3154; Tofauti itakapoanzia.
Rafiki yangu mpendwa,
Siku ya jana, mjasiriamali na mwandishi Alex Hormozi alikuwa na tukio kubwa kabisa la kuzindua kitabu chake cha pili kinachoitwa $100M Leads.
Ni kitabu cha kutengeneza wateja tarajiwa kwenye biashara, ambapo ndani yake ameeleza njia nane za uhakika za kutengeneza wateja tarajiwa wengi kwenye biashara ya aina yoyote ile.
Ili kuonyesha njia hizo alizoainisha kwenye kitabu zinafanya kazi vizuri kabisa, aliamua kuzitumia zote kwenye tukio la kuzindua kitabu hicho.
Hivyo mapema sana alitangaza tukio hilo la uzinduzi wa kitabu na kutaka watu wajiandikishe kwenye mtandao.
Mimi ni mmoja wa waliofanya hivyo.
Kwa wiki zisizopungua sita, alitumia njia zote anazofundisha kwenye kitabu na akapata wahudhuriaji zaidi ya laki 5 waliojiandikisha kwenye tukio hilo.
Kwa kweli aliweka mategemeo ya kila mtu juu sana, akiahidi kuna kitu kikubwa ambacho atakitoa kwa wale tu watakaoshiriki uzinduzi huo mubashara kwa njia ya mtandao.
Siku ikafika ambayo ilikuwa ni jana na akafanya uwasilishaji bora kabisa kuwahi kutokea, kwa dakika 90.
Alieleza dhana nzima ya kitabu na kugusia njia hizo nane kwa mifano ya jinsi zinavyofanya kazi vizuri sana.
Mwisho akashirikisha mifumo 8 aliyoandaa ya kumsaidia mtu kwa uhakika kutengeneza wateja tarajiwa wengi kwenye biashara.
Alithaminisha mifumo yote 8 atakayompa mtu na ikawa zaidi ya dola elfu 12, hiyo ni karibu milioni 30 za Kitanzania.
Na ni kweli hiyo mifumo ina thamani kubwa mno, hatanii.
Kilichofuata baada ya hapo ndiyo kilitushangaza wote.
Kwa jinsi ninavyojua masoko na uwasilishaji, nilishajua wapi anaelekea.
Nilikuwa na uhakika atatoa mifumo hiyo kwa punguzo la bei kwa kuonyesha thamani kubwa ambayo mtu unaenda kuipata kwa kuwa nayo.
Na nilijiambia kwa uhakika bei atakayotaja haitapungua dola 900 na haitazidi dola elfu 5.
Akaendelea na uwasilishaji,
Akasema thamani hiyo ya zaidi ya dola elfu 12, ataitoa kwa dola elfu 4.
Akasema hapana, ataitoa kwa dola elfu 2,
Mpaka hapo nikawa najua wapi anaenda.
Lakini akaniacha na butwaa pale aliposema gharama halisi atakayotoza ni dola 0!
Kwa kweli sikuyaamini macho yangu.
Kila aliyeshiriki tukio hilo alishangazwa na kufurahishwa kwa wakati mmoja.
Nimejifunza masoko na mauzo kwa muda mrefu na niseme wazi, sijawahi kuona kitu cha aina hii.
Ni kitu cha kipekee mno, maana wengi huwa wanakisema, ila yeye amekitekeleza kwa uhakika.
Hakukuwa na mtego wowote, ni thamani ya dola elfu 12 ambayo unaipata bure kabisa, kwa kushiriki tu.
Kuna ofa nyingine alizotoa na ambazo alizopanga vizuri kwa kutumia mbinu ya uhaba, ambayo ilifanya kazi vizuri sana.
Lakini thamani kuu aliyoahidi kutoa bure ameitoa, mara baada ya tukio alituma kweli kwenye barua pepe yangu.
Kwa kuwamegea tu, tunayo zana moja matata sana ambayo tutaenda kuifanyia kazi kwa uhakika ndani ya Bilionea Mafunzoni na tutakuwa hatari mno.
Rafiki, hayo yote ni utangulizi tu, kilichofanya nikuandikie huu ukurasa wa leo ni kile nilichoona kwa watu baada ya tukio hilo.
Nilisema hebu nione watu wengine wanasemaje kuhusu uzinduzi huo ambao kwangu umekuwa wa kipekee kabisa.
Wengi walisifia sana, wakisema Alex amepandisha sana viwango vya uzinduzi wa kitabu.
Na kama kawaida, nikakutana na wengine ambao wanasema kama kila mtu atafanyia kazi mbinu zote ambazo Alex ametoa bure, kutakuwa na ushindani mkali sana sokoni na hivyo hazitafanya kazi.
Na hapo ndipo niliposhangazwa na kupata tumaini kwa wakati mmoja.
Nilishangazwa na jinsi baadhi ya watu wasivyokuwa na shukrani, au niseme kuwa na wivu kwa jinsi tukio hilo limekwenda kwa mafanikio makubwa.
Na nilipata matumaini kwamba kuna fursa kubwa sana ya kunufaika na mbinu hizo, kwa sababu, asilimia 99 ya watu waliozipata, hawatazifanyia kazi kabisa.
Kwanza kabisa wengi hawatafanyia kazi kwa sababu tu ya uvivu. Nimechungulia mfumo aliotuma wa hizo mbinu, nimeona inahitaji angalau masaa 8 ya kuangalia video za maelekezo. Na hapo nikajua kwa uhakika, wengi hawana utulivu wala umakini wa kutenga hayo masaa 8 ya kujifunza.
Kila mtu anataka vitu vya haraka haraka.
Pili, wengi watafikiri kwamba kwa kuwa kila mtu anafanyia kazi hayo, basi hayatafanya kazi.
Hivyo kwa kiburi chao, watahangaika kufanya kwa njia ya tofauti.
Na hawatapata matokeo mazuri kama yalivyoahidiwa.
Alex ametoa bure kabisa mchakato mzima uliomwezesha kujenga biashara zake na kufikia thamani ya zaidi ya dola milioni 100.
Na wachache sana ndiyo watakaonufaika na zana hizo, huku wengi mno hawatanufaika kabisa.
Tofauti ya makundi hayo mawili inaanzia kwenye KUFANYA.
Wote tumepata maarifa sawa kabisa, lakini tutatofautishwa na ufanyaji.
Wachache sana tutakaofanya tutanufaika.
Na wengi sana ambao hawatafanya hawatanufaika.
Ni rahisi kama hivyo.
Sote tunajua falsafa yetu kuu ya KISIMA CHA MAARIFA, ambayo ni kanuni; KUJIFUNZA + VITENDO = MAFANIKIO.
Hiyo ndiyo tunayoisimamia mara zote.
Na ndiyo inayotutofautisha na wengine wengi.
Tuendelee kuidumisha hiyo.
Ndiyo itakayotufikisha kwenye mafanikio makubwa tunayoyataka.
Karibuni sana kwenye ufanyaji.
Kinachotuweka pamoja hapa ni kujifunza na kufanya.
Kama hujifunzi hupati nafasi.
Na kama unajifunza na hufanyi pia hupati nafasi.
Ni kujifunza na kufanya, ndiyo kunatutofautisha na watu wengine wote.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ni kujifunza na kufanya, ndiyo kunatutofautisha na watu wengine wote.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Tunapaswa kujifunza kutumia maarifa hayo na kuyafanyia kazi bila kuweka uvivu na uzembembe oli itutofautishe na wengine
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kujifunza na kufanya tofaut na hapo hupat matokeo
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ninaona sasa kwamba kujifunza na kufanya ni moja ya tofauti kubwa kati ya maskini na matajiri. Matajiri ni wanyenyekevu, kujifunza na kufanya. Maskini wao wana kiburi, wanajua kila kitu na kuendekeza uvivu.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kujifunza na kufanya matokeo yake ni Utajiri
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ni hak sasa kutumia maarifa hayo kwa kazi bila kuweka uvivu na uzembembe ili kujitofautisha na wengine. Kuchukua hatua kubwa na kuweka juhudi thabiti.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ni kupitia kujifunza na kufanya.Hakuna shortcut
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Kujifunza na kufanya ndio msingi mkuu wa kisima cha maaria.Nitajifunza na kufanya daima.
LikeLike
Vizuri sana
LikeLike
Kujifunza na kufanya ndiyo kuna leta mafanikio makubwa. Maarifa + Vitendo= MAFANIKIO MAKUBWA.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante kocha,Nitajifunza na kufanya ili nifikie kusudi langu la mafanikio.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kujifunza + vitendo =mafanikio
Tufanye ndio tutapata mafanikio
Asante
LikeLike
Hakika.
LikeLike
wengi watafikiri kwamba kwa kuwa kila mtu anafanyia kazi hayo, basi hayatafanya kazi.
Hapa tunajionea Kiburi cha kimasikini kinavyotesa wengi,kufanya mambo kwa hisia,matokeo yake hawafanikiwi. Asante sana Kocha.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Kujifunza na kupata maarifa mengi hakubadilishi Hali ya mtu ya kufanikiwa au kutofanikiwa, bali kinachobadilisha ni kati ya anayeweka mafunzo kwenye matendo na yule aliyesheheni mafunzo bila matendo.
Tukijifinza na kutenda tutafika mbali szna. Asante sxna KOCHA, Tunasubiri utushirikishe hizo mbinu tupambane nazo kwa kuzitendea kazi
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Aisee, ni leo tu nilikuwa namsikiliza Eben Pagan kwenye audio book ya “How to build a Profitable business Starting from Scratch” akazungumzia hili.
Anasema hakuna hata haja ya kuhofia ushindani kwa sababu watu hawatafanya. Hili limenikumbusha kwamba upekee wangu na mafanikio yapo kwenye utekelezaji zaidi.
Nilimsikia pia Andrew Tate anasema mambo ni rahisi mno kwake kwa sababu haoni watu wa kumpa changamoto kwenye ushindani, anasema watu ni wazembe na wana excuse sana, hapo alikuwa anazungumzia jinsi hakuweza kwenda hata kwenye mazishi ya baba yake mzazi.
Nashukuru sana kwa kuendelea kukumbusha hili na kulikazia. Binafsi nitaliongezea uzito mnoo kwa sababu najua hapo ndipo penyewe.
LikeLike
Asante kwa mifano hii.
Unajionea wazi jinsi haya mambo yanavyogongana.
Ni raha sana kuwa na haya maarifa, ukijua wazembe wengi hawatafanyia kazi.
Hivyo ukifanya hata kwa kidogo tu, matokeo yatakuwa makubwa.
Msisitizo ni TUFANYE.
LikeLike
Ni wachache sana watakaonufaika na huduma hiyo huku wengi mno hawatonifaika. Hii ni kutokana na kiburi cha watu
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ni kujifunza na kufanya ndiko kunakotutofautisha na wengine.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ni kujifunza na kufanya ndipo utapata matokeo,jamaa alikuwa anaongea kwa akiwa na furaha, nguvu energy kubwa,shauku basi tu
LikeLike
Na hayo ndiyo makubwa ya kujifunza kwake na kufanyia kazi.
LikeLike
Nitatenga muda maalum kila siku kwa ajili ya kujifunza.
Na pia nitajisukuma kila siku kufanyia kazi Yale ninayojifunza , hayo yote nitayafanya kuwa sehemu ya Maisha yangu na hatinae nitafanikiwa . Asante kocha
LikeLike
Vizuri, kila la kheri.
LikeLike
Asante aama kocha, ni kujifunza na kufanya tu.
LikeLike
Hakika
LikeLike