3037; Uwajibikaji haukwepeki.
Rafiki yangu mpendwa,
Mafanikio ya aina yoyote ile kwenye maisha huwa yanaambatana na uwajibikaji.
Ni uwajibikaji wa hali ya juu sana ndiyo unaozalisha mafanikio makubwa ambayo watu wanayapata kwenye maisha yao.
Mafanikio pia yanategemea sana watu ambao mtu anaambatana nao.
Kwa sababu hakuna mtu anayeweza kufanya kila kitu peke yake, watu wanahitajika sana katika kukamilisha majukumu mbalimbali yanayozalisha mafanikio.
Sasa basi, kila panapohusika watu na uwajibikaji nao unahusika.
Unapaswa kuwawajibisha watu ambao unajihusisha nao kwenye kila eneo la maisha yako.
Kama utashindwa kuwawajibisha watu unaojihusisha nao, wewe ndiye unaishia kuwajibika kwa watu hao.
Utaishia kubeba mzigo mkubwa wa watu ambao watakuwa kikwazo kwako kufikia mafanikio unayoyataka.
Watu lazima wawajibishwe ili kutekeleza yale wanayopaswa kutekelezwa.
Uwajibikaji ndiyo unaowasukuma watu kuacha uvivu na uzembe na kufanya.
Kwa asili sisi binadamu ni wavivu na wazembe, hatufanyi kitu chochote mpaka pale inapokuwa kuna madhara kwa kutokukifanya.
Ndiyo maana watu husubiri mpaka tarehe za mwisho kuchukua hatua fulani wanazopaswa kuchukua.
Hiyo ina maana kama kusingekuwa na tarehe za mwisho, kuna wengi wasingefanya kabisa.
Hivyo ndivyo ilivyo kwenye uwajibikaji,
Kama huwezi kuwawajibisha watu unaojihusisha nao, hakuna kitakachowasukuma kufanya.
Na kama watu hawana msukumo wa kufanya, wanakuwa mzigo kwako.
Unaishia kuwajibika kubeba mzigo huo wa watu au hata kuachana nao.
Ndiyo maana tunasema uwajibikaji haukwepeki.
Ni uchague kuwawajibisha watu au uwajibike wewe mwenyewe.
Unawajibika kuwawajibisha watu au utawajibika wewe mwenyewe.
Hakuna uwajibikaji rahisi,
Kuwawajibisha watu kunakutaka uwasukume kutoka kwenye mazoea yao na wafanye vitu vya tofauti. Wengi hawatapenda hilo. Hivyo kama utataka kuwafurahisha, hutawawajibisha na hivyo yanayopaswa kufanywa hayatafanyika.
Kuwajibika wewe mwenyewe ni kazi mara mbili, ufanye kazi yako mwenyewe halafu ufanye na kazi ya wengine ambao umeshindwa kuwawajibisha.
Ni muhimu sana unaposhirikiana na watu wengine kukubaliana tangu awali ni mambo gani wanayopaswa kutekeleza.
Kisha wewe kuwawajibisha kwenye kutekeleza kama mlivyokubaliana, bila ya kupokea sababu zozote zile.
Uwajibikaji ndiyo unawaweka watu kwenye kile wanachopaswa kufanya.
La sivyo ni rahisi sana kuyumbishwa na mambo mengi mapya yanayokuwa yanajitokeza kila mara.
Wawajibishe au utaeajibika kwao.
Hakuna namna unaweza kukwepa uwajibikaji.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante sana Kocha. Nitawajibika mara zote
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Nitawawajibisha wafanyakazi kwani kinyume chake nitawajibika mara 2
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante kocha
Ili kuepuka kufanya kazi mara mbili yanipasa kuwawajibisha ninaofanya nao kazi ili waweze kutekeleza majukumu tuliyokubaliana.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Ahsante sana kocha, nitawawajibisha wale wote ambao nafanya nao biashara kwaajili ya kuhakikisha matokeo ynapatikana.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante sana kocha kwa makala mazuri ya uwajibikaji nikweli uwajibikaji haukwepeki Mara mingi hili nalitumia kwenye biashara yangu yaani nisipo wapa majukumu Wasaidizi wangu ina maana mimi ndiyo nitawajibika kwa hiyo uwajibikaji haukwepeki
LikeLike
Hakika
LikeLike
Hakuna uwajibikaji rahisi ni hakika katika hilo Asante sana kocha
LikeLike
Karibu
LikeLike
Uwajibikiaji ndio kunaweweka watu kufanya kile kinachowaweka kufanya
Wawajibishe watu ili waweze kufanya
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kutokuwawajibisha wengine ni mzigo wako WA wajibu.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante kocha,ni muhimu kwa kila mtu kujua majukumu yake,na hasipoyatekeleza lazima hawajibishwe.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Nikweli lazima ukubaliane na moja kuwawajibisha au kuwajibishwa
LikeLike
Hakika
LikeLike
Hakuna uwajibikaji rahisi,
Kuwawajibisha watu kunakutaka uwasukume kutoka kwenye mazoea yao na wafanye vitu vya tofauti. Wengi hawatapenda hilo. Hivyo kama utataka kuwafurahisha, hutawawajibisha na hivyo yanayopaswa kufanywa hayatafanyika.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Niwawajibishe au niwajibike mimi.
LikeLike
Ndiyo hivyo.
LikeLike
Ukiweza kujiwajibisha wewe mwenyewe ni rahisi kuweza kuwawajibisha wengine pia.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Inaanza na wewe mwenyewe.
LikeLike
kocha Makirita Amani,anatuwajibisha wana kisima cha maarifa jamii ya tofauti Tz,na klabu za kisima cha maarifa na BM.
LikeLike
Bila uwajibikaji KISIMA CHA MAARIFA hakitaweza kuwepo.
LikeLike
Nitachagua kuwawajibisha watu.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Hakuna namna naweza kwepa uwajibikaji
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Mara zote nitakaposhilikiana na wengine , ni muhimu tukakubaliana Mambo yanayopaswa kutekerezwa Kisha
Mimi niwawajibishe kutekereza Kama tulivyokubaliana
bila kukubari sababu zozote.
LikeLike
Sahihi.
LikeLike
Ni Muhimu kuwawajibisha watu kabla ya kuwajibishwa wewe
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Sina namna ya kukwepa uwajibikaji hasa ktk safari ya mafanikio iliyopo mbele yangu.asante kocha.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nawawajibisha Ili kuwasukuma kufanya
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kama utashindwa kuwawajibisha watu unaojihusisha nao, wewe ndiye unaishia kuwajibika kwa watu hao.✍️
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ni kweli bila kuwawajibisha watu watakuwa hawafanyi vizuri
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nitaambatana na watu sahihi ili nipate mafanikio makubwa.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike