3186; Mrejesho wa watu.
Rafiki yangu mpendwa,
Sisi binadamu kama viumbe wa kijamii, huwa tunapenda sana kuwa ndani ya kundi la watu.
Ili kujihakikishia nafasi yetu kwenye kundi lolote tulilopo, huwa tunajali sana kuhusu mrejesho wa watu wengine kuhusu sisi.
Huwa tunataka sana kukubalika na kila mtu, tukiamini ndiyo njia salama ya kuwa ndani ya kundi lolote lipo.
Lakini kile tunachotaka sana kutoka kwenye makundi tuliyopo, siyo tunachohitaji kwa ajili ya mafanikio makubwa tunayoyataka.
Kama kila mtu anaamini kwenye ndoto kubwa ulizonazo kwenye maisha yako, basi ndoto hizo siyo kubwa vya kutosha.
Ni ndoto za kawaida kabisa ambazo zipo kwenye fikra za kawaida za kila mtu.
Ndoto kubwa sahihi kwako ni zile ambazo wengine wakisikia unazo wanakucheka na kukuambia unajidanganya, kwani haiwezekani kabisa.
Ndoto kubwa sahihi kwako ni zile ambazo wengi hawawezi kabisa kuzielewa. Hizo ndiyo ukizifanyia kazi zinazalisha matokeo makubwa na ya tofauti.
Kama kila mtu anakupenda na kukukubali, kuna mahali unakosea.
Na kwa sehemu kubwa unakuwa huna viwango ulivyojiwekea ambavyo unavisimamia.
Hivyo watu wanakuona wewe ni mtu poa, lakini mwisho wa siku hakuna hatua kubwa unazopiga kwenye maisha yako.
Kukubaliana au kutaka kukubalika na kila mtu ni njia ya uhakika ya kushindwa kwenye maisha.
Ili ufanikiwe ni lazima uwe na viwango vya juu ambavyo unavisimamia.
Katika kusimamia viwango hivyo kuna watu utakaowaudhi, kwa kuwakatalia vitu walivyotaka.
Na hapo watu hao watakuchukia sana.
Lakini pia watakuwepo ambao watakupenda kwa viwango hivyo ulivyojiwekea.
Kama kwenye kufanya kwako masoko na mauzo hakuna watu wanaokulalamikia kwamba unawafuatilia sana au unawapigia sana kelele, basi jua hujapiga kelele za kutosha.
Unatakiwa uendelee kuwafikia wengi zaidi na kwa ukubwa na wingi zaidi. Unapaswa kuwafikia watu mara kwa mara kiasi cha baadhi yao kuona hilo ni kero kwao.
Ni kupitia malalamiko hayo ya wengine ndiyo utaboresha zaidi hatua hizo unazochukua.
Kama hakuna watu wanaokuona una roho mbaya na hujali, unahangaika sana na mambo ya wengine kuliko mambo yako binafsi.
Utawafurahisha wengi kwa kuhangaika na mambo yao, lakini hilo litakuwa kikwazo kwako kukamilisha yako kwa sababu huyapi muda wa kutosha.
Unapaswa kuweka kipaumbele cha kwanza na pekee kwenye mambo yako na kupuuza mengi ya wengine.
Umakini wako una ukomo, upeleke kwenye mambo yako na siyo mambo ya wengine.
Kama hakuna watu wanaoamini unatumia nguvu fulani zisizo sahihi kwenye mambo yako, basi hakuna makubwa unayofanya.
Kwenye biashara uliyopo, utajua kama kweli unaufanyia kazi mchakato sahihi kama washindani wako watakuwa wanakusema vibaya kwamba unatumia nguvu za ushirikina kuteka wateja.
Kwenye maisha ya kawaida, utajua kama kweli unauishi mchakato kama kuna watu wanasema wewe ni ‘freemason’. Waseme umepewa masharti makali ambayo huwa unayafuata bila kuvunja.
Hii ni baadhi ya mirejesho kutoka kwa wengine ambayo ndani yake inakuwa na somo la tofauti na tunavyodhani.
Tuendelee kukusanya hii mirejesho kutoka kwa wengine na kufanya maboresho sahihi ili kuhakikisha tunapata matokeo makubwa tunayoyataka.
Kanuni ya uhakika ya kuweza kufanya makubwa kwenye maisha yako ni kwenda kinyume na kundi kubwa la watu.
Hiyo ni kwa sababu mara nyingi kundi kubwa la watu huwa lipo kwenye njia ya kupotea.
Ukiweza kusimama imara dhidi ya kundi hilo kubwa, hakuna namna utashindwa kupata matokeo makubwa unayoyataka.
Kuwa na ndoto kubwa, ambazo ndiyo zinakuwa kipaumbele pekee kwako na kuwa na mchakato wa uhakika unaoufuata kwenye kuzipambania.
Simama kwenye kile kilicho sahihi bila kujali kundi kubwa la watu linakuchukuliaje.
Hiyo ndiyo namna pekee ya kupata mafanikio makubwa unayoyataka kwenye maisha yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kanuni ya uhakika ya kufanya makubwa kwenye maisha ni kwenda kinyume na kundi kubwa la watu.
LikeLike
Kabisa, kundi kubwa halijawahi kuwa sahihi inapokuja kwenye mafanikio.
LikeLike
Kwenda kknyume na kundi kubwa la watu
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante sana kocha,hii kanuni ya kwenye kinyume na kundi la watu ni muhimu kwangu kwa ajili ya mafanikio na mapambano ktk kazi na maisha yangu.
LikeLike
Vizuri, ifanyie kazi.
LikeLike
Kama hakuna mtu aliyekusema wewe ni freemason, basi utakua unafanya kwa kawaida.
Ukaaji wako kwenye mchakato unapaswa uwashtue watu kwa matokeo unayopata.
Asante sana Kocha Dr. Makirita Amani
LikeLike
Hakika, kama watu wanachukulia kawaida, unafanya kawaida pia.
LikeLike
Asante kocha mtapambania lengo ili kufikia malengo makubwa na kuwa kwenda kinyume na kundi
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante Kocha,
Nimejifunza ili kuwa na mafanikio makubwa usifuate tu mkumbo.
LikeLike
Vizuri, zingatia.
LikeLike
Simama kwenye kile kilicho sahihi bila ya kujali kundi kubwa linakuchukuliaje
LikeLike
Ndiyo, msimamo ni muhimu.
LikeLike
Kama watu hawashanai au kukuona umechanganyikiwa kwenye ndoto ulizonazo basi una maisha madogo sana
Asante sama
LikeLike
Hakika, na matokeo yako yatakuwa madogo pia.
LikeLike
Kukaa kwenye mchkato bila kuacha, kufanya kwa msimamo mkubwa, kuwa mbinafsi katika mambo yangu ya muhimu kabisa, kuwa na nidhamu ya hali ya juu sana mpaka watu waone kuwa ni freemason hivi ni viwango ambavyo navifanyia kazi lakini bado cja perfdect the craft. ni muda sasa wa kuboresha na kwa kuufanya kwa ubora kuliko mtu mwingine yeyote akiwemo mimi mwenyewe kwa siku iliyo pita.
LikeLike
Vizuri, jisukume kwenye viwango vya juu kabisa kwenye maeneo yote ili kuzalisha matokeo bora.
LikeLike
Kama hakuna watu wanaokuona una roho mbaya na hujali, unahangaika sana na mambo ya wengine kuliko mambo yako binafsi.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Kama kila mtu anakupenda na kukubali basi kuna mahali unakosea Na kama kila mtu anaamini kwenye ndoto zako kubwa ulizojiwekea basi ndoto zako sio kubwa Ni za kawaida.
Ninjiwekea ndoto kubwa ili watu wakisikia wasiamini na wanichukie.
Asante
LikeLike
Tuachane na vitu vya kawaida vilivyozoeleka na kila mtu.
LikeLike
Nitaweka viwango na nitavisimamia viwango hivyo ili kujilitea mafanikio makubwa bila kujali watu wananichukuliaje.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante kocha,Nitasimamia malengo yangu pekee na kuyasimamia bila kujali nani ananiongerea vibaya ninachojali ni kupambana na mafanikio.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Asante sana
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Ili kupata mafanikio makubwa ni kusimama kwenye kile kilicho sahihi bila kujali kundi kubwa la watu linakuchukuliaje.
LikeLike
Hakika
LikeLike
kama kila mtu anasema kwamba wewe ni mtu poa, basi inaelekea ndoto yako bado siyo kubwa sana.
LikeLike
Kueleweka na kila mtu ni hatari.
LikeLike