3121; Nioge au nisioge?
Rafiki yangu mpendwa,
Kuna vitu ambavyo huwa unavifanya kwenye maisha yako bila ya kuwa na mjadala kama uvifanye au la.
Fikiria kuoga, ukifika wakati wa kufanya hivyo huwa hujiulizi iwapo uoge au usioge, huwa unaoga.
Kadhalika kupiga mswaki, haina mjadala, unapofika wakati wa kufanya hivyo, unafanya.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye kula, unaposhikwa na njaa, utafanya kila namna uweze kula.
Cha kushangaza sasa, wewe ambaye vitu kama kula, kuoga na kupiga mswaki unavifanya bila kuhoji, ndiye ambaye vitu vya msingi kabisa unavyopaswa kufanya bila kuhoji, unaishia kuhoji mpaka unashindwa kuvifanya.
Hebu fikiria kwenye kujenga na kukuza biashara yako, kuandaa mfumo wa kuendesha biashara au kujenga wateja waaminifu kwenye biashara yako.
Hayo ni majukumu muhimu mno kwenye ukuaji wa biashara yako, lakini cha kushangaza huwa ndiyo majukumu ambayo inakuchukua muda mrefu sana kuyafanya, kama hata utayafanya.
Kinachokukwamisha kwenye majukumu hayo siyo kwa sababu ni magumu sana kufanyika.
Bali ni kwa sababu hujaweza kuyageuza kuwa sehemu muhimu ya maisha yako ya kila siku.
Hujayageuza kuwa tabia ambayo unaifanya moja kwa moja.
Unakuwa huna haraka yoyote ya kuyakamilisha kwa wakati.
Na unakuwa hujayafanya yasiwe na mjadala bali kuyafanya.
Ili uweze kufanya yale unayopaswa kufanya ufanikiwe, unapaswa kuyajengea vitu hivi vinne;
Kwanza yafanye kuwa sehemu ya maisha yako ya kila siku, usiyaone kama ni kitu cha nje.
Mbili yageuze kuwa tabia unayoifanya moja kwa moja, bila hata ya kufikiria sana. Inapofika wakati wa kufanya unafanya bila ya mjadala.
Tatu weka hali ya haraka kwenye kuyafanya, usiwe mtu wa subira au kuahirisha kufanya, unapofika wakati wa kufanya, unafanya kwa haraka.
Nne ondoa mjadala iwapo ufanye au usifanye, inapofika kwenye kufanya, unachukua hatua mara moja bila ya mjadala wowote ule.
Kwa kuzingatia hayo manne, hakuna namna ambayo utakwama kufanya yale muhimu unayopaswa kufanya ili kupata kile unachotaka kwenye maisha yako.
Mafanikio kwako yanakuwa ni kama pumzi, ambayo hujishauri bali kuivuta.
Unachotaka zaidi kwenye maisha yako ni uhuru, hivyo unaupambania mpaka uupate kwa uhakika.
Unaporuhusu mjadala kwako binafsi iwapo ufanye kitu au usifanye, kwa sehemu kubwa hutakifanya.
Mafanikio yanajengwa pale unapofikia ngazi ya kufanya kitu bila ya kuwa na mjadala wa aina yoyote ile.
Inapohitajika kufanya, unafanya, kwa haraka na uhakika bila mjadala wala kufikiria.
Ukiweza kufikia ngazi hiyo ya ufanyaji, hakuna kinachoweza kukuzuia kufanikiwa.
Bado hatujafikia ngazi ambayo unaweza kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako bila kufanya.
Hivyo weka kipaumbele kikubwa kwenye kufanya.
Ni kupitia kufanya ndiyo unaweza kuzalisha matokeo yoyote yale unayoyataka kwenye maisha yako.
Ni vitu gani umeshafikia ngazi ya kufanya kila siku bila mjadala? Karibu ushirikishe kwenye maoni hapo chini.
Kwangu mimi uandishi ni namba moja.
Kama bado hujawa na kitu ambacho umeshaweza kufanya kwa aina hiyo, kipi ambacho ungependa kufanya kila siku bila ya mjadala? Shirikisha na uweke mpango wako wa kuhakikisha unaweza kukifanya kila siku bila ya mjadala.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kitu ambacho hufanya bila mjadala ni kazi.
Nafanya kazi Kwa bidii na maarifa na hilo Sina mjadala nalo.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Ni kweli ni kuoga tu kwa kuyawekea haya
1.kuyaweka kuwa sehemu ya maisha
2.kuyafanya kwa haraka bila kujadili
3.kugeuza kuwa tabia yako
4.ondoa sababu
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kitu nachofanya bila mjadala ni kuamka mapema, kusoma na kuanza kazi mapema.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Ondoa mjadala iwapo ufanye au usifanye, inapofika kwenye kufanya unachukua hatua mara 1 bila mjadala wowote ule
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kitu ambacho ninakifanya bila mjadala ni kufundisha wateja kwenye magroup ya WhatsApp
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante Kocha,
Mafanikio kwangu yatakuwa pumzi ambayo sijishauri kuivuta
Ufugaji kuku, kilimo cha mbogamboga na matunda ni shughuli ambazo daima nitaogelea humo.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kwa sasa kitu ambacho nakifanya bila mjadala ni kuamka kila siku saa kumi asubuhi na kuendelea na majukumu yangu ya siku.
LikeLike
Hongera sana.
LikeLike
Asante kocha kitu ambacho nina kifanya bila mjadala nikujenga mahusiano na wateja wangu nakufanya kazi so biashara bila sababu yoyote
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Bado sijaweza kupiga simu, kusaka na kufuatilia wateja bila mjadala
LikeLike
Jenga hayo uweze kufanya bila mjadala.
LikeLike
Kwangu Mimi kitu ninachofanya kila siku ni kujifunza kila siku
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Asante sana kocha,kitu kwangu ambacho nakifanya bila mjadala ni kuamka asbh na kushiriki vipindi vya BIT, kingine sasa ambacho nahitaji kujifanya bila mjadala na bila shuruti ni kuanza kutekeleza ratiba zangu bila kuingiliwa au kuathiriwa na chochote labda asili tu.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Asante kocha,Kitu ambacho ninakifanya kila siku bila mjadala ni kuamka mapema kila siku na kufanyia to do list ya kila siku na kuitekeleza.na kazi ndo kipaombele changu.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kwangu Mimi kusoma ni Namba moja. Japokuwa sijafanikiwa viwango vya juu . Mpango wangu ni kujiwekea Sheria kwamba kila siku kabla saa flani niwe nimeshasoma sura moja ya kitabu nitakachokuwa nimekipendekeza mwenyewe,
Asante kocha kwa mbinu /hamasa unazotupatia
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Asante sana, kwangu KUSOMA biblia kila siku nasoma sura moja na huwa sina mjadala Kwa jambo hilo
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kwangu mimi uandishi ndiyo namba moja.
Asante sana
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Kufungua ofisi mapema ni kitu ambacho nitakifanya daima.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante sana nitahakikisha nafanya bila kufikiria vitu ambavyo ni muhimu
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Kila siku najenga biashara yangu ya Restaurant Kwa kuboresha mfumo, kujenga timu,kujenga wateja waaminifu na kujifunza zaidi Nafanya kama sehemu ya maisha, kama pumziehakuna kujiuliza kama nifanye au la…
Asante Kocha
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante sana kocha kwa makala hii.
Majukumu yaliyo muhimu kwa mafanikio yangu,
1. Nitayafanya kuwa sehemu yangu ya maisha ya kila siku
2. Nitayageuza kuwa tabia yangu
3. Sitasita bali nitaweka hali ya haraka kuyafanya
4. Nitaondoa mjadala wa kwamba nifanye au nisifanye.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ibadan kwangu Haina mjadala. Nafanya asubuhi na jioni Kila siku.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kufanya Ibada kwangu hakuna mjadala. Nafanya asubuhi na jioni Kila siku
LikeLike