3081; Mambo yasiwe mengi.
Rafiki yangu mpendwa,
Kwa kuwa tunataka sana kufanikiwa kwenye maisha yetu, huwa hatuoni kama sisi wenyewe tunaweza kuwa kikwazo kwenye mafanikio yetu.
Lakini ukweli ni kwamba sisi wenyewe huwa tunakuwa kikwazo kwa mafanikio makubwa tunayoyataka kwa sababu ya mambo kuwa mengi.
Kadiri mtu anavyokuwa na orodha ndefu ya mambo ya kufanya, ndivyo inavyokuwa vigumu kwa mambo hayo kutekelezeka.
Na siyo tu kwa sababu mambo ni mengi hivyo hayapati muda, bali ni mtazamo mzima wa mambo mengi ndiyo unaokuwa kikwazo.
Kwa mambo kuwa mengi kwenye orodha, mtu ni rahisi kuzoea mambo hayo na kudhani yatafanyika tu.
Wengi huona kitendo tu cha kuwa na orodha ndefu ya vitu vya kufanya.
Halafu kuna ile hali ya mtu kuchoka kabla hata hujaanza.
Kwa kuona orodha ikiwa ndefu, mtu unashindwa kuona wapi pa kuanzia, hivyo kukwama na kushindwa kabisa kuhama.
Kingine kinachokwamisha watu kwenye ufanyaji ni masharti yanayokuwa mengi ili mtu afanye.
Hapa mtu anajiwekea vigezo vya kutimiza ili kuweza kuchukua hatua, vigezo ambavyo kwa wingi wake ni nadra sana kukamilika.
Kwa kutokamilika kwa vigezo hivyo, mtu anakwama kuchukua hatua anazopaswa kuchukua.
Kutaka kuwa na maisha yenye mlinganyo kamili ni njia nyingine ya kuruhusu mambo mengi kuwa kikwazo kwa mtu kufanikiwa.
Kwa kuhangaika na kuangalia kama kila kitu kipo sawa, inapunguza nguvu na muda kwenye yale muhimu yanayopaswa kufanywa.
Ukiangalia watu wote ambao wameweza kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yao, kuna kipindi ambapo walipunguza sana mambo kwenye maisha yao.
Walikuwa na kipindi ambacho ratiba yao yote ilikuwa ni wao na kile wanachofanya tu.
Hawakuruhusu kitu kingine chochote kuchukua muda na nguvu zao.
Inapokuja kwenye kitu chako kikuu unachofanya, usiruhusu mambo mengi kukaa kati yako na kitu hicho.
Hakikisha mara zote kitu hicho ndiyo kipaumbele kikubwa na cha kwanza kabisa kwako.
Chukua mfano wa wanariadha wawili.
Wa kwanza utaratibu wake uko hivi; kama nikiwahi kuamka, na nikawa najisikia vizuri, huku hali ya hewa ikiwa nzuri na kuna mtu wa kuambatana nayo basi nitafanya mazoezi.
Wa pili utaratibu wake uko hivi; nawahi kuamka kisha nafanya mazoezi.
Iko dhahiri hapo ya kwamba ni rahisi sana wa kwanza kukwama na kutokufanya kutokana na mambo mengi aliyojiwekea, ni rahisi kwa moja kukwama na kuzuia mengine yote.
Lakini kwa wa pili, nafasi ya kufanya ni kubwa zaidi kwa sababu hakuna mambo mengi ya kuzingatia.
Punguza sana mambo unayohangaika nayo ili uweze kubaki na machache muhimu utakayoyafanya muda wote.
Tupo kwenye msimu wa HAPANA, ambao ukiweza kutumia vizuri neno HAPANA utaepuka mambo mengi sana yanayokukwamisha.
Kati yako na ndoto yako kuu, kupitia kile kikuu unachopaswa kufanya, pasiwe na kingine chochote kinachoweza kukukwamisha.
Ni wewe na kufanya, basi.
Kwa namna hiyo utalazimika kufanya, kwa sababu huna pa kutorokea.
Hebu jaribu kufikiria tu, kama unaamka mapema kila siku na muda wote wa siku yako unauweka kwenye kujenga biashara yako.
Kwa siku nzima unatekeleza majukumu ya kujenga mfumo, timu na kukuza mauzo.
Kwa umakini wako wote kuwa kwenye eneo hilo tu na kutosumbuliwa na mengine mengi, unajiweka kwenye nafasi ya kufanya makubwa na mazuri zaidi.
Ukishajiona kati yako na kufanya kile kinachokufikisha kwenye lengo kuu kuna mambo mengi, jua unajikwamisha mwenyewe.
Anza kutumia neno HAPANA kuondoa mambo hayo ili uweze kubaki na lile lililo kuu peke yake.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Mambo yasiye mengi.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Ni kweli mambo yakiwa mengi na masharti pia mtu anakatatamaa
haraka sana na kukosa pa kuanzia ila ukiwa na vitu vichache utaweza kuwa na uhakika
LikeLike
Kweli
LikeLike
Punguza sana mambo unayohangaika nayo ili uweze kubaki na machache muhimu utakayoyafanya muda wote.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante Kocha kwa msimu huu wa hapana
LikeLike
Karibu
LikeLike
Biashara ndio kipaombele Changu cha kwanza, sitoruhusu kuwa na mambo mengi.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Nitajitahidi kujiepusha na mambo mengi ili nguvu yangu kubwa niiweke kwenye biashara. Asante kocha
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Mambo yasiwe mengi
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Mambo yasiwe mengi baki na lilokuu mbele yako
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante sana Kocha,
Ni Mimi na kufanya, basi!
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Nitasema hapana kwenye mambo yote ambayo siyo ya msingi ili kuweka nguvu zangu zote kwenye biashara
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Punguza sana mambo unayohangaika nayo ili uweze kubaki na machache muhimu utakayoyafanya muda wote.
Asante sana nakubaliana kabisa na wewe
LikeLike
Karibu
LikeLike
Kipaumbele changu ni mimi na kitu changu kikuu cha kufanya,vingine vya katikati ya mimi na kitu changu kikuu HAPANA. Asante Kocha.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Mimi ninaendelea kupunguza au kusema hapana kwa kila eneo ambalo linahusisha sehemu ya maisha yangu ili niweze kupata utulivu, muda, umakini, Raslimali fedha, kwa lengo la kuweza kupata fursa ya kutekeleza mambo yaliyo muhimu kwenye maisha yangu.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante Sana kwa waraka waleo. Mkakati Ni kupunguza Mambo kwa kutumia neno HAPANA ili kufokas. Mambo mengi yanatuchelewesha na kufa masikini
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Naweka muda wangu na umakini wangu kwenye kukuza mauzo ,kujenga timu na kujenga mfumo wa biashara ,mengine yatasubir nikishakamilisha hayo.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Hapana bado Ina nafasi ya kuniokoa na mambo mengi
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante kocha,nitaweka umakini kwenye kitu kimoja kuliko kuwa na mambo mengi yasiyokuwa na tija.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante sana
LikeLike
Karibu
LikeLike
Acha kuwa na mambo mengi.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Mafanikio kwenye biashara yanawezekana kwa kuacha kuwa na mambo mengi yasiyokuwa na mchango wowote kwenye yale tunayofanyia kazi. Umakini na juhudi kubwa zikielekezwa ipasavyo kwenye eneo moja lazima zizalishe matokeo chanya.
Asante sana Kocha.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Ni muhimu kupunguza mambo mengi kwa kutokuweka mashatri mengi.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Iko wazi kabisa ,ukiwa na Mambo mengi ktk siku yako hutoweza kuyakamilisha na Kama utakamilisha basi yatakuwa na ubora wa chini Sana kitu ambacho kitakukwamisha. Jamba muhimu ni kuwapunguza kabisa Mambo ya kufanya ili kuweza kupata mafanikio makubwa. Asante kocha
LikeLike
Karibu.
LikeLike