
Kama bomba halitoi maji, jaza kisima.
Kama utakuwa unajaza kisima kila wakati, bomba nalo litatoa maji kila wakati.
Unachohitaji ni mkakati sahihi wa kuhakikisha kila wakati maji yanaingia kwenye kisima, ili pia kila wakati maji yawe yanatoka bombani.
Kwa matokeo yoyote unayotaka kuyapata, weka juhudi za kutosha katika hatua zake za awali. Usitegemee matokeo ya mwisho kama juhudi za awali hujaweka.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Usitegemee matokeo makubwa kama hujaweka juhudi kubwa.
Asante sana
LikeLike
Wateja tarajiwa wengi=wateja wanaoununua =mauzo makubwa
LikeLike
Ni kweli hilo liko wazi maji yakipungu kwenye koki maana yake kisima kinaelekea kukauka na kwa mauzo pia wateja wakipungua maana yake tunakua tumepunguza nguvu ya usakaji na kutafuta wateja wengi
LikeLike
Usakaji haupaswi kupoa.
LikeLike
Asante,
Weka namba kubwa ya kila unachofanyia kazi,unapokutana na siyo chaguo uwe na wigo mpana kwa mengine mengi uliyo nayo.Namba ndogo unakaribisha ukomo na kukwama na kuona haiwezekani.
LikeLike
Mara nyingi tunajikwamisha kwenye maisha kwa sababu ya namba ndogo tunayokuwa tunafanyia kazi.
LikeLike
Napaswa kuwa na idadi kubwa ya wateja tarajiwa ninaowafuatilia ili niweze kuongeza mauzo.
LikeLike
Naenda kujaza kisima changu,ili nipate maji mda wote. Wateja wengi zaidi unajihakikishia mauzo.
LikeLike
Hilo ni kweli kocha, kuna mteja aliniagiza bando 3 za bati za rangi, nikamwimbia kwa sasa sina ila nakuagizia kufika juma tank zitakuwa zimefika. Nikamuomba atoe advance kidogo. Akakataa akasema zikifika analipia zote. Nikamwambia sawa.
Nikaziagiza kwa fedha zangu. Bahati mbaya Transporter akachelewa kwenda kupakia na alipopakia gari ikaharibika njiani hivyo hizo bati zikachelewa zikafika jumatatu ya wiki nyingine.
Huyo mteja alipoona jumatano hakuna bati akaenda kununua sehemu nyingine. Ila kuna mtu mwingine naye alikuwa anahitaji rangi hiyo hiyo nikampa. Hivyo kama ningetegemea mteja mmoja ningekwama na kuanza kulaumu Transporter, gari na mteja kwamba sio muelewa.
Hivyo pipeline kubwa inasaidia.
Database kubwa ya wateja.
Database kubwa ya wafanyakazi.
LikeLike
Juhudi kubwa iatangulie ndipo matokeo makubwa yatafuata
LikeLike
Asante sana, Kila wakati nitajaza maji kwenye kisima
LikeLike
Ahsante sana kocha, nitakwenda kujaza kisma maji (wateja tarajiwa) ili niweze kupata wale watakaofanya maamuzi ya kununua
LikeLike
Jukumu langu nikujaza maji kwenye Kisima.
LikeLike
Ni sahihi kabisa, kadri tunavyoweka juhudi katika kujenga wateja tarajiwa wengi ndivyo tunavyojiwekea nafasi ya kuwa na wateja kamili wengi sana.
Ahsante sana Kocha Kwa makala hii muhimu kwangu
🔥✅👏
LikeLike
Asante kocha,nitajitahidi kuweka msingi mkubwa mwanzoni na sio kuhitaji matokeo ya mwisho uku sijajiandaa mwanzoni.
LikeLike
Ni kweli kabisa
Ili kupata matokeo bora lazima niweke juhudi za kutosha katika hatua za awali.
LikeLike
Asante ni kweli kama kisima hakina maji huwezi kupata maji..
LikeLike
Hakika kisima kitupu hakiwezi kutoa maji.
LikeLike
Nitapambana kuongeza namba ya wateja
LikeLike
Asante Kocha, naendelea kuweka juhudi kufikia namba kubwa za wateja tarajiwa.
LikeLike
Kweli kabisa Kocha, yatupasa tujiwekee viwango ( number ) vya juu sana ili tuweze kupata mafanikio makubwa kwa mfano ifikapo 2030 lengo letu ni kufikia Ubilionea ( TZS 2,380,000,000,000 ), cha msingi ni kuweka kazi kwa jitihada kubwa sana.
LikeLike
Tujaze kisima maji kila siku ili mabomba yatoe maji
Asante
LikeLike
Kila unapotumia, kumbuka kujaza pia.
LikeLike
Muhimu sana hilo, maana unaweza kufurahia kutumia bila kuangalia kina kilichobaki. Halafu yanakata ghafla, kuangalia kisima ni kitupu kabisa.
LikeLike
Asante Sana kocha,kama kisima hakina maji,bomba litatoa wapi maji, nguvu kubwa lazima kwenye biashara ielekezwe kwenye wateja tarajiwa.
LikeLike
Kabisa,
Na hapo ndipo wengi wanajisahau.
LikeLike
Najaza maji kisimani Ili Bomba lisikate maji, maji yakikatika sitojiuliza sababu sababu ni kisima kitupu…wateja wengi tarajiwa ndilo suluhisho la kukosa wateja au wateja Kamili wachache.
LikeLike
Kweli ni muhimu kuboresha bank ya maji yaani Kisima kisikauke maji. Nakuza orodha ya wateja kutengeneza hazina kubwa ya wateja.
LikeLike
Napaswa kuwa makini nakujaza kisima changu kila kinapopungua ili kuwa na uhakika wa maji mara zote
LikeLike
Hakika kocha tatizo siyo maji bali ni Kisima kitupu. Asante
LikeLike
Dawa ni kuongeza JUHUDI. Kuwa na namba kubwa ninayoifanyia kazi.
LikeLike
Hakika
LikeLike