3144; Kuepuka kupoteza.
Rafiki yangu mpendwa,
Zipo njia mbalimbali za kujifunza kitu.
Njia ya kwanza ni jinsi ya kupata kitu hicho na njia ya pili ni jinsi ya kukikosa.
Tumezoea sana kujifunza njia ya kwanza ya kupata na kusahau njia ya pili ya kukosa, ambayo pia ina nguvu kubwa.
Bilionea mwekezaji Charlie Munger huwa ana kauli yake maarufu inayosema; ninachotaka kujua ni wapi nikienda nitakufa ili nisiende hapo.
Nukuu hiyo inaonyesha nguvu ya kujifunza kwa kuepuka kupoteza badala ya kutaka kupata.
Kujifunza kupitia uzoefu wa wengine huwa kuna nguvu kubwa kuliko tu kutegemea uzoefu wako binafsi.
Sasa kwa kuwa kwenye jamii tunazungukwa na watu wengi walioshindwa kuliko waliofanikiwa, tunapaswa kuangalia yale walioshindwa wanapenda kuyafanya na kwenda kinyume na hayo.
Mwandishi, mjasiriamali na mwekezaji Alex Hormozi ametupa orodha ya mambo ambayo kwa uhakika yanawaweka watu wengi kwenye umasikini.
Kwa kuyajua na kuyaepuka mambo hayo, inakuwa na nguvu ya kuwatoa watu kwenye umasikini na kuwafikisha kwenye utajiri.
Kwa majibu wa Hormozi, ambao pia ndiyo uhalisia, hivi ndivyo watu wengi wanavyobaki kwenye umasikini;
1. Kila siku kusema wataanza kesho, kitu ambacho hawaanzi kabisa.
2. Kusoma vitabu bila ya kufanya chochote.
3. Kuchukua ushauri wa watu masikini wa jinsi ya kuwa tajiri.
4. Kuchagua mwenza ambaye anakufanya ujione una hatia pale unapofanya kazi zaidi.
5. Kushindwa mara moja na kukata tamaa milele.
6. Kulaumu hali unazopitia.
7. Kusubiri mpaka kila kitu kiwe na ukamilifu.
8. Kuwalaumu wengine.
9. Kutegemea serikali ikusaidie.
10. Kuthamini maoni ya wengine kuliko maoni yako binafsi.
11. Kulalamika.
12. Kukwepa usumbufu.
13. Kufaka matokeo ya haraka baada ya kazi.
14. Kuvumilia viwango vya chini.
15. Kuahidi halafu kutokutimiza ahadi hizo.
16. Kutaka kuonekana tajiri badala ya kuwa tajiri.
17. Kufanya kazi kwa juhudi kwenye mambo yasiyo muhimu.
18. Kusema utafanya kitu, halafu usikifanye.
19. Kusubiri mpaka uwe tayari.
20. Kufanya kazi kwa asilimia 99, kutegemea matokeo kwa asilimia 1.
21. Kufanya unachoweza badala ya kufanya kinachohitajika.
22. Kusema upo kwenye umasikini kwa sababu hutaki kuvunja maadili yako.
23. Kuongea sana na kutokufanya chochote.
24. Kuanza kitu kipya leo, kuanza kitu kipya kesho na kurudia huo mzunguko.
25. Kufikiria kununua na kuuza hisa wakati hujawa na kipato cha uhakika.
26. Kufanya makosa na kurudia makosa hayo.
27. Kupata kitu kinachofanya kazi, kisha kuacha kukifanya.
28. Kudhani mara zote upo sahihi.
29. Kuchukia pale mtu anapokuwa hakubaliani na wewe.
30. Kuongeza kipato chako kisha kuongeza matumizi mara dufu.
31. Kubadili malengo yako pale yanapokuwa magumu.
32. Kufanya yale ambayo kila mtu anayafanya na kutegemea kupata matokeo ya tofauti.
33. Kutumia gharama kubwa kwenye burudani badala ya elimu.
34. Kutokufanya maandalizi.
35. Kuamini yale ambayo watu wanasema kuliko yale wanayofanya.
36. Kuona wengine wanakosea na wewe kurudia makosa hayo.
37. Kudhani kwa sababu huwezi kumudu kitu basi mteja pia hawezi kukimudu.
38. Kutaka kila mtu akupende.
39. Kudhani kupata pesa na kutunza pesa ni kitu kimoja.
40. Kudhani kwamba usipochukua hatua za hatari basi umekwepa hatari kubwa kuliko zote – kutokufanya chochote.
Rafiki, ni orodha ndefu ambayo imejumuisha tabia zote ambazo zinawaweka watu wengi kwenye umasikini.
Je ni tabia zipi kati ya hizo unazo kwa ukubwa?
Unafanyaje ili kuondokana na tabia hizo ili uweze kuondoka kwenye umasikini?
Shirikisha majibu ya haya maswali kwenye maoni hapo chini.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani, mwandishi amesema ukweli mtupu na tabia zinafanana kote duniani.
Tujenge utajiri kwa kuiga kuishi umasikini.
LikeLike
Ni kweli kabisa hapa kuna orodha kuna tabia ambozo tunazifanya kila wakati na ni sababu ya sisi kuwa tulivyo hivyo ni muhimu Sana kuzirekebisha na kwenda kinyume nazo. Ili kufanikiwa
LikeLike
Nzuri
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante kocha, Kwa kushirikisha hili, nyingi ya tabia hizi ndiyo wengi wetu zinatuzunguka. Nimejifunza na nitaendelea kuchukua hatua za kubadilika Ili kuwa Bora zaidi.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kutaka kupendwa na watu
Ukitaka watu wakupende maana yake ni kwamba ufanye yale wanataka wao na siyo yako ajili ya maendeleo yako
Kusubiri pia hadi kila kiti kikamilike
Hilo ni jambo baya sana anzia hapo ulipo na usonge mbele huku ukiendelea kurekebisha mambo yakae sawa yote pia
Kujaribu kila kitu na kufanya kila siku kitu kipya hilo limenigarimu sana na baada ya kugundua sasa nipo kwenye mstari uliknyookeana na kitu kimoja tu kwa ubora na ukubwa wakw
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Hapa kuna baadhi ya tabia zinanihusu moja kwa moja. Nitahakikisha nazivunja tabia hizi ili zisiendelee kuwa kikwazo cha kushindwa kupata matokeo ninayotaka.
Asante.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Tabia hizi zote nilikuwa nazo kabla sijawa mwanachama wa kisima cha Maarifa lakini kwa sasa nimebadilika kwa sehemu kubwa kwa kwenda kinyume na kila tabia ili nisiwe masikini. Asante sana kocha
LikeLike
Vizuri sana, usirudi nyuma.
LikeLike
ameongea ukweli ambapo makosa mengi ndiyo tunayarudia kila siku.Nitajitoa kutokufanya aliyoshauri ili nisibaki masikini
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kuthamini maoni ya wengine kuliko maoni yako, hili ni baya sana.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Tabia zinazonihusu ni kusubiri kila kitu kiwe na ukamilifu, kurudia makosa, kusema nitaanza kesho, na kusubiri mpaka niwe tayari. Nakwenda kuachana nazo na kuendelea kujisikuma ili kupata matokeo
LikeLike
Vizuri, fanya hivyo.
LikeLike
Asante kocha kuna baadhi ya tabia zinanihusu moja kwa moja kwa hiyo nitaujenga Utajiri kwa kuiga kuishi masikini
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kwa hakika bado baadhi ya tabia hizi ninazo. Nitaendela kuziondoa haraka inavyowezekana ili niweze kupata mafanikio.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante sana Kocha,
Hapa kutaka kila mtu anipende, Kusema nitafanya kitu, halafu nisikifanye, Kusubiri mpaka niwe tayari
ni tabia ambanzo napaswa kuziacha mara moja.
LikeLike
Vizuri, fanya hivyo.
LikeLike
Kukwepa usumbufu.Sijajua mwandishi anamaanisha nini,lakini binafsi huwa sipendi usumbufu ambao hauna tija,na kama kuna nafasi ya kuukwepa nafanya hivyo.
Kuona wengine wanakosea na wewe kurudia makosa hayo.Kuna mambo mengi kwenye jamii si sahihi sana,lakini najikuta na mimi mengine nayafanya,mfano michango ya harusi,nalalamika lakini na mimi nachangia,mikutano makazini mingi ya kupoteza muda,lakini na mimi nahudhuria.
LikeLike
Rekebisha hayo.
LikeLike
Kusema utafanya kitu, halafu usikifanye. Na jambo ja pili huwa nachukia sana kama mtu hakubaliani na mimi. Nakwenda kuacha mara moja tabia hii inanikwamisha sana
LikeLike
Vizuri, tekeleza.
LikeLike
Hii orodha imetoa maelekezo ninavyocheza na mstakabali wa maisha yng sasa ni kufanya kinyume,vinavyooneka havileti utajiri na maskini kuigiza kujiona tajiri wkt tajiri anaigiza umaskini.
Asante kocha.
LikeLike
Vizuri, chukua hatua.
LikeLike
Asante sana kocha, nitaendelea kujifunza zaidi,ili kuzichambua na kuzifanyia kazi kwa usahihi.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Kubadili malengo yako pale yanapokuwa magumu.
Kudhani kwamba usipochukua hatua za hatari basi umekwepa hatari kubwa kuliko zote – kutokufanya chochote.
Haya mawili yananikumbusha kuendelea kuikabiri HATARI na Kuendelea Kuukabiri UGUMU pasipo kusubiri kila kitu kiwe sawa.
LikeLike
Vizuri, fanya hivyo.
LikeLike
*Kusoma vitabu bila ya kufanya chochote.
*Kuvumilia viwango vya chini.
*Kusema nitafanya kitu,halafu nisikifanye.
LikeLike
Chukua hatua.
LikeLike
-kudhani wateja hawawezi kumdu kwasababu mimi siwezi kumudu
-kuchukia pale mtu anapokuwa hakubaliani na mimi
-kubadili malengo pale yanapokuwa magumu
-kusubiri mpaka kila kitu kiwe na ukamilifu
Napambana ili kuacha hiz tabia za kimaskini ili siziwe kikwazo kwangu kufikia ndoto kubwa nilizo nazo.
LikeLike
Vizuri, achana nazo.
LikeLike
Kwa upande wangu nilikuwa naishi Tabia 8,11 na 28
Lakini baada ya kupata maarifa haya nimeondokana na Tabia hizi
Asante
LikeLike
Vizuri, usirudi tena huko.
LikeLike
Asante kocha,ziko tabia nyingi sana ambazo zinanihusu moja kwa moja ila kutokana na mchakato wa bm nimezipunguza sana na najitahidi kuziacha kabisa.
LikeLike
Vizuri, endelea na hilo.
LikeLike
Kubadili malengo yangu pale mambo yanapokuwa magumu ni Moja ya sababu kwangu nafanyia kazi Ili mambo yasiweze kuwa magumu zaidi
LikeLike
Achana na hilo mara moja.
LikeLike
Kuchukia pale mtu anapokuwa hakubaliani na wewe.
Kudhani kupata pesa na kutunza pesa ni kitu kimoja
Nitaishi kistoa kwa kutochukia pale mtu anapokuwa hakubaliani na mimi,
Nitaweka mikakati sahihi ya jinsi ya kutunza pesa zangu
LikeLike
Vizuri, fanya hivyo.
LikeLike
Tabia ya Kusubiri mpaka kitu kiwe kikamilifu, kuthamini Maoni ya wengine kuliko Maoni yangu binafsi. Na Kufanya ninachoweza badala ya kufanya kinachohitajika ndio tabia zinazonirudisha nyuma.
Kwa sasa nimezijua na nitaachana nazo.
LikeLike
Vizuri, achana nazo.
LikeLike
Asante sana kocha
Hizi tabia za kimasikini wengi wetu tunazo mfano Mimi nina tabia ya kufanya ninachoweza badala ya kufanya kinachohitajika
LikeLike
Vizuri, chukua hatua.
LikeLike
Makosa mengi ndio tunayorejea kila siku
LikeLike
Tuachane nayo.
LikeLike
Makosa ninayorudia Kila mara ninaachana nayo
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kusubiri kilakitu kiwe tayari huku nako sio jambo jema nitaanzia pale nilipo
LikeLike
Vizuri
LikeLike