Hili Ndilo Kosa Kubwa Unalofanya Kwenye Maisha Yako Linalokuzuia Kufanikiwa.

Mafanikio sio kazi ndogo au lele mama, linapokuja swala la mafanikio sahau kitu kama kulala masikini na kuamka tajiri. Hakijawahi kutokea kitu kama hiko na hata kilipotokea kwa bahati mbaya hakikuweza kudumu.

Tumeshazungumza mengi sana kuhusu mafanikio kwenye AMKA MTANZANIA lakini pamoja na hayo yote bado kuna kosa kubwa sana linalofanywa na watanzania wengi ambalo linawazuia kufiikia mafanikio wanayotarajia. Kosa hili linafanywa na zaidi ya asilimia tisini ya watanzania, kwa maana hii hata wewe utakuwa mmoja wa watu ambao wanalifanya kosa hili kila siku kwenye maisha yako.

Unaweza kuwa unatumia kila juhudi ili uweze kufikia mafanikio ila unashanga huyapati, wakati kuna baadhi unaona hawahatumii nguvu kama wewe ili mafanikio yao ni makubwa. Yote hii inatokana na kosa hili ambalo unafanya kila siku.

Abraham Lincolin aliwahi kusema “nipe masaa sita ya kukata mti, nitatumia masaa manne ya kwanza kunoa shoka langu”. Hii ina maana kwamba masaa mawili atakayotumia kukata mti ametumia mara mbili yake(masaa manne) kuandaa kifaa chake muhimu na hii inamrahisishia kazi.

Kwenye maisha wengi wanapokutana na mti wao wanachofanya ni kuchukua shoka na kuanza kuushambulia mti kwa kutumia nguvu nyingi sana. Kwa kuwa shoka sio kali ni vigumu sana kuweza kukata mti. Sasa chukua mfano huu na uweke kwenye maisha yako, wewe ndio shoka na mti ni kazi au changamoto unayokutana nayo kwenye maisha yako.

Je umejiandaa kiasi gani kabla ya kuanza kufanya kazi yako au kabla ya kukabiliana na changamoto unayokutana nayo? Utashangaa zaidi ya asilimia tisini ya watu hawana maandalizi yoyote, wanashambulia kazi au tatizo kwa sababu liko mbele yao. Hili ndio kosa kubwa sana kwenye maisha yako.

Ni kosa kubwa kwa sababu unatumia nguvu nyingi na unashindwa kufikia mafanikio. Ni kosa ambalo umekuwa unalirudia kila siku kwenye maisha yako na linakuzuia wewe kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako.

kitabu kava tangazo

Unawezaje kuepuka kosa hili?

Njia kubwa ya kuepuka kosa hili ni kuwekeza ndani yako mwenyewe na kujiandaa kabla ya kufanya kazi au kukabiliana na changamoto unayokutana nayo. Kuna njia nyingi sana unazoweza kuzitumia kuwekeza ndani yako na kujiandaa kwa changamoto zozote unazoweza kukutana nazo kwenye maisha, kazi au hata biashara yako. Hapa nitaeleza njia tatu muhimu unazoweza kuanza kuzitumia ili uweze kunoa shoka lako;

1. Jifunze kila siku.

Kama mpaka sasa unafikiri kujifunza kuliisha ulipohitimu masomo basi shoka lako tayari lina kutu. Kama kweli unataka kufikia mafanikio jifunze kila siku. Jifunze mambo mbalimbali kuhusu kazi au biashara unayofanya, na hata maisha kwa ujumla. Unaweza kujifunza kwa kujisomea vitabu, kusikiliza vitabu vilivyosomwa au hata kujifunza kwa kupitia mtandao kama AMKA TANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA. Kama unataka kupata vitabu vilivyosomwa ambavyo unaweza kusikiliza na kujifunza popote ulipo bonyeza maandishi haya.

2. Hudhuria semina mbalimbali.

Kuna semina nyingi sana zinazofanyika mara kwa mara ambazo zinaweza kukusaidia sana kuongeza ufanisi wako na kukuwezesha kukabiliana na changamoto. Semina zinatoa elimu na uhamasishaji mzuri sana unaoweza kukusikuma kufanya mambo makubwa kwenye maisha yako. Fuatilia semina zinazofanyika na kisha hudhuria semina hizo, utapata thamani kubwa sana zaidi ya gharama utakayolipia.

3. Jifunze kutoka kwa wengine.

Unaweza kuwa na mtu wa kukuongoza na kukufundisha kwenye kitu unachofanya au unachotaka kufanya. Mtu huyu anakuwa anakufuatilia kwa karibu na kukuambia unapokosea na kukurekebisha. Kwa jina lingine mtu huyu tunamuita MENTOR. Kama unataka kupata mtu wa kukufuatilia, kukufundisha na kukuelekeza kwenye kile unachofanya nitumie email kwenye amakirita@gmail.com kisha nitakutumia maelezo ya MENTORSHIP PROGRAM ya AMKA MTANZANIA.

Kwa vyovyote vile hakikisha shoka lako(wewe mwenyewe) ni kali kabla ya kuchukua jukumu la kukata mti(kazi au changamoto unayokutana nayo). Kwa kufanya hivi utaona mafanikio makubwa sana kwenye maisha yako na shughuli yoyote unayofanya.

Nakutakia kila la kheri kwenye harakati zako za kuboresha maisha yako na ya watanzania wenzetu.

TUKO PAMOJA.

Tafadhali endelea kuwaalika marafiki zako kulike page yetu ya facebook. Bonyeza maandishi haya na kisha like halafu nenda sehemu ya invite friends kisha waalike nao walike ukurasa huu ili tuweze kuwafikia wengi zaidi. Naomba sana ushirikiano wako kwenye hili na utakuwa balozi mzuri wa kuwaamsha watanzania wenzetu. Asante sana kwa ushirikiano wako.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: