Shuhuda Za Walioshiriki Semina Zilizopita Kwa Njia Ya Mtandao.

Habari za leo rafiki?
Naamini uko vizuri sana, hongera kwa hilo. Na endelea kuweka juhudi ili maisha yako yaendelee kuwa bora zaidi.
Kumbuka ubora hauna kikomo, haijalishi umefikia wapi kwa sasa, bado unaweza kuwa bora zaidi ya ulivyo leo. ndio maana kila siku tunakuandalia makala bora za kukuwezesha kuwa bora zaidi.
Naomba nikukumbushe kwamba zimebaki siku mbili za kuweza kujiunga na semina MIMI NI MSHINDI, Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu.
Semina hii ambayo itakukumbusha na kufufua ule ushindi ambao upo ndani yako, itaendeshwa kwa njia ya mtandao kupitia email, kundi la wasap na mesej za kawaida.
Mwisho wa kujiunga na semina hii ni ijumaa tarehe 02/10/2015 na mafunzo ya semina yanaanza jumatatu tarehe 05/10/2015. Ikishapita ijumaa hutakuwa tena na nafasi ya kujiunga na mafunzo haya mazuri sana. Hivyo fanya hima kama bado hujajiunga na ujiunge sasa ili usikose mafunzo haya mazuri sana.

CHETI UTAKACHOPATA BAADA YA KUSHIRIKI SEMINA HII.

 
Leo nakushirikisha shuhuda za baadhi ya wasomaji ambao walishiriki kwenye semina zilizopita ambazo tuliendesha kwa njia ya mtandao. Kama hujawahi kushiriki semina hizi na labda una wasiwasi kama kweli utajifunza vizuri, pitia shuhuda hizi kisha utaona mwenyewe kama semina hizi zinakufaa au la.
Karibu ujifunze kupitia shuhuda hizi ambazo zilitolewa baada ya semina ya MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA ambayo iliendeshwa mwezi wa tano mwaka huu 2015.
Habari za leo, hakika nimejifunza mengi sana ambayo sikuwa nayafahamu ama sikuwa na uelewa nayo katika pilika za ujasiriamali ukweli kila jambo linahitaji kujifunza aidha kupitia mtu mwingine ama kutokana na changamoto utakazopitia mimi binafsi naweza kusema nimenufaika na nimeweza kufuatilia mada hii takribani kila mada uliotuma kwa kila siku na hata kuzirudia kwani nimetumia muda mwingi wa asubuhi kusoma mada hizi nikipanda daladala tu nafungua email yangu nakuta mada naanza kusoma mpaka nikifika kwenye majukumu yangu nakuwa nimemaliza mada, wakati mwingine nikisafiri safari ndefu basi narudia mada hivyo natumai nitakuwa nimeondoka na jambo fulani ambalo kama sio leo basi kesho  litanisaidia katika mapambano ya ujasiriamali na mada ya leo naimalizia kwa kuisoma nikiwa ndani ya daladala kutokea kibaha kuja dar hivyo ni namna gani nimetumia muda wa kusoma mada bila kuanza kushangaa na kufanya mambo yasiyo ya msingi.
Nakupa pongezi na naomba nishirikishe katika mada zijazo kunako majaliwa tutashirikiana na kama yapo mambo ya vitabu ama vipeperushi tuma kwa anwani yangu ya posta hapo chini nakutakia kila la kheri katika uelimishaji wako wa ujasiriamali. Mwenyezi Mungu akupe nguvu na moyo wa kuendelea.
Karibu Iringa. Tuwekeze katika kilimo cha miti kwa ajili ya maisha ya kustaafia ili kuepuka kuhangaika uzeeni kunako majaliwa.
Ahsante.
Kilua Mbezi
kiluwa9@gmail.com
Asante sana Amani kwa kutupatia elimu ya chuo kikuu kwa njia ya mtandao. 
Nimeshaanza kufanyia kazi . naamini nitatoa mrejesho kwa hatua nitakazofikia.
Ombi kwa upande wangu. kupata mafunzo kama haya jinsi ya kuweka akiba/uwekezaji katika taasisi mbalimbali  na tabia za pesa  kwa undani kidogo. Nikiangalia makala ulizokwishatoa kuhusu mada hii zinakuwa ni fupi kidogo kidogo .
joyce shoo joycek1969@yahoo.com
Habari.
Natoa shukrani nyingi kwako kwa namna unavyojitoa ili kutuelimisha na kutuonesha njia ya kufikia mafanikio.
Binafsi sina biashara lakini hapa nimejifunza na nimeng’amua kwamba hobby yangu inaweza kugeuka na kuwa biashara. Nafuga kuku wa asili kama hobby tu. Sasa nimeona njia ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa kwa kuigeuza hobby kuwa biashara.

Nakiri kwamba baada ya mafunzo haya sasa naziona fursa nyingi sana kuliko kabla.
Asante sana. Mungu akubariki na pia abariki kazi zako.
Tuko pamoja.
Bridget Mbawala
bridgetgm@gmail.com
Habari ndugu Amani, binafsi nashukuru sana kwa mafunzo haya. Somo kubwa nililojifunza kwenye mafunzo haya ni UMUHIMU wa kuwa wa tofauti na wa kipekee kwa kile unachofanya na maisha kwa ujumla. Na Ili kuwa wa tofauti na wa kipekee ni lazima upate maarifa sahihi ya kufanya kazi zako kwa ubora wa hali juu. Nimepata kujua mengi ambayo mwanzoni sikujua. Mifano chache ya hayo niliojifunza ni; 1) IMANI nzuri ina nafasi kubwa sana kwa mafanikio ya biashara yako (Kujiamini binafsi na kuamini juu ya kile unachofanya) 2.Jifunze juu ya kile unachofanya ili kuepuka kuwa wa kawaida. 3.Nimejua jinsi ya kushinda mshindani wako, kwamba nisifanye kazi ya kutaka kumwondoa yeye au kushindana na yeye bali kuangalia kuwa bora kwenye kazi yako kila siku. Kutatua matatizo ya watu, kutengeneza thamani. Nimejifunza mengi na NIMEJITOA KUYAFANYIA KAZI ILI NIFIKIE MAFANIKIO NINAYOYATAMANI.
Kazi njema!
Ngutiti Molell ngutitim@gmail.com
Hizi ni baadhi tu ya shuhuda nyingi ambazo washiriki wa semina hizi wamekuwa wanazitoa.
Je na wewe usingependa kuona maisha yako yakibadilika kwa kupata maarifa sahihi ambayo ukiyatumia yatakuletea manufaa?
Kama upo tayari kwa hili basi jiunge leo na semina hii, kwa sababu ndio semina ya mwisho kwa njia ya mtandao kwa mwaka huu 2015.
Kujiunga na semina hii bonyeza haya maandishi na ujaze taarifa zako kisha lipa ada ya kushiriki semina ambayo ni tsh elfu 30. Ada tuma kwenye namba zifuatazo, tigo pesa na airtle money tuma kwenye namba 0717 396 253 mpesa tuma kwenye namba 0755 953 887. Jiunge leo kuhakikisha hukosi nafasi hii ya kipekee.
Kama hukupata taarifa za mwanzo kuhusu semina hii haya ndio yatakayofundishwa;
SEMINA; MIMI NI MSHINDI, Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu.
1. Nilizaliwa kushinda.
2. Maisha yangu ni jukumu langu.
3. Ninaamini ninaweza kushinda.
4. Ninapima ushindi wangu kwa malengo.
5. Mimi kama mshindi ni mwaminifu.
6. Nimejitoa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.
7. Muda ni mali ya thamani kwangu.
8. Nimezishinda hofu zote.
9. Kujifunza kila siku ndiyo nguzo yangu.
10. Nimeacha kutafuta sababu.
11. Wakatishaji tamaa hawaniyumbishi.
12. Ninafanya kile nilichopanga kufanya leo.
13. Kukosea ni sehemu ya ushindi wangu.
14. Ninakazana kuwa bora na sio kuwashinda wengine.
15. Ninajua hakuna njia ya mkato.
16. Kulaumu na kulalamika ni mwiko kwangu.
17. Mimi ni king’ang’anizi, sikubali kukata tamaa.
18. Ninashukuru kwa maisha haya ya ushindi.
19. Ninashirikiana na washindi wenzangu.
20. Ninachukua hatua mara moja.
Masomo haya 20 yameandaliwa vizuri sana kiasi kwamba kadiri unavyokwenda unaendelea kuvunja minyororo yote ambayo inakuzuia kufikia mafanikio. Kumbuka mabadiliko ya kweli kwenye maisha yako yanaanza na wewe mwenyewe, na ndio maana mafunzo haya yameandaliwa ili kukuwezesha wewe mwenyewe kubadilika, kujiahidi kwamba utashinda na baadae utashinda kweli.
CHETI CHA AHADI.
Ili kuongeza na kuweka msisitizo zaidi kwenye ahadi hii, baada ya mafunzo haya tutaandaa vyeti maalumu vya wewe kujiahidi mambo haya muhimu. Utaweka sahihi kwenye cheti hiko na kukiweka mahali ambapo kila siku unaweza kukiona na kujikumbusha kwamba wewe ni mshindi na ni mambo gani unafanya kama mshindi.
Yaani nakuhakikishia, kama utajiunga na mafunzo haya, na kuyafanyia kazi, na ukapata cheti hiki ambacho kitakuwa kinakukumbusha kila siku, hakuna kitu chochote, narudia tena, HAKUNA KITU CHOCHOTE kinachoweza kukuzuia wewe kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
GHARAMA ZA SEMINA HII.
Kwa yote haya mazuri upo tayari kulipia kiasi gani cha fedha?
Hakuna thamani unayoweza kuweka kwenye mafunzo haya, yana thamani kubwa sana ambayo huwezi kuitathmini kwa viwango vya fedha. Lakini kwa sababu wewe ni rafiki yangu, na lengo langu ni kukuona wewe unafanikiwa, utachangia mchango mdogo wa kuhakikisha semina hii inaweza kuendeshwa.
Na mchango huo utakuwa tsh elfu 30(30,000/=) kwa mafunzo ya semina. Kwa wale watakaotaka kupata vyeti vya kumbukumbu ya ahadi yao wataongeza gharama kidogo za kupata cheti kile, tutajuzana baadae.
Hii ni gharama ndogo sana ambayo huwezi kuipata kwa mafunzo kama haya ambayo utayapata.
KUJIUNGA NA MAFUNZO HAYA.
Ili uweze kushiriki mafunzo haya, unahitaji kujiunga kwa kujaza taarifa zako na kisha kulipia ada ya mafunzo.
Kujiunga na kulipia kumefunguliwa leo tarehe 18/09/2015 na mwisho wa kujiunga na kulipia itakuwa tarehe 02/10/2015. Baada ya hapo hutakuwa tena na nafasi ya kujiunga.
Ili kuhakikisha washiriki wanapata mafunzo bora, nafasi za ushiriki huwa zinakuwa chache. Hivyo ni vyema ukachukua hatua haraka.
Kujaza taarifa zako
bonyeza maandishi haya na malipo fanya kwa namba zifuatazo; M PESA 0755 953 887, TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717 396 253.
Chukua hatua haraka kabla nafasi hii ya kipekee haijakupita.
Nakukaribisha sana kwenye mafunzo haya ambayo ninaamini bila ya kusita kwamba yatabadili maisha yako. Nimejitoa kuweka kila ninachojua kwenye mafunzo haya ili yawe msaada mkubwa sana kwenye maisha yako, usijaribu kabisa kuyakosa.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
P.S Kama bado hujajaza fomu ya kujiunga bonyeza maandishi haya sasa na ujiunge na mafunzo haya mazuri.
N;B Kumbuka ZIMEBAKI SIKU MBILI TU kujiunga na mafunzo haya, BONYEZA HAPA kujaza fomu sasa ili usikose mafunzo haya muhimu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: