Mara nyingi sana watu wamekuwa wakiulizia wazo zuri la biashara. Wengi unakuta hela wanayo ila hawajui ni biashara gani wanaweza kuifanya na kupata faida nzuri. Au wanaweza kuwa kwenye biashara ambayo haifanyi vizuri na hivyo kuona walikosea kuchagua biashara na hivyo kufikiria kubadili na kuingia kwenye biashara nyingine ambayo wanaoifanya wanaonekana kupata faida.

BIASHARA NAFAKAbiashara

  Wewe ni mmoja wa watu waliojikuta kwenye hali hii na huna uhakika ufanye nini? Iwe tayari up kwenye biashara ama unampango wa kuingia kwenye biashara basi hii ni siri unayotakiwa kuijua. Sisemi siri ili uifiche, ila nasema ni siri kwa sababu wengi huwa hawaangalii upande huu. Tunakazana kufikiria mawazo mengi sana ya biashara ila ukishapata wazo hilo bado mambo yanakuwa magumu. Yote hiyo inatokana na kutokujua siri hii iliyo wazi.

  Biashara yoyote unayoona watu wanafanya basi ujue inalipa. Kama kuna mtu anafanya biashara zaidi wa mwaka mmoja na haifungi basi ujue kuna faida(hata kama ni kidogo) anaipata. Kama angekuwa hapati faida yoyote na anapoteza hela basi biashara isingeweza kuwepo zaidi ya mwaka mmoja. Kwa maana hiyo basi kila biashara inalipa na kila wazo la biashara ni wazo zuri na linalolipa. Hii ndio siri kubwa. Kujua tu hivyo hakutoshi kwa wewe kuingia na kuanza kufanya biashara(kitu ambacho wengi wanafanya)

BIASHARA4BIASHARA5

  Ni mara chache sana wazo la biashara linaweza kuwa jipya kabisa, mara nyingi tunapata mawazo ya biashara kutoka kwenye biashara zinazofanyika. Ni rahisi kujenga biashara kwenye mawazo ambayo yameshafanyika kuliko kwenye wazo jipya kabisa. Kwenye wazo jipya kabisa inabidi uwe na nguvu ya kutosha kutengeneza soko kitu ambacho ni kigumu kwa wajasiriamali tunaoanza na mitaji kidogo.

  Kwa kuwa biashara inafanyika na kuna wengi wanapata faida haimaanishi ujitose kwa mategemeo na wewe utaanza kutengeneza faida. Hilo ni kosa kubwa sana ambalo wajasiriamali wengi wanalifanya mwanzoni. Angalia wanaofanya biashara hiyo wanafanyaje na ujue ni njia gani unaweza kutumia ili uweze kunekana katika kundi. Tafuta ni kitu gani kinakosekana ama hakifanyiki ambacho ukikifanya wewe utatengeneza wateja wengi zaidi ya wenzako wanaofanya biashara hiyo. Kumbuka lengo la bishara yoyote ni kutengeneza wateja na ili kutengeneza wengi lazima utoe kitu cha tofauti kitakachowavutia.

  Kitu kibaya katika biashara ni ‘kukopi na kupesti’, na hiki ndicho kinachosababisha biashara nyingi kushindwa. Fikiria mtu mmoja kafungua bucha, biashara inaonekana nzuri, baada ya muda unakuta mabucha kumi kwenye eneo hilohilo na wote wanauza kwa mtindo mmoja wa kutundika nyama na kusubiri wateja. Tayari hapo biashara ni ngumu hivyo kwenda wewe wa kumi na moja na kutumia mbinu hiyo hali itakuwa ngumu zaidi kwako kwa sababu hujatengezeza wateja(la sivyo iwe ni eneo lenye watu wengi kama sokoni).

bucha

  Kama ukiweza kuumiza kichwa na kupata wazo la kufanya kwa tofauti unaweza kwenda kuweka bucha pembeni ya hayo mabucha kumi na ukauza kuliko wote. Hii itawezekana pale tu utakapchukua hatua ya kutaka kutafuta utofauti. Kwa mfano unaweza kuhakikisha nyama yako ni ya kiwango cha juu kila siku na ukaamua kuwapelekea wateja majumbani au ukawatafuta wauza vyakula wa eneo ulipo na kuwapelekea nyama. Hayo ni baadhi ya mawazo machache unayoweza kuyafikiria, yapo mengi.

  Kila biashara inayofanyika ni biashara yenye faida cha msingi ni wewe kujua uwezo na kipaji chako na jinsi ya kuweza kuvitumia kuwa wa tofauti kati ya wengi wanaofanya biashara unayofanya ama unayotaka kufanya.