FREAKNOMICS ni kitabu kinachoelezea dhana za kiuchumi kwenye maisha ya kawaida ya mwanadamu. Ni kitabu ambacho kimeandikwa kwa misingi ya kuuliza maswali ambayo ni ya wazi na ambayo watu wamekuwa wakifikiri majibu ya wazi kumbe ni vitu havina uhusiano.
1. Kila binadamu anaendeshwa na motisha(incentive). Maamuzi unayofanya kwenye kazi au maisha yako ni yanatokana na motisha iliyopo kwenye hiko unachopata.
2. Kujua motisha unaowaendesha watu kwenye maamuzi wanayofanya, ni njia nzuri sana ya kuwez akutatua tatizo lolote. Au kujua kw anini baadhi ya mambo yanatokea vile yanavyotokea.
3. Mabadiliko yoyote makubwa yanayotokea hayatokani na kitu kimoja kikubwa kilichofanywa ghafla, bali yanatokana na sababu nyingi ambazo zinakuwa zimetokea kw amuda mrefu sana. Ndio baadae watu mnaona mabadiliko makubwa. Mfano waandishi wametumia kupungua kw auhalifu marekani mwishoni mwa miaka ya 90, sababu kubw ailikuwa kupitishwa kwa sheria ya kuruhusu kutoa mimba miaka kama 20 iliyopita. Hivyo wale watoto ambao wangezaliwa kwenye mazingira magumu na hivyo kuishia kuwa wahalifu walitolewa kwenye mimba.
4. Taarifa ni nguvu na baadhi ya watu wanatumia taarifa walizonazo kupata kipato au kunufaika zaidi. Kwa mfano dalali anapokushawishi ununue kitu, tofauti yako wewe na dalali ni kwamba dalali ana taarifa zaidi kuhusiana na kupatikana kw akile anachokushawishi ununue.
5. Unaponunua kitu ambacho kuna dalali katikati, na dalali ananufaika kwa wewe kununua, neno lolote atakalokuambia dalali ni uongo, mpaka pale utakapodhibitisha wewe mwenyewe. Mara zote kumbuka hili na utajikuta ukiepuka matatizo mengi unaponunua au kuuza kitu kupitia dalali.
6. Kuja kwa mtandao wa intaneti kumepunguza sana nguvu ya watu kutumia taarifa walizonazo kunufaika zaidi. Sasa hivi karibu kila taarifa inapatikana kwneye mtandao wa intaneti. Na kadiri siku zinavyokwenda, watu wanaweza kufanya manunuzi wenyewe wakiwa na taarifa za kutosha bila ya kutegemea mtu wa kati.
7. Linapokuja swala la uhalifu, watoto wote hawapo sawa, na wala hawakaribiani. Watoto wanaozaliwa na kukulia kwenye mazingira magumu wana nafasi kubwa sana ya kuwa wahalifu ukubwani.
8. Kuwa makini sana na unaoambiwa ni ushauri wa kitaalamu. Maana wataalamu nao ni binadamu na binadamu wote tunaongozwa na motisha(incentive). Kwa mfano kwa tafiti za dunia zinaonesha maeneo yenye madaktari bingwa wengi wa wanawake, wanawake wengi hujifungua kwa upasuaji kuliko maeneo ambayo hayana wataalamu hao. Sababu kubwa inaweza kuwa mtaalamu kaona tatizo na hiyo ni njia ya kulikwepa, ila pia upasuaji unamlipa zaidi mtaalamu kuliko njia ya kawaida.
9. Ili uweze kujifunza vyema kutokana na tafiti, unatakiw akujua vitu viwili muhimu.
Moja, jua ni nini unachotaka kupima.
Mbili, jua jinsi ya kukipima.
Majibu yote unayotaka yanatokana na vitu hivyo viwili.
10. Kuna aina tatu za motisha(incentive)
1. Motisha wa kiuchumi, hapa ni pale mtu anapofanya jambo ili kupata fedha au manufaa yoyote yale ya kiuchumi.
2. Motisha wa kijamii, kufanya mambo ili kukubalika na jamii, kufanya yale ambayo ni sahihi kwa jamii husika.
3. Motisha wa kimaadili, kufanya mambo kwa sababu ndivyo unavyopaswa kufanya.
11. Motisha wowote unaweza kuleta madhara chanya au madhara hasi. Kwa mfano shule inasisitiza wazazi kulipa ada kwa wakati, lakini wazazi wachache hawalipi. Baadae inaweka faini kwa wanaochelewa kulipa ili iwe motisha kwa wazazi kulipa kwa muda. Hii inaweza kuongeza idadi ya wale ambao hawalipi kwa sababu watajua nitatoa tu faini na mambo yataisha.
12. Kila binadamu anadanganya. Na kudanganya huwa kunaongezeka zaidi pale ambapo kutaka kupata kitu au kushinda kitu kunapokuwa kunahitajika kwa hali ya juu sana. Labda unataka sana kushinda kitu halafu unaona kunanjia ya mkato ya kufanya hivyo ambayo hupaswi kuitumia, lakini unaona ukiitumia hakuna anayeweza kujua.
13. Kinachowafanya watu kudanganya ni ile tamaa ambayo ipo ndani ya mtu ya kutaka kupata zaidi kwa juhudi au gharama kidogo. Kwenye michezo, kwenye siasa, kwenye kazi na kila eneo, unapokuwa na tamaa ya kupata zaidi kwa kutoa kidogo, unasukumwa zaidi kudanganya.
14. Taarifa ndio sarafu ya kwenye mtandao wa intaneti. Mwenye taarifa muhimu na ambazo zinahitajika na wengi ana nafasi kubwa ya kufaidika.
15. Wataalamu wanatumia taarifa ambazo wewe huna. Na ili kuonesha utaalamu wao, kitu cha kawaida watakuambia kwa lugha ngumu na wewe utaona ni vitu vikubwa sana hivyo kuwa tayari kulipia gharama kubwa.
16. Kuna mambo ambayo yamezoeleka kufanywa, halafu kuna ukweli. Mara nyingi watu hufikiri mambo ambayo yamezoeleka kufanywa ndio ukweli wenyewe. Lakini ukweli ni kwamba kuna mambo ambayo yamezoeleka kufanywa lakini ni ya uongo. Ni jukumu lako kujiuliza je kile unachofanya ndio ukweli au ni mazoea.
17. Inapokuwa watu wengi wao tayari kufanya kazi fulani, basi kazi hiyo inakuwa haina maslahi mazuri. Yaani kama kazi unayofanya kila mtu anaweza kuifanya basi huwezi kulipwa vizuri kwa sababu huna cha kuringia ili uongezwe kipato, ukiacha kuna wenzako wengi wapo tayari kufanya. Hii ni dhana kubwa inayotumika kwenye ubepari, kuhakikisha kazi kubwa inagawanyw akwenye vipande ambavyo kila mtu anaweza kufanya.
18. Kazi nyingi ni kama mashindano ya ligi, wanaanza watu wengi na wanaanzia chini kabisa, lakini mshindi atakuwa mmoja tu. Na mshindi anapata faida kubwa kuliko wengine. Hivi ndivyo ilivyo kwenye kazi za mashirika, muziki, uigizaji na kadhalika. Vijana wengi wanaingia kwneye kazi hizo wakiangalia wachache waliopo kileleni, bila ya kujua kuna wengi wanakazana na kuishia njiani.
19. Kama unaingia kwneye biashara ambayo mnashindana na kugombana na wengine muda wote, unapoteza muda wako bure. Unapokuwa kwenye hali ya mashindano unakosa muda w akufuatilia biashara na hivyo unasihia kupata hasara.
20. Uhalifu mkubwa hautokei ghafla. Bali huanza na uhalifu kidogo ambao unapuuzwa. Kwa mfano mtoto akivunja dirisha moja na hakuchukuliw ahatua ataona kwmaba kuvunja madirisha sio tatizo, hivyo siku nyingine atavunja zaidi. Ni vyema kuadhibu makosa madogo madogo maana haya ndio yanamjengea mtu ujasiri wa kufanya makosa makubwa.