Safari ya kufikia mafanikio sio rahisi na wala haijawahi kuwa rahisi(soma; ingekuwa rahisi kila mtu ngefanya). Kuna magumu na vikwazo vingi njiani. Kila aliefanikiwa anahadidhi ndefu ya vikwazo alivyopitia. Na kila alieshindwa ana hadidhi ndefu zaidi ya vikwazo na jinsi vilivyosababisha yeye ashindwe.

vikwazo3

  Katika mzingira hayo ya magumu na vikwazo kuna wanaofanikiwa na kuna wanaoshindwa. Nini kinasababisha yote haya? Kama ulikuwa hujui ni vyema ukajua leo ili uweze kufikia malengo yako na kufanikiwa licha ya kuwepo kwa vikwazo vingi.

  Licha ya vikwazo vingine vyote, kuna kikwazo kikuu ambacho kinazuia watu kufikia malengo yao na kufanikiwa. Kikwazo hiki ni kigumu sana kukitambua na kukivuka na ndio sababu wachache wanafanikiwa na wengi wanashindwa.

  Kikwazo kikuu cha wewe kufikia mafanikio yako ni wewe mwenyewe, baasi. Huamini ama huelewi? Kikwazo kikubwa kinachowafanya wengi kutopata mafanikio ni wao wenyewe. Hivi vikwazo vingine vya kimazingira vinapata nguvu kutoka kwenye kikwazo kikuu ambacho ni wewe.

  Kama unapopitia magumu ama vikwazo unakubali vikushinde basi wewe mwenyewe ndio umejiandaa kushindwa na sio vikwazo vimesababisha ushindwe. Kuna watu wengi wamepitia ulikopitia na wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa sana. Kuna wengi wamefanya kazi unayofanya ama biashara unayofanya na wamefanikiwa sana. Na kuna wengi wanafanya hivyohivyo na wameshindwa.

vikwazo

  Kuna wengine hawana hata hivyo ulivyonavyo na bado wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa. Kila kada ya jamii kuna waliofanikiwa na walioshindwa, wote wanafanya kitu kimoja kwenye mazingira sawa. Hii inaonesha mazingira hayana mchango mkubwa sana kwenye kushindwa ama kufanikiwa kwa mtu. Bali kila kitu kinaanza na mtu mwenyewe.

  Vikwazo vyote kwenye safari yako ya mafanikio vinaanza na wewe mwenyewe. Kama ukikataa kukwamishwa na chochote hakuna kitakachokukwamisha. Kama ukikubali kukwamishwa basi kila utakachokutana nacho kitakuwa sababu ya wewe kushindwa.

   Amua kutokuwa kikwazo cha maisha yako, kuwa changamoto yako mwenyewe na ifurahie safari ya mafanikio. Unapokutana na vikwazo vifurahie maana unajua haviwezi kukutoa kwenye njia.

  Tafadhali bonyeza hapa kuipigia blog hii kura kwenye shindano la blogs tanzania. Ipigie kura blog amkamtanzania.blogspot.com