3036; Ndiyo ni Hapana kubwa.
Rafiki yangu mpendwa,
Wakati tupo kwenye msimu wa HAPANA, tukumbushane jambo muhimu sana kuhusu NDIYO na HAPANA.
Unaposema HAPANA kwenye kitu kimoja, unakuwa umekikataa kitu hicho kimoja tu.
Hilo linakupa fursa ya kuweza kuangalia mambo mengine mazuri yanayoendana na kile unachofanya na kuweza kuyasemea NDIYO.
Kwa maana hiyo basi, kusema HAPANA kunakuacha ukiwa huru zaidi.
Unaposema NDIYO kwenye kitu kimoja, unakuwa umekikubali kitu hicho kimoja, lakini pia unakuwa umevikataa vitu vingine vingi zaidi.
Kwa kusema NDIYO unakuwa umezikataa fursa nyingine nzuri zaidi zinazoendana na kile unachofanya.
Kwa kuwa muda unaoweka kwenye kile ulichosemea NDIYO, ni muda ambao huwezi kuupeleka kwenye kitu kingine.
Kwa maana hiyo basi, kusema NDIYO ni sawa na kusema HAPANA kubwa.
Utakuwa salama zaidi kwa kutumia HAPANA kuliko ndiyo.
Kwa sababu hata ukikosea, kwenye hapana una nafasi ya kujirekebisha, maana unakuwa umekataa kimoja tu, unaweza kusema ndiyo kwenye kingine.
Lakini ukikosea kwenye NDIYO, unakuwa umefunga milango mingi, huwezi kufanya mengine kwenye kipindi hicho kimoja.
Kuwa makini sana na matumizi yako ya NDIYO na HAPANA.
Ni bora utumie hapana zaidi kuliko ndiyo.
Nasisitiza sana hili kwa sababu kuna watu wengi huwa wanahofia kusema HAPANA kwa kuona watakosa fursa nzuri.
Mwishowe wanajikuta wamenasa kwenye fursa mbovu na kukosa fursa nzuri zaidi zinazokuwa zimekuja.
Richard Branson amewahi kusema fursa ni kama daladala, ukikosa moja, kuna nyingine inakuja.
Na mimi naongeza kwa kusema, ni bora ukose daladala moja, kuliko uipande wakati haiendi kule unakotaka kwenda.
Kwani nauli uliyonayo ni ya safari hiyo moja tu, ukishaitoa hutaweza tena kupata daladala nyingine.
Ni bora useme HAPANA kwenye fursa usiyokuwa na uhakika nayo na uikose hata kama umekosea, kuliko useme NDIYO na uipate na iwe siyo sahihi kwako.
Kwa kusema NDIYO kwa fursa moja isiyo sahihi, unakuwa umesema HAPANA kwa fursa nyingi sahihi kwako.
Ni muhimu sana kuzijua rasilimali tulizonazo kwa uhaba na kuzilinda sana.
Muda, nguvu na umakini wetu, ni vitu ambavyo hupaswi kukosea kuvitoa au kuviwekeza kwenye kitu.
Ndiyo unaweza kuja kukataa chochote baadaye, lakini utakuwa umejiingiza kwenye migongano isiyokuwa na tija.
Maana kusema NDIYO halafu baadaye uje useme HAPANA kwa kitu ambacho tayari ulishakikubali kunafanya watu wakuone mbabaishaji na usiyeaminika.
Watu watakuamini na kukuheshimu kwa kusema HAPANA tangu awali kuliko ukianza kwa kusema NDIYO halafu ukaja kusema HAPANA.
Unapowaambia watu hapana tangu awali wataumia, lakini unakuwa hujawapotezea muda kwa kuwapa matumaini yasiyo sahihi.
Hilo litawafanya wakuheshimu.
Lakini ukiwaambia watu NDIYO, kwanza unakuwa umewapa matumaini na wanaweka mategemeo makubwa kwako.
Unapokuja kugeuka na kusema HAPANA, unavunja matumaini na mategemeo wanayokuwa wameweka kwako.
Hilo siyo tu litawachukiza, bali pia litawafanya wakudharau na kutokukuamini. Wakati mwingine hawatakuwa na imani na mambo unayoahidi, hata kama unayamaanisha kweli.
Sema HAPANA zaidi ya unavyosema NDIYO.
Ni salama kukosea kwenye HAPANA kuliko kukosea kwenye NDIYO.
Linda sana rasilimali zako muhimu zisipotee hovyo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ndiyo ni hapana kubwa.
LikeLike
Unafunga mengi kwa kusema ndiyo.
LikeLike
Ahsante sana kocha, nitasema hapana zaidi kwenye daladala zote ambazo haziendi kule ninakoelekea kwani nauli yangu ni ya daladala moja tu.
LikeLike
Huo ndiyo ukweli.
LikeLike
Hapana zangu zinapaswa kuwa nyingi kuliko ndio.
LikeLike
Kinyume na hapo hutoboi.
LikeLike
Nitakua makini kwenye ndio na Hapana kwa kuhakikisha nazitumia sehemu sahihi
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante sana Neno HAPANA lina nguvu zaidi na kukupa Uhuru zaidi.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ni salama kukosea kwenye hapana kuliko kukosea kwenye ndio.
Asante kocha.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante kocha,Hapana inakuweka huru.kuliko kusema ndio baadae ukabadilisha kwa kusema hapana.hivyo hapana ndo njia kuu.
LikeLike
Ni bora uanze na HAPANA halafu ufuate na ndiyo kuliko kuanza na NDIYO halafu kufuata hapana.
LikeLike
Hapana ni uhuru zaidi kuliko ndio. Watanzania wengi tunakubali kwa kusema Ndio lakini hakuna commitment ya ukweli, najifunza kusema hapana nibaki na mambo muhimu
LikeLike
Kweli, wengi wanakwama sana hapo kwenye ndiyo za mdomoni.
LikeLike
Hapana itaniweka huru.
LikeLike
Kweli.
LikeLike
Ahsante Sanaa kocha, nitasema HAPANA nyingi kuliko NDIYO nyingi zenye hatari zaidi
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kusema HAPANA inakupunguzia lawama na watu, kwa mfano, watu wanaokupa KADI za michango ya harusi, ukisema hapana mwanzo ataumia lakini atakuja kuelewa lakini ukichukua KADI na kusema ndiyo halafu uje useme hapana baadaye utaonekana mnafiki.
Chora mstari wa ndiyo na hapana.
LikeLike
Mstari unatakiwa kuchorwa kwa wino mkali ili usifutike.
LikeLike
Najiweka sehemu salama na kwenye nafasi ya kuheshimiwa na kuaminiwa Kwa kusema hapana zaidi ya ndio …nokikosea hapana moja nimekosa kimoja tuu.
Nikisema NDIO kimakosa nimefunga milango ya fursa nyingi nzuri.
Asante Kocha
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Sema hapana zaidi ya unavyosema ndio
Asante
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ndio nyingi zinatutoa kwenye ramani ya mafanikio yetu, nitasema Hapana zaidi kutimiza ndoto zangu.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ni kweli hapana lina nguvu ya kuweza kuja kubadilika mbele lakini ndiyo ikibadilika kuwa hapana inashusha heshima yako na kuonekana hueleweki na mbele utakosa fursa nzuri kwa kua huaminiki ni rahisi kubadilika
LikeLike
Huu ni ukweli ambao wengi huwa hawapati nafasi ya kuujua.
LikeLike
Nimejifunza kuwa Nikisema hapana nakuwa na uhuru zaidi.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Asante sana kocha kwa makala mazuri kwa Maneno yangu mara mingi nitatumia neno hapana
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Nitaendelea kuwa makini ktk matumizi ya maneno HAPANA na Ndiyo,ni bora kusema hapana mara nyingi.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitasema hapana nyingi hata kama itaniumiza.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
small yes it is a BIG NO
LikeLike
Sure.
LikeLike
Watu watakuamini na kukuheshimu kwa kusema HAPANA tangu awali kuliko ukianza kwa kusema NDIYO halafu ukaja kusema HAPANA.✍️
LikeLike
Huo ndiyo ukweli.
LikeLike
Sema hapana zaidi ya unavyosema ndiyo
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
LikeLike
Tukae humu.
LikeLike
Hapna zinapaswa kuwa nyingi na ndiyo kidogo
LikeLike
Kabisa, kanuni ya demand and supply.
LikeLike
Asante sana, nitayaishi maisha ya kusema HAPANA mara nyingi kuliko kusema NDIO
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike