3124; 1, 10, 100, 1,000 na kuendelea.
Rafiki yangu mpendwa,
Mafanikio yoyote unayoyataka kwenye maisha yako, ni muhimu ukawa na namba za kuyapima.
Hiyo ni kwa sababu kitu chochote kile ambacho hakipimwi, hakiwezi kuboreshwa wala kukuzwa.
Pamoja na umuhimu huo mkubwa wa namba na kupima, bado watu wengi sana hawana namba wanazojipima nazo, kitu kinachokuwa kikwazo kikubwa kwao kupata mafanikio wanayokuwa wanayataka.
Hapa kuna namba rahisi sana ambazo nataka uanze kujipima nazo ili kuweza kupata mafanikio makubwa unayoyataka, kupitia biashara unayofanya.
Anza kwa kufikiria mteja mmoja anayekufurahisha sana kwenye biashara yako. Mteja ambaye unatamani wengine wote wangekuwa kama yeye.
Huyo ni mteja anayeielewa thamani unayoitoa, analipia kwa ukamilifu na kwa wakati, anarudi kununua mara kwa mara na kwa wingi na anawaleta wateja wengine wengi kwenye biashara.
Kisha jiulize kama ungekuwa na wateja wa aina hiyo 10 ni manufaa kiasi gani ungeyapata kwenye biashara yako?
Vipi ukiwa nao 100, au1,000 na kuendelea?
Kokotoa manufaa ya kuwa na wateja hao wazuri 10, 100, 1,000 na kuendelea.
Kwa kila namba utakuwa unajionea jinsi ambavyo manufaa ni makubwa.
Ukiwa na wateja bora 10, unaondoa kabisa wasiwasi wa iwapo mmoja akiondoka itakuwaje. Unapokuwa na mmoja pekee, kila mara unahofia kuondoka kwake. Lakini wanapokuwa 10, hata kama hupati faida kubwa, unakuwa huna wasiwasi mkubwa.
Ukiwa na wateja bora 100, biashara yako inakuwa inaweza kujiendesha vizuri kabisa na kwa faida. Wateja bora 100 ni idadi nzuri ya kukuwezesha kuendesha biashara yako vile unavyotaka wewe, huku ukiyafurahia maisha yako.
Idadi ya 100 unaweza kuihudumia vizuri na kwa upekee mkubwa kitu ambacho unaweza kuwabakisha kwenye biashara yako kwa muda mrefu.
Ukiweza kutengeneza wateja bora 100 na ambao ni mashabiki wa kweli wa biashara yako, unakuwa umejitengenezea uhakika kwenye biashara yako.
Ukiwa na wateja bora 1,000 na kuendelea, unakuwa umejihakikishia kupata mafanikio makubwa sana unayotaka kuyapata. Kwa namba hiyo ya elfu moja, hakuna chochote ambacho kinaweza kushindikana.
Wateja wa uhakika elfu moja na kuendelea ni kama bima ya uhakika kwenye biashara na maisha yako. Kwani hao wana nguvu ya kuweza kuikuza biashara kupitia manunuzi ya mara kwa mara, makubwa na kwa kuwaambia wengine.
Ukishafikia namba ya elfu moja, kwenda zaidi ya hapo ni rahisi kuliko ilivyokuwa kwenye kufika hapo.
Tukirudi kwenye namba 1, hii nina uhakika kabisa kwamba unayo.
Kwa wateja wote ulionao sasa, kuna mmoja ambaye anakufurahisha sana kwenye biashara yako.
Anza kwa kujiwekea lengo la kutengeneza wateja 10 wa aina hiyo.
Angalia ni kwa jinsi gani ulimpata huyo na umekuwa unamhudumiaje mara zote.
Kisha rudia zoezi hilo kwa wengine mpaka ujenge 10 ambao ni wa uhakika kabisa.
Baada ya kujenga wateja hao wa uhakika 10, lengo linalofuata ni kufikia 100. Hapo pia unarudia mchakato uliokufikisha kwenye 10 na kuufanya kwa ukubwa ili kufika kwenye 100.
Kadhalika kwenye kufikia wateja wa uhakika 1,000 na kuendelea, unarudia zoezi hilo hilo.
Kitu kimoja kitakachokushangaza ni kadiri unavyokwenda, ndivyo zoezi linavyokuwa rahisi.
Ukianza na mteja 1 kwenda 10, kazi inakuwa kubwa na ngumu. Na pia inaweza kuchukua muda mrefu kukamilisha.
Kutoka 10 kwenda 100, ugumu wa kazi unapungua huku pia muda wa kufanikisha ukiwa mdogo kuliko hatua ya nyuma.
Kutoka 100 kwenda 1,000 kazi pia inakuwa rahisi huku muda nao ukiwa mdogo kuliko hatua iliyopita.
Na kuanzia 1,000 na kuendelea, kazi unaweza hata usiifanye wewe, bali wateja bora wakawa wanakuja wenyewe kwa sababu tayari wengine bora wapo.
Kabla hujaanza utekelezaji wa zoezi hilo unaweza kuliona ni gumu kadiri unavyokwenda mbele.
Lakini uhalisia ni kinyume chake, linakuwa rahisi zaidi kadiri unavyokwenda.
Kilicho muhimu ni uepuke tamaa ya makubwa kabla hujakamilisha madogo.
Unaweza kuona 10 ni ndogo hivyo kukimbilia 100 kabisa.
Ni fikra nzuri, lakini kwenye utekelezaji ni vigumu.
Ni rahisi sana kuanza kutekeleza 10 kabla ya 100.
Ukishakamilisha wateja wa uhakika 10, ni rahisi sana kwenda kwenye lengo la 100.
Kadhalika kwenye namba zinazoendelea, unapokamilisha kwa namba za chini, inakuwa rahisi zaidi kwenda kukamilisha kwenye namba za juu.
Mafanikio makubwa unayoyataka yapo kwenye kujenga wateja bora na wa uhakika wa biashara yako.
Weka juhudi kubwa kwenye hilo na utaweza kupata chochote kile unachotaka.
Uzuri ni kwamba kama umeweza 1, utaweza pia 10, kisha 100, 1,000 na kuendelea.
Ukiangalia hizo namba zinakwenda kwa mara 10 na siyo kujumlisha, kwa sababu ukuaji unaohitajika ni mkubwa ili mafanikio makubwa yaweze kufikiwa kwa uhakika.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante sana Kocha kwa formula hii 1, 10, 100, 1000 ukuaji wowote ni mchezo wa namba tu itatupeleka tunapotakiwa.
LikeLike
Tukae kwenye mchezo huo wa namba, namba zituongoze.
LikeLike
Wateja wa uhakika elfu moja na kuendelea ni kama bima ya uhakika kwenye biashara na maisha yako.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Huo ni uhakika.
LikeLike
Anza ba mteja mmoja kufika 100 zoezi linakua rahisi sana
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Unatumia njia ile ile iliyokuwezesha kupata wateja 10 kwenye kupata wateja 100, 1000 na kuendelea.
LikeLike
Haina haja ya kugundua upya tairi (reinvent the wheel)
LikeLike
Kama nimeweza moja basi hata 10,100,1,000 nitaweza.
Wateja Bora 100 ni bima ya biashara na maisha yangu Kwa ujumla, napambana kupata bima hii.
LikeLike
Vizuri, ipambanie hasa.
LikeLike
Asante Kocha,
Nakaa kwenye mchakato wa kuzidisha kwa IO daima.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
asante sana kocha,
Tunaanzia na lengo la chini na tunalizidisha mara 10 kila tunapo lifikia.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Mafanikio makubwa ya biashara yapo kwenye kujenga wateja bora. Nitaweka juhudi kutengeneza wateja bora.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Nitahakikisha Nawashilikisha wakamilishaji wangu, kila mkoja ainishe wateja wake wazuri kabisa na kumuwekea malengo ya kuongeza idadi mara 10 zaidi na kuendelea.
Pia niitaangalia wakamilishaji walio bora kwenye kampuni yangu na kuweka mkakati wa kutafuta wakamilishaji bora kama hao ambao watakuwa wanaleta mauzo makubwa zaidi kama hao au zaidi yako. Asante sana Kocha kwa haya mafundisho. Mwalemi 🙏🏽
LikeLike
Mkakati mzuri sana huu, utekeleze kama ulivyopanga.
LikeLike
Nitahakikisha Nawashilikisha wakamilishaji wangu, kila mmoja ainishe wateja wake wazuri kabisa na kumuwekea malengo ya kuongeza idadi mara 10 zaidi na kuendelea.
Pia niitaangalia wakamilishaji walio bora kwenye kampuni yangu na kuweka mkakati wa kutafuta wakamilishaji bora kama hao ambao watakuwa wanaleta mauzo makubwa zaidi kama hao au zaidi yako. Asante sana Kocha kwa haya mafundisho. Mwalemi 🙏🏽
LikeLike
Mafanikio yeyote kwenye maisha ni muhimu unaware na namba za kujipima
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante sana kocha, hakika nahitaji kujenga wateja bora kwa kuanzia chini,namba ni muhimu kwenye biashara.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Tutoe huduma Bora sana Kwa wateja Kwa wateja 10 na Kwa hakika tutapata wateja 100 ,1000 na biashara kuweza kukua zaidi
Asante
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kwa kuwa nimeweza 1, hatimaye nitaweza 100 na zaidi.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Uepuke tamaa ya makubwa kabla hujakamilisha madogo.
LikeLike
Anza na mdogo kwenda kwenye makubwa.
LikeLike
Asante kocha,Mafanikio ninayoyataka kwenye biashara ni kujenga misingi bora ya wateja,nikianza na 1 na pia 10 nitaweza kufikia 100, na 1,000.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kutokuwa na Namba za kujipima ktk Yale tufanyayo ni
Kikwazo kikubwa ktk kupata mafanikio, hivyo kuwa na Namba za kujipima nazo ni hitaji la lazima ikiwa tunataka kufanikiwa.
Asante Sana kocha
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nitakua kwa mtindo wa kuzidisha mara kumi.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
NIKWELI KAMA NIMEWEZA 1 NA 1000 INAWEZEKANA
LikeLike
Ndiyo
LikeLike