3216; Fokasi, Muda Na Msimamo.
Rafiki yangu mpendwa,
Kila kitu kinafanya kazi,
Kila biashara inalipa,
Kila kazi inaweza kukupa chochote unachotaka.
Lakini bado tunaona watu wanahangaika na mambo mengi na hawapati kile wanachotaka.
Siyo kwamba watu hao hawajui wanachotaka, wanakuwa wanajua sana.
Siyo kwamba wanakuwa hawajui wanachopaswa kufanya, wanakijua sana.
Na wakati mwingine siyo kwamba ni wavivu au wazembe, wanaweza kujitahidi sana tu.
Lakini hayo ambayo yalipaswa yamsaidie mtu, ndiyo yanakuwa kikwazo kwake.
Kwa kujua kile anachotaka, anakuwa anatamani sana kukipata kwa haraka.
Kwa kujua anachopaswa kufanya ili kupata, anahangaika kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja na hivyo yote anayagusa juu juu tu.
Na hali ya uchapakazi ambayo mtu anakuwa nayo anajikuta akipoteza nguvu nyingi kwenye mambo ambayo hayana tija kabisa.
Baada ya mtu kujua unachotaka na unachopaswa kufanya ili kukipata, unahitaji muunganiko wa vitu vitatu ambavyo kwa pamoja vina nguvu sana.
Vitu hivyo ni Fokasi, Muda na Msimamo.
Tukianza na fokasi, hapa ndipo wengi sana wanakwama, hasa pale wanapoona wamechelewa.
Wanakazana kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja, kitu kinachotawanya sana nguvu zao.
Hivyo wanatumia nguvu nyingi lakini matokeo yanakuja madogo, kwa sababu nguvu hizo wanazitawanya sana.
Kama wangekusanya nguvu hizo kwenye eneo moja, ambapo ndiyo kufokasi, wangezalisha matokeo makubwa zaidi.
Tukienda kwenye muda, tunajua dhahiri kwamba mambo mazuri yanahitaji muda kujijenga.
Lakini inapokuja kwenye ufanyaji, watu huwa wanasahau kabisa hilo.
Wanapoweka juhudi na wasione matokeo, wanaona juhudi hizo hazifanyi kazi.
Hivyo wanaacha na kwenda kwenye kitu kingine.
Huko nako hali inajirudia.
Ni lazima mtu ukubali kwamba muda unahitajika kwenye kujenga kitu chochote kikubwa.
Hakuna juhudi unazoweka zikapotea, bali zinakuwa zinajikusanya tu, wakati sahihi ukifika matokeo yatazalishwa kwa wingi na ukubwa.
Mwisho kuna watu ambao wamejipa muda mrefu kwenye kufanya kitu, lakini bado hakuna hatua kubwa ambazo wamepiga.
Wanaweza kulalamika jinsi ambavyo wamekuwa kwenye kitu fulani kwa muda mrefu.
Unaweza hata kuwaonea huruma kwa jinsi wameweka muda mrefu kwenye kitu.
Lakini unapochunguza kwa undani jinsi wanavyofanya ndiyo unaona wapi wamekuwa wanajikwamisha.
Wengi sana wanashindwa kufanya kitu kwa msimamo bila kuacha.
Wanaweza kupata shauku na hamasa ya kufanya kitu, wanafanya kwa siku chache kisha wanaacha.
Wanasubiri tena hamasa nyingine.
Kwa hiyo licha ya kuwa kwenye kitu kwa muda mrefu, matokeo makubwa yanakosekana kwa sababu ya kutokuwepo kwa ufanyaji kwa msimamo.
Fokasi, katika mengi ya kufanya, chagua moja ambalo ndiyo utalipa kila ulichonacho.
Jipe muda wa kutosha, mambo yote mazuri yanahitaji muda kujijenga na kukua.
Na fanya kwa msimamo bila kuacha, hata kama unafanya kidogo kidogo, wewe usiache kufanya. Inyeshe mvua, liwake jua, wewe fanya.
Ukiweka vitu hivyo vitatu pamoja, unakuwa kiumbe hatari sana hapa duniani.
Kwa sababu ni lazima utapata kila unachotaka, bila ya kujali ni njia ipi uliyoitumia.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Nitaweka fokasi muda na msimamo kwenye mambo makubwa mawili.Biashara na uwekezaji.Naamini kwa hakika kuwa yana uwezo wa kunifikisha kwenye ubilionea ninaouhitaji.
LikeLike
Nafanya kwa msimamo bila kuacha, inyeshe mvua, liwake jua nitafanya.
LikeLike
Nafokasi, inyeshe mvua, lije jua.
LikeLike
Fokasi, muda na nidhamu.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Asante kcha,
Fokasi, muda na msimamo kwa mafanikio makubwa
LikeLike
Jipe muda wa kutosha, mambo yote mazuri yanahitaji muda kujijenga na kukua.
LikeLike
Nitaweka Fokasi, muda na msimamo kwenye biashara ya kiwanda na uwekezaji linyeshe mvua, liwake jua lazima nifanye na mafanikio kwangu ni swala la muda tuu
LikeLike
Hakika kocha nimechagua machache kwenye mwaka mpya wa mafanikio nitauza gesi na vinywaji vya jumla na reja reja basi,vingine vyote vitasubiria.
LikeLike
Safi, weka nguvu kubwa hapo.
LikeLike
Baada ya kujua ninachotaka na ninachopaswa kufanya ili Kukipata nahitaji muunganiko wa vitu vitatu:-
1. Kufokasi kwa kuchagua moja ambalo ndiyo nitalipa kila nilichonacho.
2. Kujipa muda wa kutosha kwani mambo yote mazuri yanahitaji muda kujijenga na kukua.
3. Kufanya kwa msimamo bila kuacha, hata kama ni kidogo kidogo. Inyeshe mvua, liwake jua, wewe fanya.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Hii imeenda na kufika,fokasi, kujipa muda na kufanya kwa msimamo, maana naona kuna wakati vitu au Mambo yanatumima uimara wetu, hivyo utulivu ni muhimu sana ktk ukuaji wa biashara.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Jambo muhimu sana kupambania Fokasi,Muda na Msimamo Asante kwa Makala bora san
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kweli kabisa kocha fokasi na kulipa Jambo Muda ni muhimu Sana maana litafanikiwa tu
LikeLike
Hakika
LikeLike