3092; Kamari yenye ushindi wa uhakika.
Rafiki yangu mpendwa,
Kila mtu anataka ushindi kwenye maisha yake.
Ni hitaji hilo la ushindi ndiyo limekuwa linawasukuma watu wengi kufanya mambo hata yasiyokuwa na tija, ili tu kuona wameshinda.
Tunaona watu wengi wakiwa na ushabiki mkubwa wa michezo mbalimbali. Yote hiyo ni kutaka ushindi.
Na kwenye hiyo michezo, kumeongezeka kitu kingine ambacho kimezidi kuwateka watu kwenye hitaji lao la ushindi.
Kitu hicho ni kamari au kaka wanavyoita kwa lugha ya kuhadaa, michezo ya kubahatisha.
Watu wengi wamekuwa na uraibu na kamari hizo, huku wakipoteza fedha nyingi, lakini hawaachi kwa sababu ya matumaini ya kupata ushindi.
Lakini huo unakuwa ushindi ambao siyo wa uhakika.
Pamoja na kukosekana huko kwa uhakika wa ushindi, bado watu wanaendelea na kamari hizo kwa sababu ya matumaini wanayokuwa nayo, hasa kwa ushindi mdogo waliowahi kupata au kwa kuona ushindi wa wengine.
Leo nataka nikushirikishe aina ya kamari ambayo ushindi ni wa uhakika.
Kamari hiyo unapewa kete mbili uzirushe kwa pamoja, zote zikionyesha namba sita juu, unapata fedha.
Kama zitaonyesha namba nyingine tofauti, hutapata fedha, lakini pia hutapoteza chochote.
Lakini pia unapata nafasi ya kuendelea kurusha hizo kete.
Swali ni je utafanya nini ili uweze kupata fedha nyingi zaidi?
Jibu ni moja, kurusha kete hizo mara nyingi uwezavyo.
Kwa sababu ukipatia unapata fedha, na ukikosea hupotezi chochote, hivyo ukirusha mara nyingi, unajiweka kwenye nafasi ya kupatia zaidi na kuingiza fedha nyingi zaidi.
Sasa fikiria kamari hiyo hiyo, lakini kwa sasa siyo kete, bali wateja unaowafikia ili kuwauzia.
Hiyo ni kamari, lakini yenye uhakika.
Ukimfikia mteja, iwe ni kwa kumtembelea au kwa simu na kumshawishi kununua, kama atanunua utakuwa umeingiza fedha.
Na kama atakataa kununua huingizi fedha, lakini pia unakuwa hujapoteza fedha yoyote ile.
Hivyo swali linakuja tena, unatakiwa kufanya nini ili kuingiza fedha nyingi zaidi kwenye mauzo?
Na jibu ni moja tu, wafikie wateja wengi zaidi.
Mauzo ni kamari yenye uhakika wa ushindi.
Kwa kuwafikia wateja na kuwashawishi kununua, wakikubali unaingiza fedha.
Na wakikataa, hakuna unachokuwa umepoteza.
Hivyo ili kupata ushindi kwa uhakika, unapaswa kuwafikia wateja wengi zaidi.
Kwa nini watu hawachezi kamari hii ya uhakika wa ushindi na isiyo na kupoteza?
Kwa sababu inahusisha kufanya kazi.
Na watu huwa hawapendi kazi,
Badala yake wanataka njia za mkato za kupata fedha.
Na njia hizo za mkato zinaishia kuwakata hata fedha kidogo wanazokuwa nazo.
Wewe epuka njia za mkato na kuwa tayari kuweka kazi, ushindi utakuwa wa uhakika kwako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Mauzo ni kamari yenye uhakika wa ushindi. Epeka njia za mkato na kuwa tayari kuweka kazi na ushindi utakuwa wa uhakika kwako.
LikeLike
Mtapambana na mauzo ili kucheza kamari ya uhakika siyo ya kubahatisha
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Hakika
LikeLike
Hii kamari ya uhakika kushinda maana inahusisha kuweka kazi ambayo ni kitu kigumu kwa wengi
LikeLike
Kweli
LikeLike
Naepuka njia za mkato ,nipo tayari kuweka kazi kubwa ili nipate matokeo ya uhakika.
Asante kocha.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Kamari ni moja tu kuwatembelea na kuwapigia simu wateja wengi zaidi.Nikifanikiwa maana yake nimeuza na kuingiza hela,nikishindwa maana yake hakuna nilichopoteza.
LikeLike
Raha iliyoje
LikeLike
Hivyo swali linakuja tena, unatakiwa kufanya nini ili kuingiza fedha nyingi zaidi kwenye mauzo?
Na jibu ni moja tu, wafikie wateja wengi zaidi.
LikeLike
Wengi zaidi.
LikeLike
Ukiwafkkia wateja wengi na kueleza sera zako ni lazima utaweza kushinda na usiposhinda utapata kumweka jwenye nafasi nzuri ya wewe kushinda baadae
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante sana kocha,Mauzo ni kamari yenye uhakika kwa kuwatembelea na kuwashawishi,wakikubali umewauzia,wakikataa pia hakuna ninachopoteza,
Asante sana pia kwa Neno la Leo.SALAMA NI HATARI NA HATARI NI UHURU “kama pia nilivyosema jumamosi,na leo tumeona kwenye ajira mteja ni mmoja, kwenye biashara kuna namba za kufanyia kazi, lakini kwenye ajira hakuna namba
LikeLike
Sahihi kabisa, bila kuwa na namba unazunguka na kurudi pale pale.
LikeLike
Mauzo ni kamari yenye uhakika na ushindi . Hivyo wafikie wateja wengi zaidi ili kuwashawishi wanunue.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Mauzo ni kamari yenye uhakika wa ushindi. Nitajitahidi kuwafikia wateja wengi ili niweze kuuza zaidi. Asante kocha
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kwa hakika kazi ndiyo kila kitu, hakuna njia ya mkato kupata mafanikio au ushindi.
LikeLike
Kweli kabisa.
LikeLike
Hakuna njia ya mkato yeyote ambayo inaweza ikatupa pesa kwa uhakika hivyo jambo kubwa ni kuhakikisha tunafuata mchakato kamili
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Mauzo ni kamari ambayo hupotezi; sharti moja tu weka kazi!
Asante Kocha.
LikeLike
Ni kuendelea kucheza bila kuacha.
LikeLike
Mauzo ni kamari yenye uhakika wa ushindi kama utakaa kwenye mchakato wa mauzo.
LikeLike
Kukaa kwenye mchakato ndiyo lililo muhimu zaidi.
LikeLike
Nitacheza kamari ya kwa kuwafikia wateja wengi na kuwashawishi kununua
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Mauzo ni kamari yenye uhakika wa ushindi.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Mauzo ndiyo kamari yenye uhakika wa ushindi.
Na ili kupata ushindi kwa uhakika,napaswa kuwafikia wateja wengi zaidi.Asante Kocha.
LikeLike
Hakika, ni kucheza kwa wingi zaidi.
LikeLike
Naepuka kazi za mkato, na nakuwa na uhakika wa ushindi
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Mauzo ni kamari yenye uhakika wa ushindi!
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante kocha ni kweli mauzo ni kamari ya uhakika bila mauzo hakuna biashara na bila mauzo maisha yanakuwa magumu sana kwasababu maisha yetu yanategemea fedha sana
LikeLike
Hakika
LikeLike