Katika makala ya hizi ndizo fursa unazozipita kila siku, niliahidi kuwatumia wanachama wa mtandao huu kitabu ambacho kina hadithi ya mkulima alieuza shamba lake kwenda kutafuta almasi. Mkulima yule hakuijua almasi inafananaje na hivyo hakuweza kupata almasi. Baadae ikaja kufahamika kumbe shamba alilouza lilikuwa na almai nyingi sana. Hadithi hiyo ina funzo kubwa sana juu ya fursa zinazotuzunguka.

acres of diamond

  Mara nyingi sana kuna fursa nyingi zinazotuzunguka ila huwa tunashindwa kuziona ama kuzitumia.
  Fursa hizo zipo kwenye maisha yetu ya kawaida, biashara tunazofanya ama kwenye ajira zetu.
  Kuweza kuzitambua na kuzitumia fursa hizi kutarahisisha sana safari yetu ya kufikia malengo mbalimbali tuliyojiwekea.
  Katika kijitabu hiki kidogo(kiuhalisia sio kitabu bali ni risala) mwandishi ameelezea kwa mifano jinsi ya kuweza kuzatambua fursa zinazotuzunguka.
  Kitabu hiki kimewasaidia wengi sana kuweza kuyabadili maisha yao na ya wanaowazunguka.
  Natumaini kitabu hiki pia kitatusaidia sisi kuweza kuyabadili maisha yetu na kufikia malengo tuliyojiwekea.
  Hata kama wewe ni mvivu wa kusoma ama umeshindwa kumaliza kusoma vitabu vingine nilivyotuma usiache kusoma kitabu hiki kwa sababu ni kifupi sana(kina kurasa 30 tu) na kina mambo mazuri sana.
Kitabu hiki kinaitwa 
ACRES OF DIAMONDS na risala hiyo iliandikwa na Russell H. Conwell.
Bonyeza haya maandishi hapa chini kudownload kitabu hiko
ACRES OF DIAMONDS by Russell H. Conwell.

  Jiunge na mtandao huu ili kupata vitabu vingine na mambo mengine mazuri yatakayokusaidia na kukutia moyo kwenye safari yako ya mafanikio. Kujiunga na mtandao huu bonyeza haya maandishi.
Kila la heri katika safari yako ya mafanikio.
Endelea kutembelea blog yako
AMKA MTANZANIA ili uendelee kupata mambo mazuri.
  Waalike marafiki zako nao wapate mambo haya mazuri