3311; Tatizo sahihi na kazi.
Rafiki yangu mpendwa,
Tamaa ya kupata mafanikio makubwa kwa njia za mkato ni kitu ambacho hakijawahi kuisha kwa watu.
Kwenye kila zama huwa kunakuwa na njia za mkato ambazo huwa zinaibuliwa na kuonekana ni njia bora ya kufanikiwa bila kuweka kazi.
Lakini njia hizo hazijawahi kufanya kazi.
Njia ya uhakika ya kujenga mafanikio makubwa, ambayo imedumu vizazi kwa vizazi ni kutatua tatizo sahihi na kuweka kazi kubwa.
Tatizo sahihi ni lile ambalo linawakabili wengi na ambalo wapo tayari kuingia gharama kulitatua.
Na kazi kubwa ni kupitia kuweka juhudi kubwa ya kazi, kwa kutumia akili na nguvu.
Hivyo vitu viwili haviwezi kutenganishwa kwenye safari ya kujenga mafanikio makubwa.
Na ndiyo maana hata mataifa ambayo yamekuwa yanakuwa na nguvu kubwa duniani, yanakuwa na watu wengi na falsafa sahihi.
Uwepo wa watu wengi inatoa fursa ya tatizo kuwa sahihi, kwa sababu ya wingi wa watu ambao wanakuwa na tatizo linalotatuliwa.
Na uwepo wa falsafa sahihi inawafanya watu kuwa tayari kuweka kazi kwa sababu wanakuwa na uhakika wa kupata mafanikio makubwa.
Ukiangalia mataifa mawili, Marekani na Urusi, ni mataifa yenye watu wengi. Lakini Marekani limekuwa na mafanikio zaidi kwa sababu ya falsafa sahihi inayowafanya watu kuweka kazi zaidi kuliko Urusi.
Kadhalika taifa la China, lina watu wengi, ila miaka ya nyuma halikuwa na mafanikio kama yaliyopo sasa. Hiyo ni kwa sababu miaka ya nyuma halikuwa na falsafa sahihi inayowasukuma watu kuweka kazi kubwa.
Tumeangalia mifano ya mataifa, lakini ndivyo ilivyo hata kwa watu binafsi.
Ni utatuzi wa tatizo sahihi na kuweka kazi kubwa ndivyo vitakavyokupa mafanikio makubwa unayoyataka.
Yafanyie kazi hayo kwa uhakika na utapata unachotaka.
Epuka njia za mkato za mafanikio kama ukoma.
Usikubali kudanganyika kwamba zama zimebadilika.
Utatuzi wa matatizo sahihi na uhitaji wa kuweka kazi kubwa ni vitu vya zama zote, havitakuja kupitwa na wakati.
Visimamie vizuri na utaweza kufanya makubwa sana kwenye maisha yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kazi inahitaji mara zote kama unataka kufanikiwa.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Utatuzi wa tatizo sahihi.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante Kocha,
Utatuzi wa matatizo sahihi na uhitaji wa kuweka kazi kubwa ni falsafa ya kudumu daima.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Utatuzi wa matatizo sahihi na uhitaji wa kuweka kazi kubwa ni vitu vya zama zote, havitakuja kupitwa na wakati. Nitasimamia hivi siku zote
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Siku zote njia za mkato hazifai kabisa,tutatue matatizo kwa njia sahihi.
LikeLike
Kweli kabisa.
LikeLike
Kimbia njia za mkato Kama ukoma
Weka kazi na akili kupata mafanikio.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Tatizo sahihi na kazi ndio msingi wa mafanikio.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ni utatuzi wa tatizo sahihi na kuweka kazi kubwa ndivyo vita kavyo nipa mafanikio makubwa ninayo yataka.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Falsafa sahii na kuweka kazi tu basi ndiyo onayoleta mafanikio
LikeLike
Ndiyo
LikeLike