Hivi unajua kwa nini licha ya kuwepo kwa mafunzo mengi ya mafanikio bado watu wengi sana hawajafanikiwa? Jibu ni moja, mafanikio makubwa kwenye maisha ni matokeo ya mchakato na siyo tukio. Na mchakato huwa unachukua muda mrefu kuliko watu wanavyoweza kuvumilia.

Vitabu gani bado hujawa navyo hapo, wasiliana na 0678977007 kupata vitabu.

Mafanikio makubwa kwenye maisha siyo kitu kinachotokea mara moja au kwa ajali. Bali ni kitu kinachojengwa kwa muda mrefu, kwa juhudi ambazo mtu anakuwa anaziweza bila kuacha wala kuchoka. Mafanikio huwa yanajengwa hatua kwa hatua kwa kipindi cha muda mrefu.

Kwa sababu watu wengi huwa wanapenda kuona matokeo ya haraka na hawana uvumilivu wa muda mrefu, mafanikio makubwa yamekuwa yanashindikana kwao. Wapo wengi ambao wanakata tamaa katika kipindi ambacho walikuwa wameyakaribia kabisa mafanikio yao makubwa.

Ili kukusaidia wewe rafiki yangu uweze kukaa kwenye mchakato wa mafanikio kwa muda mrefu bila kuchoka wala kukata tamaa, ninakushauri uiishi kila siku yako moja kwa mafanikio makubwa.

Unaweza kutekeleza hilo la kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa kwa kuchagua kitu kimoja ambacho utakuwa unakifanya kila siku bila ya kuacha. Unaweza kuchagua chochote, lakini unapaswa kuhakikisha kinakuwa na sifa hizi;

1. Kinakuwa na mchango wa kukufikisha kule unakotaka kufika.

2. Hakitegemei mtu mwingine kufanya, yaani ni wewe tu.

3. Unaweza kukifanya kila siku bila kuacha.

4. Kinakuwa ndiyo kitu cha kwanza kwako kufanya pale tu unapoamka.

5. Unaweza kuendelea kuwa bora kupitia kujifunza na kufanya.

Tarehe 01/01/2015 nilichagua kitu hicho kuwa ni kuandika. Na tangu tarehe hiyo, kila siku bila kuacha, kwa miaka 9 sasa nimekuwa naandika kila siku makala za kurasa.

Katika kipindi hicho nimekuwa kwenye mazingira na hali mbalimbali ambazo zingeweza kuzuia hilo lisiwezekane. Lakini kwa sababu nilishaweka kama kitu cha lazima kufanya, basi nimekuwa naweza kufanya bila kukwama.

Leo tarehe 01/01/2024 nimechagua kitu kingine ambacho nitakuwa nakifanya kila siku bila kuacha. Kitu hicho ni kuendesha vipindi vya ONGEA NA KOCHA moja kwa moja kila siku kuanzia saa 1o kamili alfajiri mpaka saa 11 kamili alfajiri.

Rafiki, nakukaribisha tuungane pamoja. Hebu na wewe uchague kitu kimoja ambacho utakuwa unakifanya kila siku bila kuacha, kisha tuambatane pamoja. Karibu ushiriki vipindi hivi vya kila siku, ambavyo ni vya wazi kwa watu wote na iwe sehemu ya wewe kuendelea kuimarisha ufanyaji wa kile ambacho umechagua.

Kujiunga na channel maalumu ya kupata kipindi cha ONGEA NA KOCHA, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Karibu usikilize kipindi cha ONGEA NA KOCHA cha leo ili ujifunze kwa kina zaidi kuhusu dhana hii ya kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa kupitia kufanya kitu ulichochagua kila siku bila kuacha.

Angalia kipindi hapo chini.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

0678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 2. KISIMA CHA MAARIFA, 3. CHUO CHA MAUZO na 4. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.