3233; Usiseme, onyesha.
Rafiki yangu mpendwa,
Hii dunia haijawahi kuishiwa wasemaji.
Kila mtu anaweza kusema, kwa kupanga na kuahidi mambo mengi.
Lakini inapokuja kwenye ufanyaji, kuna uhaba mkubwa wa watu.
Ni watu wachache sana ambao ni wafanyaji kweli kwenye kile wanachotaka.
Kila mtu anataka mafanikio makubwa na utajiri.
Kila mtu anataka kuwa na maisha mazuri.
Lakini hi wachache sana ambao wanapata vitu hivyo.
Siyo kwa sababu hao wachache wamependelewa au wana bahati kuliko wengine.
Bali ni kwa sababu hao wachache ndiyo wapo tayari kutoka nje ya mazoea yao na kufanya vitu vipya na vikubwa.
Kama na wewe unataka kuwa sehemu ya hao wachache ambao wanapata kile wanachotaka, unachopaswa kufanya ni kuacha kusema na kuanza kuongesha.
Unapaswa kuacha maneno na kuweka kazi.
Chukua hatua kubwa na za tofauti.
Fanya vitu ambavyo hujawahi kufanya.
Nenda nje ya mazoea yako.
Wala siyo kwamba watu ni wavivu kihivyo.
Kinachowazuia kuchukua hatua siyo uvivu.
Bali ni ile hofu ya kushindwa au kupoteza pale mtu anapofanya kitu kipya na ambacho hajazoea.
Hivyo kinachohitajika hapa ni kubadili mtazamo.
Kwa sababu kinachofanya mtu ashindwe siyo kufanya na kushindwa, bali kutokufanya kabisa.
Ukifanya na kushindwa unakuwa umejifunza, hivyo wakati mwingine utafanya kwa ubora zaidi.
Lakini usipofanya, hakuna unachojifunza.
Kuna ambao huwa wanapata msukumo wa kuchukua hatua kubwa.
Na mwanzoni wanachukua hizo hatua kweli kweli.
Lakini hawapati matokeo waliyokuwa wanategemea kuyapata.
Na hilo linawapelekea kukata tamaa na kuacha.
Hiyo ni changamoto nyingine inayowakwamisha wengi.
Hutafanikiwa kwa kufanya mara chache au pale unapojisikia kufanya.
Bali utafanikiwa kwa kufanya kila mara, kwa msimamo bila kuacha.
Ni ule msimamo wa kufanya ndiyo wenye nguvu kuliko hata ukubwa wa ufanyaji wenyewe.
Kama huwezi kufanya kitu kwa msimamo na kwa muda mrefu bila kuacha, jua dhahiri kabisa kwamba hutaweza kupata matokeo makubwa unayotaka kuyapata.
Kinachopelekea ndoto za wengi kufa siyo kwa sababu haziwezekani.
Bali ni kwa sababu hawazipi ndoto hizo juhudi za kutosha.
Kuota pekee hakuna nguvu kubwa, kila mtu ana ndoto nyingi na kubwa.
Ni kuchukua hatua ndipo mafanikio yalipo.
Kufanya ndiyo kunazileta ndoto kwenye uhalisia.
Hivyo basi, unapokuwa na ndoto, unaweza kuchagua kuendelea kulala ili kufurahia ndoto hizo ila maisha yako halisi yakabaki vile vile.
Au unaweza kuamka na kwenda kuchukua hatua kwenye ndoto ulizonazo na ukaweza kuzileta kwenye uhalisia.
Pale ndoto zinaposhindwa, matendo huwa yanafanikiwa, mara zote.
Usiwe tu mtu wa kusema, onyesha kwa kufanya na hivyo ndivyo unavyoleta mabadiliko ya kweli na yanayokupa mafanikio unayoyataka.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asantee kocha nimejifunza kutumia matendo kuliko maneno hii itanifanya niweze kufikia ndoto zangu na kuwa mtu tofauti na wengi wanaoishia kupanga MIPANGO mingi ya maneno na kutekeleza hakupo asantee sana kwa ujumbe huu nakwenda kuufanyia kazi
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante kocha nitapambana kufanya bila kuchoka
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nashukuru kwa somo la leo kocha, kwamba sipaswi kuwa mtu wa kusema, bali kuonyesha kwa kufanya na hapo ndipo nitaleta mabadiliko ya kweli na yatakayo nipa mafanikio ninayotaka.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ni kufanya ndiko kunakoleta utofauti.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Naenda kuonesha matokeo Kwa vitendo
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante Kocha,
Nikifanya na kushindwa ninakuwa nimejifunza; hivyo wakati mwingine nitafanya kwa ubora zaidi. Lakini nisipofanya hakuna ninachojifunza.
LikeLike
Kweli
LikeLike
Asante sana kocha kwa somo zuri,onyesha kwa matendo siyo maneno,na ni kufanya mara nyingi ndiyo unaweza kufanikiwa, naendelea kumshkr Mungu kwa huu mwezi wa kumi na moja wenye baraka nyingi kwangu, leo tarehe kama yale ya mwezi huu nilifunga pingu za Ndoa takatifu, lakini mwezi huu ndiyo nilifunga biashara muhimu ni kuendelea kufanya na kuonyesha kwa matendo.asante.
LikeLike
Hongera sana kwa kumbukizi hizi muhimu sana kwenye maisha yake.
Najua umuhimu wake kwa sababu katika yote mawili uliweza kuvuka vikwazo ambavyo kwa muda mrefu vilikushinda.
Endelea kupambana.
LikeLike
Kufanya ndiyo kunazileta ndoto kwenye uhalisia.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Napaswa kuacha maneno na kuweka kazi.
Napaswa kuchukua hatua kubwa na za tofauti.
Napaswa kufanya vitu ambavyo sijawahi kufanya.
Napaswa kwenda nje ya mazoea.
Ili nionyeshe na sio kusema tu.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike