3028; Maamuzi ya mtu mmoja.
Rafiki yangu mpendwa,
Makosa mengi kwenye maisha huwa yanafanyika wakati wa kufanya maamuzi.
Na kadiri watu wengi wanavyohusika kwenye kufanya maamuzi, ndivyo nafasi za kufanya makosa zinavyokuwa nyingi.
Maamuzi bora ni yale yanayofanywa na mtu mmoja, ambaye ana uelewa wa kina kuhusu kile anachokiamulia.
Mtu huyo anaweza kuchukua maoni ya wengine, lakini ana uhuru wa kuamua kile kinachofaa na siyo kuamua ili kuwaridhisha wengine.
Kadiri maamuzi yanayotakiwa kufanywa yanavyokuwa makubwa na muhimu, ndivyo wengi huhofia kuyafanya peke yao na hivyo kutafuta kikundi cha watu cha kujificha nyuma yao.
Hivyo ndivyo kamati mbalimbali huzaliwa.
Kamati huwa zinaundwa ili kuelewa jambo kwa kina na kulifanyia maamuzi.
Lakini kwa bahati mbaya sana, siyo wote wanaokuwa kwenye kamati wanakuwa wametenga muda na kuelewa kwa kina kile wanachopaswa kuamua.
Hivyo unapofika wakati wa kufanya maamuzi, wanaishia kufuata mkumbo wa wengi wako upande gani.
Maamuzi ya kuangalia watu wengi wako upande gani hayajawahi kuwa maamuzi sahihi.
Na hilo ndiyo linafanya maamuzi yanayofanywa na kamati kutokuwa sahihi.
Wewe kama kiongozi mkuu wa biashara yako, unapaswa kuwa ndiye mfanyaji maamuzi mkuu kwenye biashara hiyo.
Hivyo epuka sana kujificha nyuma ya kamati au watu wengine.
Hakuna anayeweza kujali kuhusu biashara yako zaidi yako wewe mwenyewe.
Hili halimaanishi uwe na kiburi na usisikilize maoni ya wengine.
Sikiliza maoni ya wengine, ila yachuje kwa uhakika kabla hujayatumia kufanya maamuzi.
Maoni mengi unayokuwa unapewa na watu ni ya jumla na ya juu juu. Hayajazingatia jambo kwa kina na msingi wake.
Ni muhimu kushirikiana na wengine kwenye ujengaji na uendeshaji wa biashara yako.
Lakini wewe mwanzilishi, ambaye ndiye mbeba maono makubwa ya biashara yako, unapaswa kuwa ndiye mfanyaji maamuzi mkuu kwenye biashara.
Endelea kujinoa na kuwa bora kupitia maamuzi yote unayoyafanya.
Unapofanya maamuzi, andika sababu ulizotumia katika kuyafanya.
Kisha matokeo yanayopatikana, yapime pia na matarajio yako, na hapo utaweza kulinganisha matokeo yanayopatikana na matarajio yaliyokuwepo.
Unafanya hivyo siyo kwa ajili ya kujiumiza kwa matokeo ya tofauti unayokuwa umepata, bali kujiboresha ili wakati mwingine ufanye maamuzi bora zaidi.
Kila nchi ina raisi mmoja,
Lila jeshi lina jenerali mmoja,
Na kila kampuni ina CEO mmoja.
Haimaanishi kwamba watu hao waliopata hizo nafasi ndiyo wajanja kuliko watu wengine wote.
Bali inamaanisha ni watu ambao wamejitoa kuwajibika kwenye kile wanachoongoza.
Usipokuwa tayari kukosea,
Na usipokuwa tayari kujifunza na kulielewa eneo lako kwa kina,
Hutaweza kujijengea hali ya kujiamini na kufanya maamuzi sahihi.
Utajikuta ukihangaika na mambo mengi lakini ukikwepa kufanya maamuzi kwenye mambo ambayo ni muhimu.
Ni muhimu sana maamuzi yote makubwa yafanywe na mtu mmoja.
Mtu mwenye uelewa wa kina kwenye eneo hilo na ambaye anachukua maoni ya wengine na kuyachakata vyema.
Sisi viongozi wa biashara ndiyo watu sahihi wa kufanya maamuzi yote makubwa kwenye biashara.
Hivyo tunapaswa kuhakikisha kila wakati kuwa kwenye nafasi nzuri ya kufanya maamuzi bora na yenye tija.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Siku zote nitakuwa ndiye muamuzi mkuu kwenye biashara yangu
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kwenye biashara yangu mimi kama kiongozi ndie mafanya maamuzi mkuu hata kama nitashirikiana na watu wengine bado nitakua ndie mtoa maamuzi mkuuu kwani mimi ndie niliebeba maono makubwa ya biashara.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Maamuzi yoyote yale hufanywa na kiongozi mkuu, baada ya kuchakata maono ya wanakamati.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Asante ni kweli kabisa ni Muhimu sana taasisi kuwa na Maamuzi ya kwa mtu mmoja. Kuna usemi una sema ni bora kuongozwa na generali mmoja mpumbavu kuliko kuwa na majemedali wawili waelevu
LikeLike
Kabisa,
LikeLike
Nahakikisha kila wakati nipo kwenye nafasi ya kufanya maamuzi bora.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kwa kuwa mimi ndio mmiliki wa Biashara nitakuwa muamuzi wa mwisho
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
kujifunza na kufanya maamuzi yaliyo bora ili kufanya biashara ikue
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kila mtu akiwa msemaji kwenye biashara hakuna mwelekeo utakaochukuliwa.
Dereva ni mmoja, waswahili walisema, manahodha wengi, chombo huenda mrama.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Hilo liko wazi kabisa.
LikeLike
Sitajificha nyuma ya ushauri na mawazo ya wengine kuepuka kufanya maamuzi muhimu Kwa ukuaji Wa biashara, nihakikisha najitoa kujifunza,kubobea na kuliekewa eneo langu Kwa kina Ili kufanya maamuzi yote makubwa ya biashara yangu.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Lazima kuwe na mtu wa mwisho katika kufanya maamuzi ambaye ana taarifa za kutosha na anayewajibika kwa maamuzi hayo.
LikeLike
Watu hukimbia maamuzi kuepuka uwajibikaji.
LikeLike
Japo ntashirikisha wengine,lakini linapokuja suala la kufanya maamuzi,muamuzi wa mwisho nitabaki kuwa mimi,kwani mimi ndiyo ninayejua kwa hakika wapi nataka kufika.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kwenye biashara yangu sitaruhusu mtu anifanyie maamuzi,kama kiongozi nitakuwa mtoa maamuzi ya mwisho, Asante sana kocha kwa somo hili, maana hata ndani ya familia lazima awepo mtoa maamuzi ya mwisho.
LikeLike
Bila mfanya maamuzi mmoja hakuna kitakachoamuliwa.
LikeLike
Kama kiongozi mkuu wa biashara ya sikiliza mawazo mba li mbali lakini fanyia kazi mawazo Bora
Asanante
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Nimeelewa Kuwa Maamuzi Bora Ni yake yanayofanywa na mtu mmoja mwenye uelewa wa kutosha kuhusu kile anachokifanyia maamuzi. Anaweza kuchukuwa maoni ya wengine lakini ana uhuru wa kuamua kinachofaa si kwa lengo la kuwaridhisha wengine
Nitajifunza na kuielewa kwa kina biashara yangu ili nifanye maamuzi Bora.
Asante
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kama Ceo nitatatfuta maarifa mengi ili niweze kufanya maamuzi sahihi ….
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Naendelea kujinoa ili nifanye maamuzi Bora mara zote
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kila wakati napaswa kuwa kwenye nafasi ya kufanya maamuzi bora kwa ajili ya biashara.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Sisi viongozi wa biashara ndiyo watu sahihi wa kufanya maamuzi yote makubwa kwenye biashara.
Hivyo tunapaswa kuhakikisha kila wakati kuwa kwenye nafasi nzuri ya kufanya maamuzi bora na yenye tija.
Ahsante sana Kocha.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Ni kweli chukua maamuzi na chakata na na ukimaliza chukua maamuzi kama mbeba maono na tena ni vema ufanye kwa kukosea ili ujifunze
LikeLike
Kabisa, unajifunza mengi kwa kukosea.
LikeLike
Asante Sana Kocha
Sisi viongozi wa biashara ndiyo watu sahihi wa kufanya maamuzi yote makubwa kwenye biashara.
Hivyo tunapaswa kuhakikisha kila wakati kuwa kwenye nafasi nzuri ya kufanya maamuzi bora na yenye tija.
Maneno haya yamebea commitment kubwa Sana kwenye swala la kufikia uamuzi mkubwa kwenye biashara
LikeLike
Hakika.
LikeLike