3012; Kama hakuna tatizo ni tatizo.
Rafiki yangu mpendwa,
Kama unaiendesha biashara yako kwa kasi na mabadiliko tunayoenda nayo, kuna matatizo mengi ambayo utayatengeneza.
Mabadiliko yoyote unayofanya, lazima yazalishe matatizo mbalimbali.
Kadhalika pale unapokwenda kwa kasi kubwa, lazima ufanye baadhi ya makosa ambayo yanaleta matatizo.
Kama unaendesha biashara yako na hakuna matatizo wala changamoto zozote, hilo ni tatizo kubwa.
Ni tatizo kwa sababu hakuna makubwa au ya tofauti unayofanya na hivyo biashara hiyo haiwezi kukua.
Kuajiri watu kwenye biashara kunazalisha matatizo yake.
Kutafuta wateja wapya kwenye biashara kunakuja na matatizo yake.
Kujenga mfumo wa kuiendesha biashara kunaleta matatizo mbalimbali.
Kuwepo kwa matatizo na changamoto ni kiashiria kwamba mabadiliko na kasi vinafanyika kwenye biashara.
Na hiyo ni ishara njema kwani inaleta fursa ya kupiga hatua zaidi.
Kuwepo kwa matatizo kunawafanya watu wachukue hatua za tofauti, kitu kinacholeta mabadiliko.
Kutokuwepo kwa matatizo kunafanya watu waende kwa mazoea kitu kinachozuia mabadiliko.
Kuendesha biashara inayokua ni sawa na kazi ya kuzima moto.
Kila wakati kuna moto unaopaswa kuuzima, yaani matatizo yanayokuwa yamejitokeza kutokana na mabadiliko unayokuwa umeyafanya.
Hakuna mzimamoto makini anayeukimbia moto, hiyo ndiyo kazi yake.
Kadhalika hakuna mfanyabiashara makini anayeyakimbia matatizo ya biashara, hiyo ndiyo kazi yake kuu kwenye kuikuza biashara yake.
Kama unaiendesha biashara yako na hakuna tatizo lolote, hilo ni tatizo kubwa.
Ni kiashiria unafanya mambo kwa mazoea na ukawaida mkubwa.
Kufanya mambo kwa mazoea na ukawaida ni kukaribisha ushindani ambao utakuondoa sokoni.
Wakati mwingine matatizo unayokuwa nayo kibiashara yanawatisha wengine hata wasijaribu kufanya unachofanya, kwa sababu wanaona hawataweza kuhimili yale unayoyapitia.
Kwa kuwa wewe tayari umeshajijenga kuwa imara, unaweza kuyavuka matatizo yoyote bila ya kuhofia.
Kwa kuwa unayategemea matatizo, hayakushangazi na wala huyakimbii.
Unayakaribisha na kuyatatua, ukijua utazalisha matatizo mengine zaidi ambayo pia utayatatua.
Unajua huo ndiyo mchezo wa maisha yako yote utakayokuwa kwenye biashara.
Na unaufurahia hasa, kwa sababu unafurahia matokeo ya tofauti unayozalisha, licha ya kuwa yameambatana na matatizo zaidi.
Kama umekuwa unategemea ujenge biashara kubwa bila ya matatizo yoyote umekuwa unajidanganya.
Kama unadhani kuna siku matatizo ya kibiashara unayokutana nayo yataisha, unajiandaa kukata tamaa.
Biashara inayokua na matatizo ni mapacha ambao hawawezi kutenganishwa.
Nenda nao kwa pamoja na utapata matokeo bora kabisa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ni mapacha maana ukiona tatizo ni lazima likukatishe tamaa
Ukilegea tu umekwisha tunapaswa kuwa makini na kupambana na matatizo ili biashara na sisi tuendelee kuwa bora zaidi
LikeLike
Nitakuwa tayari kukabiliana na matatizo ambayo yatajitokeza kwenye biashara yangu
LikeLike
Hakika, biashara na matatizo ni mapacha au ndugu wanaoishi pamoja.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Hakuna shaka matatizo ndiyo fursa ya kusonga mbele.kama hakuna matatizo basi hufanyi chochote.
LikeLike
Kwa hakika hii habari ni nzito kwa kuzingatia haya,
Biashara inayokua na changamoto ni mapacha huwezi kuwatengamisha
LikeLike
Ukiona tatizo kuna kisababishi. Kitafute kifanyie kazi ili kuleta mabadiliko ambayo ndiyo maendeleo.
LikeLike
Kujenga biashara kubwa lazima utatue matatito makubwa
Asante
LikeLike
Matatizo ni sehemu ya biashara, hivyo tunatakiwa kuyapokea na kuyatafutia ufumbuzi
LikeLike
Sitayakimbia matatizo kwenye biashara ,nitayakabidhi ili niendelee kuwa imara kwani matatizo hayawezi kuisha kwenye biashara,na nikiyakimbia matatizo nijiambie tu ukweli kwamba biashara imenishinda.
LikeLike
Matatizo yataendelea kuongezeka na ukuaji wa biashara, lakini nitapaswa kuyatatua ili kuendelea kukua zaidi na kukaribisha mengine ambayo nayo nitayatua pia.
LikeLike
kujiondoa kwenye ushindani ni kutafuta matatizo ya kutatua ili wakati wao wanaona ni tatizo kumbe ndo unajiondoa kwenye ushindani
asante kocha.
LikeLike
Biashara inayo kuwa na matatizo ni mapacha wasioweza kutenganishwa mara zote nitakuwa niki-tatua matatizo kwa shauku kubwa Maana najua ya kwamba biashara yangu inakuwa.
LikeLike
Shida ya tulio wengi tunakimbiaga shida na matatizo badala ya kutatua
LikeLike
Asante sana Kocha kwa ujumbe huu.
Nimejifunza kuwa biashara inayokua na Matatizo ni mapacha ambao hawawezi kutenganishwa.Ili kupata matokeo bora kabisa hatuna budi kwenda nao pamoja
Asante sana.
LikeLike
Mzima moto hakimbizi moto Bali anaukabili na kuuzima…sitayakimbia matatizo ya biashara Bali nitayakabili hasa
LikeLike
hata kwenye maisha kama hupitii matatizo/changamoto ujue hufanyi makubwa na unaenda kwa mazoea
LikeLike
Hakuna mzimamoto makini anayeukimbia moto, hiyo ndiyo kazi yake.
Kadhalika hakuna mfanyabiashara makini anayeyakimbia matatizo ya biashara, hiyo ndiyo kazi yake kuu kwenye kuikuza biashara yake.
Ahsante Kocha.
Nitayakabili matatizo kikamilifu.
LikeLike
Kama unaiendesha biashara yako na hakuna tatizo lolote, hilo ni tatizo kubwa.
Ni kiashiria unafanya mambo kwa mazoea na ukawaida mkubwa.
LikeLike