3122; Kukosa tatizo ni tatizo.
Rafiki yangu mpendwa,
Kuna watu huwa wanajipa matumaini hewa na ambayo yamekuwa kikwazo kikubwa kwenye maisha yao.
Moja ya matumaini hewa ambayo yamewapoteza wengi ni kusubiri mpaka matatizo waliyonayo yaishe ndiyo waweze kufanya yale wanayotaka kufanya.
Wanachokuja kugundua ni kwamba pale tatizo moja linapotatuliwa, matatizo mengine yanazaliwa.
Yaani hata tu suluhisho la tatizo lililopo tayari ni chanzo cha matatizo mengine.
Mtu yeyote anayekuambia hana tatizo huenda hajawa na uelewa wa kutosha kwenye kitu husika ili kuweza kuyatambua matatizo yaliyopo.
Au mtu huyo anakudanganya kuhusu matatizo aliyonayo.
Matatizo na changamoto unazokuwa nazo ni sehemu ya maisha.
Hivyo ndivyo vinavyofanya maisha yawe na maana kuyaishi.
Ni kupitia kutatua matatizo na changamoto ndiyo mtu anayafurahia maisha yake.
Kama maisha yako yanakwenda sawa bila tatizo au changamoto zozote, hilo ni tatizo kubwa sana.
Huenda kuna namna unavyowadanganya wengine na hata kujidanganya wewe mwenyewe pia.
Huwa ni rahisi sana kujidanganya wewe mwenyewe na huwa wengi wanafanya hivyo.
Inahitaji umakini wa hali ya juu sana kuweza kuyaona matatizo kabla hata hayajawa na madhara makubwa. Hilo linawapa fursa ya kupiga hatua kubwa na kwa haraka.
Lakini kwa wale waliokosa umakini kwenye chochote wanachofanya, huwa hawayaoni matatizo mapema kabla hayajawa makubwa.
Na hilo hupelekea kuingia gharama kubwa kutatua matatizo hayo yakiwa yameshaleta madhara makubwa.
Pale unapojiona huna tatizo lolote, pata wasiwasi, hakuna namna ukawa huna kabisa tatizo lolote lile.
Kila wakati jitafakari kwa kina na jua kwa undani kila unachofanya ili uweze kuyaona matatizo kabla hayajawa wazi kabisa.
Pia kutatua matatizo unayokuwa nayo haimaanishi ndiyo umeyamaliza kabisa, bali jua umezalisha matatizo mengine kutoka kwenye suluhisho ulilopata.
Usiogope wala kuhofia matatizo unayokutana nayo kwenye maisha.
Hayo ni sehemu ya kuyafanya maisha kuwa na maana.
Yajue, yapende, yapokee na yatatue matatizo mbalimbali kwenye maisha yako na utaweza kupiga hatua kubwa sana.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Sitaogopa wala kuhofia matatizo kwa sababu ndiyo yanayoleta maana kwenye maisha
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Usiogope wala kuhofia matatizo unayokutana nayo kwenye maisha. Hayo ni sehemu ya kuyafanya maisha kuwa na maana. Yajue, yapende, yapokee na yatatue matatizo mbalimbali kwenye maisha yako na utaweza kupiga hatua kubwa sana.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Matatizo ni sehemu ya kukupeleka ngazi nyingine na kuwa wa maana sana kuliko ulipokua lakini unazalisha tatizo lingine na litakupeleka mahali bora zaidi
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Sitaogopa wala kuhofia matatizo ninayokutana nato kwenye maisha maana ndo yanaleta maana ya maisha
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Natambua na kuelewa, matatizo na changamoto ninayokutana nayo ni sehemu ya maisha yangu.
Sitaogopa wala kuhofia matatizo nitakayokutana nayo kwenye maisha yangu _Muhimu najua nipo sehemu sahihi ambapo ni kisima cha maarifa.
Asante sana kocha.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kwa kila namna nifahakikisha nina tatua matatizo nakupiga hatua zaidi
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Usiogope na matatizo unayokutana nayo kwenye maisha.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kukosa tatizo ni tatizo kubwa kwani matatizo ndiyo chanzo cha mafanikio makubwa. Asante kocha
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Nikweli hakuna kipindi matatizo yakaisha
LikeLike
Hakika
LikeLike
Matatizo ni sehemu maisha yetu tunapoyakabili matatuzo ndio tunakuwa zaidi
Asante sana
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Nitayajua,kuyapenda na kutatua matatizo mbalimbali kwenye maisha yangu ili kupiga hatua kubwa.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Matatizo ndiyo yanaifanya dunia kuwa bora, kila matatizo yanapotokea, yanakuja na namna bora ya kuifanya dunia kuwa bora.
Asante sana
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Nitaangalia kila upande wa maisha Yangu Na changamoto Zote ctoziogopa tena najua ni njia ya kufanya Maisha yangu yawe bora
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Ni kweli kabisa,
Matatizo na Changamoto ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku.
Kutatua changamoto au matatizo ni raha na ndio yanafanya maisha kuwa na maana.
Pia kutatua matatizo unayokuwa nayo haina maana kuwa ndio umeyamaliza bali ndio umezalisha matatizo mengine toka kwenye suluhisho ulilopata.
LikeLike
Sahihi
LikeLike
Asante kocha,Sintaogopa na wala kuhofia matatizo ndo njia ya kuwa imara kwenye maisha na suruhisho la kufanikiwa.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kila siku zipo changamoto, Kuna kipindi mtu unakuwa na Changamoto ya kukosa wateja wa kuwahudimia. Ukipata wateja nao wanaleta changamoto ya jinsi ya kuwamudu kwenye huduma.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Pale unapoona huna tatizo lolote,pata wasiwasi.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kukosa tatizo ndio tatizo kubwa kuliko tunavyodhani.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Nayajua,nayapokea,nayatatua… matatizo ni sehemu ya maisha na Ndiyo yanafanya maisha yawe na maana.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Usiogope wala kuhofia matatizo unayokutana nayo kwenye maisha.
Hayo ni sehemu ya kuyafanya maisha kuwa na maana.
Yajue, yapende, yapokee na yatatue matatizo mbalimbali kwenye maisha yako na utaweza kupiga hatua kubwa sana.
LikeLike
Kabisa
LikeLike