3067; Imani, Ujuzi, Kazi.
Rafiki yangu mpendwa,
Kuna kanuni chache sana za mafanikio.
Lakini zimekuwa zikipinduliwa pinduliwa na kuishia kuonekana kama ni nyingi na ngumu.
Hilo huwa linawakatisha tamaa wengi na kushindwa kufanikiwa.
Maneno matatu yaliyopo hapo juu, siyo mageni kuyasikia.
Na hata maana za maneno hayo unazijua vizuri kabisa.
Lakini leo nataka niyapindue pindue maneno hayo na uone jinsi yalivyo mafiga matatu muhimu ya kupata chochote unachotaka kwenye maisha yako.
IMANI.
Kupata chochote unachotaka kwenye maisha yako, kunaanza na imani kali sana na isiyoyumbishwa kwamba utapata kile unachotaka.
Hata ukiwekewa bastola kichwani na kuambiwa ukiamini kwenye kile unachotaka risasi inafyatuka na usipoamini haifyatuki, wewe umaamini bila ya shaka.
Unatakiwa ujiamini sana na uamini sana kwenye kile unachotaka kiasi cha watu kukuona umechanganyikiwa.
Na kipimo kizuri cha imani yako kwako na kwa ndoto zako ni watu kuona umechanganyikiwa.
Yaani kama hakuna watu wana wasiwasi na wewe juu ya utimamu wako wa akili, hujiamini na wala huamini kwenye ndoto zako vya kutosha.
UJUZI.
Ili upate chochote unachotaka kwenye maisha yako, kwanza lazima ujue kwa hakika nini unachotaka, kisha ujue jinsi unavyoweza kukipata.
Lazima ujue kwa hakika ni hatua zipi unazopaswa kuchukua ili upate unachotaka.
Na hapa huhitaji kuja na uvumbuzi wowote mpya.
Badala yake ni kuangalia yale waliyofanya ambao wameshapata unachotaka na wewe kuyafanya.
Mafanikio huwa yanaacha alama.
Ili kufanikiwa, angalia yale waliofanikiwa wanafanya na wewe uyafanye.
Huo ni ujuzi muhimu sana ambao usipokuwa nao utakwama sana.
KAZI.
Nidhamu kali ya kazi inahitajika sana ili mtu uweze kupata kile unachotaka.
Kufanya kazi kwa juhudi kubwa hakukwepeki kama mtu unayataka mafanikio makubwa.
Kazi ndiye rafiki wa kweli ambaye ukiambatana naye utapata mazuri.
Pamoja na umuhimu mkubwa wa kazi kwenye mafanikio, wengi bado wamekuwa wanajaribu kuikwepa.
Wengi wamedanganyika kwa njia za mkato ambazo zimewapotezea muda na fedha.
Unahitaji kufanyia kazi vitu vyote vitatu kwa pamoja ndiyo uweze kupata matokeo makubwa na bora sana.
Hayo ndiyo mafiga matatu ya kupika mafanikio, likikosekana hata moja, inaathiri sana mafanikio ambayo mtu anaweza kuyapata.
Kama mtu atakuwa na UJUZI na kuweka KAZI ila akakosa IMANI, matokeo atakayopata yanakuwa madogo ukilinganisha na ambayo angepata kama angekuwa na vyote vitatu.
Kama mtu atakuwa na IMANI na UJUZI ila akakosa NIDHAMU YA KAZI, ataonekana mwenye ahadi hewa, kwa sababu chochote anachoahidi hakikamiliki.
Kama mtu atakuwa na IMANI na NIDHAMU YA KAZI lakini akakosa UJUZI, atahangaika sana na kuchoka, lakini kila wakati atakuwa anabadili kile anachofanya. Hapa ndipo penye wale wa kubadili fursa kila wakati, ambao leo watakuja na fursa fulani, ila kesho wataachana nayo kabisa na kuwakuta wakinadi fursa nyingine ya tofauti.
Unahitaji mafiga yote matatu ili kupika mafanikio makubwa.
Safari ya ubilionea.
Kwanza lazima UAMINI bila ya shaka yoyote kwamba utakuwa bilionea.
Imani yako inapaswa kuwa kali sana kiasi cha watu kuona kama umechanganyikiwa hivi.
Yaani imani yako inapaswa kuwa kama vile umeingiwa na pepo la aina fulani.
Usipoamini, huwezi kudumu kwenye hii safari kwa muda mrefu.
Pili UJUE mchakato kamili wa kufika kwenye ubilionea. Jua kwa hakika kila unachopaswa kufanya ili uweze kufikia ubilionea.
Na kwa bahati nzuri sana, tayari mchakato kamili tunao, ambao umeeleza kila hatua za kuchukua na jinsi ya kuzichukua.
Safari yetu ya ubilionea ni kupitia kujenga BIASHARA na kufanya UWEKEZAJI.
Kwenye biashara tunajenga MFUMO, TIMU na WATEJA.
Huku kwenye uwekezaji tukifanya kwenye MASOKO YA MITAJI na MALI.
Hatua za kuchukua kwenye kila eneo zimeelezwa kwa kina kwenye vitabu BILIONEA MAFUNZONI na CHUO CHA MAUZO.
Tatu lazima uweke KAZI kwa nidhamu ya hali ya juu sana.
Kazi inayohitajika kwenye hii safari ni nje kabisa ya mazoea.
Masaa ya kufanya kazi kwa siku ni mengi (angalau 16) na siku za kufanya kazi kwa wiki ni nyingi (6 mpaka 7) huku wiki za kazi kwa mwaka zikiwa zisizopungua 50 kati ya wiki 52 za mwaka.
Kwenye miaka sasa, siyo chini ya miaka 10.
Kama kwa kusoma hizo namba kwenye ufanyaji kazi unaona ni kitu kigumu, upo sahihi, siyo rahisi, hivyo lazima ujitoe sana.
Ingekuwa rahisi kila mtu angekuwa ameshaupata ubilionea na ungekosa thamani.
Mafiga matatu; IMANI, UJUZI, KAZI, jijengee yote kwa uhakika ili uweze kupika chakula kitamu ambacho ni mafanikio unayoyataka kwenye maisha yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Imani, ujuzi, kazi.
LikeLike
Mafiga matatu.
LikeLike
Imani,ujuzi,kazi….
ukiondoa kimoja hapa vingine vikabaki bado matokeo hayatakua mazuri.Ni vitu muhimu kwenda sambamba vyote
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Mafiga matatu ili kufika ubilionea IMANI,UJUZI NA KAZI.Likikosekana lolote ni changamoto.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nahitaji kuwa na Imani, Ujuzi na kazi ili niweze kufikia safari yangu ya ubilionea.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Imani, ujuzi na kazi.
Natembea navyo vyote kwenye maisha yangu.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Naenda kuimarisha Imani, Ujuzi na kuweka nidhamu kali kwenye kazi ili niweze kufikia malengo yangu makubwa niliyojiwekea. Asante sana kocha kwa mafiga haya ya kupikia mafanikio.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ili kufikia ubilionea lazima tuwe na mafiga matatu.
IMANI, UJUZI NA KAZI ni mafiga matatu ya kupika mafanikio ( matokeo makubwa na bora sana). Asante sana! Uungwana ni vitendo!
LikeLike
Hakika, tukae humo.
LikeLike
Imani, Ujuzi na Kazi
Ndio mpango mzima
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Imani,Ujuzi kazi lazima ziende sambamba kitu Cha msingi zaidi
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Vitu vya kujenga Imani Ya ninachokifanya, ujuzi na kazi kaazii
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Jiamini sana na uamini sana kwenye kile unachotaka kiasi cha watu kukuona umechanganyikiwa.
Mafiga matatu IMANI,UJUZI na KAZI
Ukifanyia kazi vitu hivi vitatu lazima utafanikiwa
Asante sana
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Imani,ujuzi,na kazi kama bilionea mtarajiwa ni sehemu ya maisha yangu ktk kupambana.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Mafiga matatu, Imani,ujuzi kazi
Naamini bila ya shaka yoyote,najengo ujuzi na Ubobevu na weka kazi Ili nifanikiwe.
LikeLike
Safi sana
LikeLike
Nimeyaelewa haya mafiga kwa ukaribu zaidi kwamba yote yanafanya kazi na haiwezekani kwa kwa pamoja na ni lazima watu wakuone umechanganyikiwa kwa hapana nyingi na pengine kutokushirikiana nao wewe ukipambana na lengo lako ambayo kwao wanaona ni gumu hutaweza kulifikia
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kwa waliozaliwa mjini huenda wengi hawajui mafiga matatu maana yake nini. Kwa sisi tuliozaliwa vijijini na kushuhudia namna watu wanavyopika chakula kwa kuni kwa kutumia mafiga matatu tumeelewa vizuri sana kielelezo Cha mafiga matatu. Huwezi kupika chakula kwa mafiga mawili au moja. Hivyo huwezi kufanikiwa bila kuwa na imani, ujuzi na kuweka kazi.
LikeLike
Asante sana, kweli bwana, mtu asiye na picha ya mafiga na kupika, anaweza kupata ugumu kuelewa.
Na iko wazi kabisa, utatu huu ni muhimu sana.
LikeLike
Imani + Ujuzi + Kazi = NINAPATA CHOCHOTE NINACHOKITAKA
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Mafiga matatu ya kuivisha mafanikio makubwa.
IMANI+UJUZI+KAZI=MAFANIKIO MAKUBWA.
Asante sana Kocha.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Nitajenga imani,nitatafuta ujuzi na kuweka kazi kubwa ili kuupata Ubilionea….
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nidhamu kali ya kazi inahitajika ili mtu apate anachotaka.
LikeLike
Kweli.
LikeLike
Imani, ujuzi, na kazi nazingatia hayo kia siku kama nataka kupata chochote ninachotaka kwenye maisha yangu.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Imani, ujuzi, na kazi nazingatia hayo kia siku kama nataka kupata chochote ninachotaka kwenye maisha yangu. Asante sana.
LikeLike
Ili uweze kupata mafanikio makubwa kwa Chochote unachotaka ni lazima utumie mafiga matatu ambayo ni
IMANI __ UJUZI__KAZI
Kama litakosekana figa figa moja kati ya hayo matatu basi mafanikio yataathilika.
Asante kocha
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ingekuwa rahisi kila mtu angekuwa ameshaupata ubilionea na ungekosa thamani.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Imani, ujuzi na kazi ndiyo mafiga ya jufikia ubilionea
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
nitaweka mbele imani ujuzi na kazi ili nifanikiwe
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike