UMEAMUA KUWAPOTEZA HAWA WATEJA MILIONI SITA?

  Kulingana na takwimu za mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), Tanzania inakadiriwa kuwa na watumiaji wa mtandao milioni 5.9. Kwa hesabu za karibu kuna watumiaji milioni sita wa mtandao Tanzania.

  Kutokana na takwimu hizi inaonesha Tanzania kwa sasa kuna soko kubwa sana kwenye mtandao. Kwa biashara yoyote unayofanya kuna wateja wengi sana unaoweza kuwafikia kama ukiweza kuutumia mtandao vizuri.

  Unaweza vipi kuutumia mtandao kwa manufaa ya biashara yako?

  Katika matumizi ya mtandao kibiashara kuna vitu ambavyo wengi tunavifahamu na kuna ambavyo unavifahamu ila hatujajua uzito wake kwenye maendeleo na ukuaji wa biashara yako.

mtandao

  Kuna njia kuu tatu za kuweza kuwafikia wateja wa kwenye mtandao kwa biashara yoyote unayoifanya. Mbili unazifahamu sana na huenda umeshazitekeleza, moja huifahamu vizuri ama unaitekeleza vibaya. Hapa utajifunza njia hiyo ya tatu kwa undani zaidi na uanze kuitumia kukuza biashara yako.

  Njia ya kwanza ya matumizi ya mtandao ni kuwa na website. Hii kila mtu anajua umuhimu wake na siku hizi kwa gharama ndogo sana unaweza kuwa na website na kuiweka biashara yako kwenye mtandao. Kama huna website mpaka sasa utakuwa umeamua makusudi kutowapata watumiaji wa mtandao.

  Njia ya pili ni kutumia mitandao ya kijamii, facebook, twitter, linkedin na mingine. Mtandao wa kijamii unaotumika sana na wafanyabiashara wengi wa kitanzania ni facebook kwa kuwa unaweza kutengeneza magroup na fan page ambako unaweza kutangaza biashara zako na kushirikiana na wateja wako. Pamoja na urahisi wa kutumia facebook kibiashara bado kuna watu wameshindwa kuitumia vizuri kwa ukuaji wa biashara zao.

  Njia ya tatu ambayo wafanyabiashara wengi wa Tanzania hawajajua nguvu yake ni kutumia blog. Nguvu ya blog katika kukuza biashara kwenye mtandao ni kubwa kuliko website na mitandao ya kijamii. Ninaposema blog sisemi na wewe uwe na blog ya udaku ya kuripoti sijui nani kapiga picha za uchi, hapana, namaanisha kuwa na blog inayoandika mambo mbalimbali yanayohusiana na biashara unayofanya. Kupitia blog unaweza kufanya mambo makuu matatu kwa biashara yako;

1. Kujenga imani kwa wateja. Siku zote wateja wanapenda mtu anaewajali na anaewapa taarifa zaidi juu ya matatizo yao na sio kuwauzia tu bidhaa ama huduma. Kwa kuwa na blog unakuwa unaandika taarifa mbalimbali za kufundisha, kuelezea ubora wa bidhaa ama huduma na pia kutatua matatizo watu wanayokutana nayo kwenye maisha yao ya kila siku. Tabia moja ya binadamu huwe tunawaheshimu na kuwaamini sana watu walioko tayari kutusaidia. Kwa kufanya hivi unajenga uaminifu mkubwa kwa wateja wako.

2. Kuwaleta watu kwenye website yako na kujua biashara yako. Duniani kuna website nyingi mno, na Tanzania kwenyewe kuna website zaidi ya milioni. Unafikiri ni kitu gani kinaweza kumfikisha mtu asiyekujua moja kwa moja kwenye website yako? Mara nyingi tunapokuwa na shida huwa tunaingia GOOGLE na kuandika tatizo letu kisha kupata sehemu za suluhisho. Kwa kuwa na blog inayondika jinsi ya kutatua matatizo ya watu yanayohusiana na biashara yako ni rahisi kwa watu kukufikia kupitia GOOGLE. Kwa kuwa blog utakuwa unaandika mara kwa mara(tofauti na website ambayo haibadilishi mara nyingi) ni rahisi kwa watu kukufikia kwa njia ya google.

3. Blog itakurahisishia mpango wako wa masoko kwa kuwa gharama yake ni kidogo. Kama una utaalamu kidogo wa kutumia kompyuta basi unaweza kuendesha blog yako mwenyewe au ukahitaji msaada kidogo sana. Hakuna gharama ya ziada utakayolipa kwa kuendesha blog, na unaweza kutenga masaa machache kwa siku kufanya shughuli zako za blog. Kama ratiba yako ni ngumu sana unaweza kutoa kazi hiyo ya blog kwa watu wanaoweza kufanya hivyo na ukalipa gharama kidogo.

 

  Kumbuka kwa kuwa na blog kunarahisisha kuweka makala kwenye blog na pia kuzipeleka moja kwa moja kwenye mitandao ya kijamii. Na blog nayozungumzia hapa ni vizuri ikawepo kwenye website ya biashara yako moja kwa moja.

  Amka na unufaike na soko hili kubwa la watumiaji wa mtandao tanzania.

  Kama biashara yako haina blog ama unablog il hujajua jinsi ya kuweza kuitumia vizuri kukuza biashara yako bonyeza hii link(maandishi haya) kwa msaada zaidi.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: