3072; Usilale.
Rafiki yangu mpendwa,
Tuna maadui wengi sana ambao wanapambana kwa kila namna kutuzuia tusipate mafanikio makubwa tunayoyataka.
Maadui wanaokuwa na nguvu sana siyo wa nje, bali wale wa ndani yetu.
Hao ni maadui wanaokuwa na nguvu kwa sababu wanatujua kiundani.
Uvivu, uzembe na mazoea ni maadui ambao wengi hawajui madhara yao kwenye mafanikio yao.
Wamekuwa wanafanya kazi kwa chini chini kuhakikisha mtu hapati mafanikio makubwa anayoyataka.
Halafu kuna adui mwingine mkubwa sana ambaye amekuwa kikwazo sana.
Adui huyo ni kulala.
Adui kulala tunayemzungumzia hapa, siyo kule kulala kitandani, bali kulala kurudi nyuma pale mtu anapokuwa ameshapanga kusonga mbele.
Ni mara ngapi umesoma kitabu au kupata mafunzo au wazo lolote na kujiambia kuanzia sasa nakwenda kubadilika?
Unajiambia utaamka mapema, utapangilia muda wako wote na utaweka juhudi kubwa kwenye kazi bila kupoteza muda na kuahirisha mambo.
Siku chache za mwanzoni unatekeleza kama ulivyopanga.
Lakini siku siyo nyingi unakuwa umerudi iwenye mazoea yako ya nyuma.
Hapo ndiyo unakuwa umerudi kulala, baada ya kuwa umeamka kwa muda mrefu.
Leo tunakwenda kujifunza kanuni rahisi sana ambayo itakuzuia usirudi kulala pale unapokuwa umeamka.
Kanuni hiyo ina hatua muhimu tatu za kuzingatia mara zote ili mtu usirudi kulala.
Hatua ya kwanza ni hamasa ambayo ndiyo inakuamsha.
Sisi binadamu ni viumbe wa kihisia na hivyo maamuzi yetu yote huwa tunayafanya kwa kusukumwa na hisia.
Mabadiliko yoyote kwenye maisha yetu huwa yanaanzia kwenye hamasa ambayo mtu unakuwa umepata.
Inaweza kuwa hamasa chanya ya tamaa ya kupata vitu fulani vizuri au hamasa hasi ya hofu ya kukosa au kupoteza vitu vizuri.
Hatua ya pili ni nidhamu ambayo ndiyo inakufanya uendelee kuwa macho.
Baada ya hamasa kukuamsha, nidhamu ndiyo inayokufanya uendelee kukaa kwenye yale uliyopanga kufanya.
Kukosekana kwa nidhamu imekuwa chanzo kikubwa cha watu kurudi kulala muda mfupi baada ya kuamshwa na hamasa.
Wengi hutegemea hamasa ndiyo iwasukume kila wakati, kitu ambacho hakipo.
Hamasa inawasha tu moto, nidhamu ndiyo inauchochea moto huo.
Kukosa nidhamu kumekuwa kikwazo cha wengi kukaa kwenye kitu kwa muda mrefu.
Hatua ya tatu ni kusudi ambalo ndiyo linakuzuia usirudi kulala.
Kusudi linakupa msukumo mkubwa sana wa kuendelea hata pale mambo yanapokuwa magumu na kuonekana kushindwa.
Kadiri kusudi ambalo mtu anakuwa nalo linakuwa kubwa, ndivyo msukumo wa kuendelea kulipambania unavyokuwa mkubwa pia.
Huwa kuna kauli inayosema ukiwa na KWA NINI KUBWA, utaweza kuvumilia chochote ili kuitimiza.
Wengi huwa wanapata hamasa ya kubadilika, ila wanakuwa hawajui kwa nini wanadilike.
Wanakuwa hawajajua kwa nini wateseke na mabadiliko wanayoanzisha.
Hivyo wanapokutana na mateso, huwa wanaacha haraka sana, wanarudi kulala.
Kusudi ni muhimu sana kukuzuia usirudi kwenye uvivu, uzembe na mazoea ya nyuma.
Kwa zama tunazoishi sasa, hakuna uhaba wa hamasa.
Hamasa zinapatikana kwa wingi na kila mahali.
Lakini pamoja na wingi huo wa hamasa, bado watu wengi hawafanikiwi.
Na sababu ni kukosekana kwa vitu hivyo vingine viwili.
Watu wanakosa nidhamu kali sana ya kuamua na kufanya kwa msimamo bila kuacha.
Na zaidi, wanakosa kusudi la kuwasukuma kuendelea na mabadiliko licha ya magumu wanayokabiliana nayo kwenye safari.
Haya yote unayajua, ila huenda hujawahi kuyaunganisha kwa pamoja hivi na ukaona nguvu yake.
Hivyo yalete pamoja na kila siku hakikisha unayafanyia kazi.
Hamasa inakuamsha kutoka kwenye usingizi wa uzembe, uvivu na mazoea.
Nidhamu inakufanya uendelee kuwa macho, kwa wakati wote kuendelea na mabadiliko uliyoanzisha.
Na kusudi linakuzuia usirudi kwenye usingizi wa uzembe, uvivu na mazoea hasa pale unapokutana na magumu na changamoto mbalimbali.
Kama hutaki kulala kwenye hii safari ya mafanikio, hakikisha unatumia HAMASA, NIDHAMU NA KUSUDI kubadilika na kudumu kwenye mabadiliko hayo bila kurudishwa nyuma na kitu chochote.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ni rahisi mtu kurudi kulala kama huna nidhamu, kusudi la kuendelea kufanya.
Ukiamka halafu ukisema ngoja nilale kidogo hapo ndiyo hatari huanzia.
Unapaswa kulipuka kutoka kitandani na kuendelea na KWA NINI KUBWA iliyokutoa kitandani.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kama hutaki kulala kwenye safari hii ya mafanikio hakikisha unatumia HAMASA, NIDHAMU na KUSUDI kubadilika na kudumu kwenye mabadiliko hayo
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nitamtumia hamasa, nidhamu na kusudi Kuhakikisha nasogea melee katika safari yangu ya mafanikio
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante sana kocha kwa kutukumbusha haya matatu muhimu.
LikeLike
Karibu.
LikeLike
HAMASA, NIDHAMU NA KUSUDI Ndio misingi ya mafanikio ktk safari yetu ya Ubilionea. Asante sana Kocha!
LikeLike
Karibu
LikeLike
Kama hutaki kulala kwenye hii safari ya mafanikio, hakikisha unatumia HAMASA, NIDHAMU NA KUSUDI kubadilika na kudumu kwenye mabadiliko hayo bila kurudishwa nyuma na kitu chochote.
Asante sana
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Hamasa nidham na kusudi
LikeLike
Humo.
LikeLike
HAMASA, NIDHAMU& KUSUDI
LikeLike
Tukae humo.
LikeLike
Nitatumia hamasa, nidhamu na kusudi ili kuzuia kurudi kulala baada ya kuamka
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Ni kweli kabisa hamasa pekee haitoshi kukufikisha kwenye mafanikio makubwa.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Hamasa nidhamu na kusudi vitaondoa usingizi wa kuto elekea katika mafanikio yangu makubwa.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Hamasa, nidhamu na kusudi ndio zinazotufanya nikose usingizi na kupigania ndoto zangu
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Asante sana kwa somo la leo.
Naahidi kutokulala,bali ni kukaa macho mpaka kieleweke.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante kwa kutukumbusha haya matatu kocha yaani HAMASA, NIDHAMU na MUSUDI,ni kweli angalia asbh unavyokuwa unaamka na unavyoingia kwenye kipindi ni vitu 2 tofauti muhimu ni kujitoa na kuwa na Nidhamu Kali ya kuamua na kufanya.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Typing error “HAMASA, NIDHAMU na KUSUDI”
LikeLike
Nikishahamasika, nitahakikisha nidhamu Kali. Kusudi langu litatokana na kwanini kubwa.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante kocha,Nitajitahidi kuwa na Hamasa,Nidhamu na Kusudi ili kufikia ndo yangu.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ukiwa na kwanini kubwa utaweza kuvumilia chochote ili kuitimiza.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Uwe na kwanini kubwa.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ni kweli hamasa ni chanzo cha kusisimka lakini siyo ya muendelezo ni lazima uwe na lengo kuu na kuwa na msimamo wa kufanya bila kurudi tena kulala na ukiwa na KWANINI KUBWA HAKUNA WA KUKUZUIA
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nitajipa hamasa kila siku kuwasha moto,na nitakua na muongozo wa nidhamu kali na kuwa na ndoto ya kile nachotaka kwa maisha yangu.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitatumia hamasa,Nidhamu na kusudi kufanya kile nilichoamua kufanya.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante Kocha, nitatumia hamasa, nidhamu na kusudi kuhakikisha silali kwenye safari yangu ya mafanikio.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Hamasa, nidhamu na kusudi ni vitu muhimu kuifanyia kazi kwa pamoja
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Hamasa inakuamsha kutoka usingizini
Nidhamu inakufanya uendelee kuwa macho
Kusudi linakufanya usirudi kwenye uzembe na uvivu
Asante kwa kutukumbusha hili
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Ni kweli kocha kuwa na kwanini kubwa pia itakupa nidhamu na kukufanya usirudi kulala
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
uzembe, uvivu na mazoea ni adui namba moja wa mafanikio, nitapambana na maadui hawa mpaka nihakikishe nawashinda.
Makala bora sana hii na inatugusa wengi.
Asante sana Kocha
LikeLike
Vizuri na kila la kheri.
LikeLike