Tumia Asilimia Hii Tatu(3%) Tu Na Uone Mabadiliko Makubwa Kwenye Maisha Yako.

Wiki iliyopita niliweka makala kuhusu UWEKEZAJI MUHIMU kwenye maisha yako. Tuliona kwamba uwekezaji muhimu kuliko wote ni uwekezaji kwenye maendeleo yako binafsi.

Kama tunavyojua hakuna maendeleo kama hakuna uwekezaji, hivyo ndivyo ilivyo kwenye maendeleo yako binafsi. Ni lazima uwekeze ndio uweze kuona maendeleo yako binafsi. Na unapokuwa na maendeleo binafsi ndio unaweza kuona mabadiliko makubwa kwenye maisha yako kuanzia kipato mpaka kwenye hadhi ya maisha.

jiendeleze

Na kama ilivyo kwenye uwekezaji wa aina yoyote ile ni lazima kuna kitu unatakiwa kukitoa. Inawezekana ikawa muda, au ikawa fedha au vikawa vyote. Katika uwekezaji wetu wa maendeleo binafsi, muda na fedha vyote vinahusika.

Uwekezaji wa muda.

Unahitaji kutenga muda kila siku kwa ajili ya kutafakari maisha yako, kuweka malengo na mipango ya maisha yako, kujisomea na hata kujitathmini ni wapi unaelekea na maisha yako. Hakuna njia ya mkato kwenye kutumia muda wako kuboresha maisha yako na hakuna anayeweza kukufanyia yote hayo.

Uwekezaji wa fedha.

Unahitaji kutenga fedha kwa ajili ya kujiendeleza wewe binafsi. Unahitaji kununua vitabu vizuri vya kujisomea, kulipia mafunzo mbalimbali ya kukuendeleza, na hata kununua vitabu vilivyosomwa(AUDIO BOOKS) kwa ajili ya kujifunza zaidi.

Hakuna njia yoyote unayoweza kutumia kukwepa hili kama kweli unataka kuongeza thamani na ubora wako.

Unapata wapi fedha kwa ajili ya kuwekeza kwenye kujifunza?

Najua unachokisema kwamba kipato changu ni kidogo hivyo siwezi kupata fedha ya kulipia kitu chochote cha kuniendeleza. Na nakuambia kwamba kinachosababisha mpaka sasa hivi ushindwe kulipia mafunzo au kununua vitabu vya kukuendeleza ni kwa sababu hujapata elimu hii. Na kukosa elimu nzuri ya kukuendeleza ndio kumesababisha mpaka sasa unaona maisha yako ni magumu na hata ukipata fedha hujui zinakwenda wapi.

Sasa kuanzia sasa weka mpango wa kujifunza na kujiendeleza kuwa sehemu ya maisha yako. Katika kipato chochote unachopata weka asilimia tatu pembeni kwa ajili ya kujifunza na kujiendeleza binafsi.

Kama unapata tsh elfu kumi weka pembeni tsh mia tatu, kama unapata laki moja weka pembeni elfu tatu na kuendelea. Fedha hii iwekeze kwenye maendeleo yako kwa kununua vitabu, AUDIO BOOKS, kulipia mafunzo mbalimbali. Fanya hivi kwa mwaka mmoja tu na utaona mabadiliko makubwa sana kwenye maisha yako.

Kama mpaka sasa unasumbuka na kupata au kutunza fedha zako nakushauri leo hii ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA ili uanze kutatua tatizo lako la fedha. Mwezi huu wa nane ndani ya KISIMA CHA MAARIFA tunajadili kuhusu kujenga tabia nzuri ya matumizi ya fedha na jinsi ya kuongeza kipato. Usikose mafunzo haya mazuri ambayo yatakuletea ukombozi kwenye maisha yako.

Unaweza kuona ni gharama kubwa sana kupata mafunzo ya kujiendeleza binafsi ila hujajua ni gharama kiasi gani unaingia kwa kukosa mafunzo haya. Unapoteza nusu ya muda na fedha zako bila ya wewe kujua. Unashindwa kufanikiwa kwenye kazi, biashara na hata maisha kwa sababu hujui ni mbinu zipi zitakuwezesha kufikia mafanikio.

Amua sasa kufanya maendeleo yako binafsi kuwa sehemu ya kwanza kwenye maisha yako. Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi hayo na uchague uanachama utakaohitaji na uanze kuchukua hatamu ya maisha yako. Kwa tsh elfu kumi(10,000/=) tu kwa mwaka utapata nafasi ya kujifunza na kujenga tabia zitakazokuwezesha kufikia mafanikio makubwa.

Nakutakia kila la kheri kwenye maendeleo binafsi ya kukuletea ukombozi kwenye maisha yako.

TUKO PAMOJA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: