3304; Kukwepa kuwajibika.
Rafiki yangu mpendwa,
Unakumbuka ulipokuwa mdogo na ukatamani sana kuwaonyesha watu jinsi unavyoweza kufanya mambo yanayofanywa na watu wazima.
Na baada ya kufanya hivyo yakageuka kuwa sehemu ya majukumu yako.
Yaani baada ya kuonyesha kwamba unaweza, ukaanza kupangiwa uyatekeleze.
Ni hali hiyo ya kuwajibika ndiyo imekuwa inapelekea watu wengi kutokuwa tayari kuonyesha uwezo mkubwa ulio ndani yao.
Unakuta mtu anaweza kabisa kufanya mambo makubwa, lakini anaficha hilo kwa sababu anajua akishaonyesha kwamba anaweza kufanya, atategemewa aendelee kufanya makubwa mara zote.
Sasa kwa kuwa watu wengi hawapendi kuwajibika, wanaona ni bora wafiche ule uwezo wao ili wasitegemewe kwa makubwa.
Pamoja na hilo kuwa changamoto, kwa wengi wenye uwezo kuuficha ili wasiwajibike nao, pia ni fursa nzuri kwa ambao wapo tayari kuwajibika.
Kwa kuchagua kuonyesha wazi uwezo mkubwa ulio ndani yako na watu wengi kuwa tayari kukutegemea kwenye uwezo huo unapata mafasi kubwa ya kutegemewa na walio wengi.
Ni kupitia kutegemewa huko ndiyo unaweza kufanya mambo makubwa na ya tofauti na kuzalisha matokeo bora na ya kipekee.
Kila unapokutana na watu wanaoficha uwezo wao mkubwa ili wasiwajibishwe nao, wewe ona fursa ya kuonyesha ulichonacho ili kuweza kufanya makubwa.
Kuwa kihere here wa kuonyesha wengine yote unayoweza kufanya, ili sifa zako zisambae kwa wengi zaidi.
Sifa zako zinapowafikia wengi, unakuwa na umejiweka kwenye nafasi nzuri ya kutoa thamani kwa wengi na hilo litakupa mafanikio makubwa.
Usiogope kutegemewa na wengi kwenye yale makubwa uliyoonyesha unaweza kufanya.
Hilo linakusukuma wewe kufanya kwa ubora zaidi kwa hao walio wengi.
Na hilo litachangia wewe kuweza kufanya makubwa zaidi na zaidi.
Mafanikio yoyote makubwa yanaanzia kwenye kuwa tayari kuwajibika kwa ukubwa na kwa wengi.
Fursa za kuwajibika huko zinapojitokeza, zitumie vizuri ili ziache manufaa makubwa kwako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Mafanikio makubwa yanatokana na kuthubutu kufanya yale makubwa ambao wengiine hawataki kufanya na ukifanya kwa ubora yataonekana na kukufanya wewe uwe bora zaidi
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Mafanikio yoyote makubwa yanaanzia kwenye kuwa tayari kuwajibika kwa ukubwa na kwa wingi
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nimechagua kuwajibika na maisha yangu, Nimekubali kwamba kila linalo tokea kwenye maisha yangu ni mimi nimesababisha. Nimeshika hatamu ya maisha yangu kwa kuchukua hatua sahihi kwenye kila jambo na kamwe sitalaumu au kumlalamikia yeyote juu ya matokeo ninayopata.
LikeLike
Vizuri na hongera sana.
LikeLike
Ukitaka mafanikio makubwa kuwa tayari kuwajibika
Asante
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nipo tayari kuonesha uwezo mkubwa nilionao, kuwajibika, nipo tayari kutegemewa mara zote kulingana na thamani kubwa ninayokwenda kutoa kwa jamii yangu kupitia biashara yangu
LikeLike
Vizuri, tekeleza hayo.
LikeLike
Sitaogopa kutegemewa na wengi kwenye yale makubwa niliyoonyesha naweza kufanya.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Kuwajibika,nipo tayari kujitoa kuwajibika pamoja na changamoto najua wapo watakaotambua kutokana na kuwajibika kwangu ili niwahudumie
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Mara zote sintakwepa kuwajibika kwa sababu mafanikio
yote makubwa yanaanzia kwenye kuwa tayari kuwajibika kwa ukubwa na wingi.
Asante kocha
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante Kocha,
Nitatumia kikamilifu fursa ya kuwajibika kwa ukubwa na kwa wengi ili kuyafikia mafanikio makubwa.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Mafanikio yoyote makubwa yanaanzia kwenye kuwa tayari kuwajibika kwa ukubwa na kwa wengi.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kuonyesha uwezo na kuwajibika.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike