HICHI NDICHO KINACHOKUZUIA WEWE KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA.

   Umewahi kuona mtu hajafanikiwa na hana mpango wowote wa kuelekea kwenye mafanikio ili hali ana uwezo wa kufikia lengo fulani? Unaweza ukamshangaa sana na kuona labda amelogwa ama ana matatizo. Watu wengi kwa kipindi fulani kwenye maisha yao wanapitia hali hiyo na wanaoweza kuitambua na kujiondoa ndio wanafikia mafanikio makubwa.

  Kila mtu ana eneo la faraja ‘comfort zone’ ambapo nje ya eneo hilo hawezi kutulia mpaka ahakikishe yuko kwenye eneo la faraja. Bila ya mtu kundolewa kwenye eneo la faraja ni vigumu sana kwake kuchukua hatua. Kama mtu ameshajiwekea eneo lake la faraja ataishi kwa hali hiyohiyo kwa muda wote ambao atakuwa anafarijika.

  Kwa mfano unaweza kukuta mtu ameajiriwa lakini kila siku anasema anataka kufanya biashara ila miaka inaenda anashindwa kuanzisha biashara. Mtu anaweza kufanya kazi isiyo na maslahi bora kwa zaidi ya hata miaka ishirini kwa sababu tu yupo kwenye eneo ya faraja. Kwa mfano mtu anaona kuwa na nyumba na kupata chakula na mahitaji mengine ya familia yake ndio faraja yake kwenye maisha. Anaweza akawa na uwezo wa kupata mengi zaidi ya hapo ila hafanyi kwa sababu hajapungukiwa.

  Watu wengi waliofanikiwa sana duniani historia zao zinaonesha walipitia mambo mengi magumu. Kuna ambao walifukuzwa kazi, wengine walifukuzwa shule, wengine walikosa hata pa kulala, wengine walitengwa kabisa na jamii. Mapito haya yaliwafanya waondoke kwenye ‘comfort zone ’ zao na kuangalia njia bora za kuwaepusha kupitia waliyopitia.

  Sikushauri ujipitishe kwenye hali ngumu ili kuondoka kwenye eneo lako la faraja, nachokushauri hapa ni kujitathmini wewe binafsi na kuna ni jinsi gani unaweza kufanya zaidi ya unavyofanya. Kila mtu anauwezo wa kufanya zaidi ya anavyofanya sasa hivi. HAKUNA UKOMO ZAIDI YA UNAOUWEKA MWENYEWE. KINACHKUFANYA USIFIKIE MAFANIKIO MAKUBWA NI UKOMO ULIOJIWEKEA KWENYE ‘COMFORT ZONE’ YAKO.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: