Mafanikio ni tabia, vingine vyote ni nyongeza tu.
Unaweza kuiweka kauli hiyo mahali ambapo unaweza kuiona kila siku ili iwe msisitizo kwako kuchukua hatua ya kujijenge atabia nzuri na zitakazokufikisha kwenye mafanikio.
Kwanza kabisa tunaanza kwa kujenga tabia, halafu baadae ytabia zinatujenga.
Kwa mfano kama umewahi kujifunz akuendesha baiskeli ilikuwaje siku za mwanzoni? Uliona ni kitu kigumu sana, ulikuwa unaanguka mara kwa mara. Lakini ni kitu gani kilitokea baada ya kujua kuendesha baiskeli? Ilikuw akitu cha kawaida kwako, wala huna haja ya kufikiria kwamba ni kitu kigumu. Na wakati mwingine unaweza hata kuachia mikono na kuendesha kwa manjonjo.
Tuchukue pia mfano wa kuendesha gari. Hebu fikiria wakati unajifunza ilikuwaje? Uliona ni vitu vingi vya kufanya, mguu kwenye breki, mguu kwenye mafuta, huku unaangalia mbele, mara kukata kona na vingine vingi. Vyote hivi vilionekana ni vitu vingi na vigumu. Lakini ilikuwaje baada ya kujua kuendesha gari? Sasa unaweza kuendesha huku unaongea na siku au hata ukiwa unajiremba(kama ni mwanamke).
Kitu kikubwa cha kugundua hapa ni kwmaba unatumia kazi kujenga tabia lakini tabia hii ikishakuwa sehemu ya maisha yako basi inajiendesha yenyewe, huna tena kazi ya kuanza kuifikiria tabia hii kila siku.
Na hivi pia ndio inavyokuwa kwa tabia mbaya. Kama una tabia mbaya uliyojijengea sio kwmaba utailazimisha iwepo, bali inaendele akuwepo kwa sababu imeshakuwa sehemu ya maisha yako.
Leo nataka tujadili kwa nini ni vigumu kuondokana na tabia mbaya na jinsi gani unaweza kushinda ugumu huu.
Kama tulivyoona hapo juu ni vigumu kuondokana na tabia mbaya kwa sababu sio wewe unayeendesha tena tabia, bali tabia ndio inakuendesha. Tabia inakuwa kwenye akili yako ya ndani(subconscious) ambayo inafanya akzi bila hata ya wewe kufikiri. Wakati wewe unapambana kwenye akili yako inayofikiri(conscious) mambo yanaendelea yenyewe kwenye akili yako ya ndani.
Jambo muhimu sana la kuzingatia kwenye kuacha tabia mbaya ni kutafuta tabia nzuri ambayo utakuwa unaifanya kwenye ile nafasi ya tabia mbaya. Kwa sababu tabia haikai yenyewe, huwa inachochewa na vitu, basi hakikisha kwamba pale ambapo tabia inachochewa basi kuna kitu unacho cha kufanya. Hii itakuzuia wewe kurudi kwenye tabia yako ya zamani.
Kwa mfano tuseme unataka kuacha pombe, na muda wako mwingi unaokunywa pombe ni muda ambao sio wa kazi, yaani muda wa mapumziko. Hivyo mwili wako unajua baada ya siku nzima ya kazi kinachofuata ni kunywa pombe. Hata kama utakazana kiasia gani kuacha, utajikuta unasukumwa kwenda kwenye pombe. Kikubwa cha kufanya hapa ni kutafuta kiti ambacho utakuw aunakifanya baada ya kazi. Kwa mfano labda unaweka utaratibu wa kujisome akila baada ya kazi, au utaratibu wa kufanya mazoezi au utaratibu wa kuendeleza kipaji chako. Mwili wako utaanza kuhusisha tabia hizi mbili na kitakuw akitu cha kawaida kwako kufanya.
Vile vile unapotaka kujenga tabia nzuri usianze kuijenga peke yake, bali ihusishe na tabia nyingine ambayo tayari unaifanya. Kwa mfano kama unataka kujijenge atabia ya kujisome akila siku asubuhi, basi unganisha kile unachofanya kila siku asubuhi na kujisomea. Kw amfano kila unapoamka kitandani labda unaoga sasa fanya ukishamaliza kuoga ni kukaa na kusoma au kukaa na kuandika. Akili yako itaanza kuunganisha vitu hivi pamoja na baada ya muda hutakuwa na haja ya kulazimisha kitu kitokee inakuwa kawaida kwako.
Vile vile kwa tabia ya matumizi mazuri ya fedha ambayo ndio inawapa changamoto wengi unaweza kutumia mbinu hii. Ifanye kuwa tabia kwako kuweka akiba kila unapiopata kipato. Najua kwa sasa umeunganisha tabia mbili kuu, kipato na matumizi. Hujawahi kujiuliza kwa nini ukiwa na fedha matumizi hayakosekani na usipokuwa nazo baadhi ya matumizi hupotea yenyewe? Sasa unahitaji kutengeneza tabia nyingine ya kuhusisha kipato na akiba. Weka utaratibu kwmaba kila unapopokea fedha tu, kiasi fulani kinakwenda pembeni. Mwanzoni itakuwa vigumu kama ilivyokuw akwenye kuendesha baiskeli au gari. Lakini kadiri siku zinavyokwenda utaanz akuona ki kitu rahisi sana kufanya.
Kitu kingine muhimu sana kuzingatia kwneye kuondokana na tabia mbaya au kujenga tabia mpya ni kuwa mvumilivu. Kama ulivyokuw amvumilivu mpaka ukajua kuendesha baiskeli, kama ulivyokuwa mvumilivu mpaka ukajua kuendesha gari, basi unahitaji uvumilivu huo pia. Kunaw akati utaanguka, usione kama huu ni mwisho, bali anza tena na wakati huu hakikisha unakijua kile kinachokuangusha ili uweze kukikwepa.
Kitu cha mwisho kabisa ninachopenda kukushiriksiha wka siku ya leo ni kama una tabia nyingi unataka kuzijenga au unataka kuondokana nazo, basi usifanye zote kwa wakati mmoja. Anza na tabia moja au chache zinazoendana na ukimalize nenda wkenye tabia nyingine. Hakikisha unakuwa na vitu vidogo sana vya kufanya kiasi kwmaba huwezi kuacha kuvifanya.
Ni tabia gani unataka kuijenga, kuimarisha au kuondokana nayo kwa mwezi huu wa saba? Nijulishe ili niweze kukusaidia katika safari hiyo.
Nakutakia kila la kheri katika kujijengea tabia za mafanikio.
TUPO PAMOJA.