3433; Juu na chini…

Kutoka mezani kwa Kocha,

Rafiki yangu mpendwa,
Kwa kila jambo unalofanya, watu wengine huwa wanakuwa na maoni yao juu yake.
Maoni unayopata huwa yanatofautiana, kulingana na wale ambao wanakupa maoni na kile unachofanya.

Kwa wale ambao wako chini yako, watakupa maoni ya kukatisha tamaa.
Watakuonyesha jinsi gani mambo ni magumu na hayawezekani kabisa kwako.
Wengi walio chini wameshajaribu wakashindwa na hivyo kuchukulia haiwezekani kwa wote.

Kwa wale ambao wako juu yako, watakuoa maoni ya kukutia moyo.
Watakuonyesna jinsi gani mambo yanawezekana kabisa kwako.
Wote walio juu wameshafanya makubwa na kupiga hatua kubwa pia.
Wana uzoefu wa kufanya moja kwa moja na kupata matokeo.

Kamwe hutakuja kuambiwa kitu hakiwezekani na watu ambao wameshafanya nakubwa sana.
Wanajua kila kitu kinawezekana na wanao ushahidi wa hilo kupitia matokeo ambayo wameshazalisha wao wenyewe.

Pale mtu yeyote anapokuambia ndoto zako kubwa haziwezekani, usiyape nafasi hayo maoni yake.
Jua anaamini  vitu visivyokuwa sahihi kwa sabahu ndiyo uhalisia wa maisha yake.

Waepuke sana watu walio chini, kwa sababu huwa wanawavuta wengine nao washuke chini na wasiweze kabisa kupanda juu.

Uzuri ni kwamba watu huwa wanajidhihirisha wao wenyewe.
Huhitaji kupiga nao kelele sana, watajionyesha tu wao wenyewe kutokana na maoni watakayotoa kwenye ndoto zaki kubwa.

Wasikilize watu sahihi na wapuuze wasiokuwa sahihi.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr Makirita Amani.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe