Tumia Kanuni Hizi Tatu(3) Za Muhimu Sana Ili Uweze Kumfanya Mteja Asikukimbie Kwenye Biashara Yako

Siku zote ni rahisi kumpata mteja ila ni vigumu kumfanya abakie kuwa wako. Hili ni tatizo kubwa linalowakumba wafanyabiashara wengi, wateja wanakuja kwenye biashara zao mara moja au mbili kisha hawaonekani tena, jambo ambalo limekuwa likiibua hisia tofauti kwa wafanyabiashara. Wafanyabiashara wengine wanasema wamerogwa au bidhaa ni mbaya. Unakuta mtu ana bidhaa nzuri, huduma inaridhisha lakini anashindwa kumfanya mteja anayekuja kwenye biashara yake aendelee kuwa mteja wake wa kudumu. Tatizo Hili linatokana na huduma mbaya kwa wateja inayosababishwa na mazingira yasiyovutia, lugha mbaya na mteja kutohudumiwa kwa wakati.

Kwa upande mwingine tatizo hili linasababishwa na kutokuwa na utashi wa kujua aina za wateja maalumu na namna maalumu ya kuwahudumia kwa maana ya tabia zao na namna ya kuwahudumia. Wafanyabiashara wengi wamekosa utashi wa kujua aina za wateja, tabia zao na namna ya kuwahudumia, suala linalosababisha kuona kuwa wateja ni watu wa kutanga tanga, hawashikiki au hawana sehemu maalumu ya kununua bidhaa au huduma, jambo ambalo si kweli. Tambua kuwa Kutanga tanga kwa wateja kuna sababishwa na wafanyabiashara wenyewe kushindwa kuwafanya waendelee kubaki kuwa wao na wasiende kwingine. Huna haja ya kwenda kwa mganga ili kumfanya mteja abakie kuwa wako, bali ni kwa kutumia kanuni za kibiashara ambazo ni kuuza bidhaa zenye ubora, kutumia lugha nzuri, kuwa mbunifu, kumpa mteja zaidi ya kile alichokitarajia. Kanuni tatu za kumfanya mteja asikukimbie kwenye biashara yako

1. Kuwa mbunifu

Tambua kuwa ili uweze kumfanya mteja asikukimbie kwenye biashara yako ni lazima uwe mbunifu katika biashara unayoifanya na Kutokana na ubunifu huo wateja wanakuwa wengi kwasababu wanavutiwa na wanahisi kuwa wanapata zaidi ya kile wanachokilipia, wanaridhika na kuifurahia huduma hiyo na wengine wanashindwa kuvumilia kuridhika huko na kufurahishwa, matokeo yake wanawaambia wenzao na wenzao wanawaambia wenzao! .Matokeo yake habari nzuri zinasambaa kuhusu huduma yako au bidhaa, wateja wanazidi kumiminika, unajikuta umejenga mtandao mkubwa wa wateja na kushinda ushindani ulioko kwenye biashara husika.

2. Mpe mteja zaidi ya kile alichokitarajia

Mara nyingi wafanyabiashara wanajisahau katika hili la kumpa mteja zaidi ya kile anachokitarajia, wanafanya hivyo wakati wanaanzisha biashara zao mpya, wakiona biashara imezoeleka kidogo wanasitisha na wateja nao wanakata miguu. Hapa sizungumzii promosheni bali nazungumzia jambo endelevu litakalomfanya mteja aendelee kuwa wako na asiende kwa mtu mwingine. Kumpa mteja kitu cha ziada zaidi ya kile alichokuwa anakitarajia kutoka kwako, namaanisha kile kitu ambacho ukimpa hakiwezi kuathiri biashara yako na hapa ni suala la ubunifu zaidi ndio unahitajika. Kwa haraka ukiangalia unaweza kuona unapata hasara lakini ukifanya uchunguzi wa kina utagundua kuwa sehemu hizo zinapata faida kubwa ukilinganisha na idadi kubwa ya wateja wanaokuja katika biashara hiyo .

3. Uza bidhaa zenye ubora.

Sehemu nyingine nimeona wafanyabiashara wanaouza biashara nzuri ila wanakabiliwa na ukosefu wa wateja wa kutosha na kuamua kutumia mbinu ambazo hazizai matunda. Mfano unakuta nje ya biashara kuna bango limeandikwa: “Ukimleta mteja akanunua bidhaa tunakulipa.”Binafsi niliona kuwa mbinu hii haina ushawishi mkubwa na inaonekana kuwa inashurutisha zaidi na ni ya kizamani, wafanyabiashara hao wamekosa utashi wa kibiashara, mbinu za kijasiriamali ambazo wakati mwingine hazihitaji matumizi makubwa ya nguvu ya pesa au mwili, bali ni kufuata mbinu na kanuni za kijasiriamali, kisha utashangaa wateja wanakuja, huna haja ya kutafuta watu wakupigie debe biashara yako. Mbinu hizo nilizozitaja hapo juu na juhudi za kuwavutia wateja katika biashara yako zinatakiwa ziambatane na utashi wa kujua aina za wateja, tabia zao na namna ya kuwahudumia ili uweze kupata mbinu zaidi zitakazokupa nguvu na uwezo wa kumfanya mteja abakie kuwa wako. Endelea kutembelea mtandao huu wa AMKA MTANZANIA kwa mambo mazuri ya kujielimisha na kujihamasisha na kuwa bora zaidi jiunge na KISIMA CHA MAARIFA.

Tunakutakia mafanikio mema katika biashara yako na TUPO PAMOJA.

Makala hii imeandikwa na Geofrey Mwakatika, Unaweza kutembelea blog yake Geofrey Mwakatika kujifunza zaidi.

kitabu-kava-tangazo4323

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: