Imebaki Siku Moja Ya Wewe Kuweza Kuufanya Mwaka 2016 Kuwa Mwaka Bora Sana Kwako. Chukua Hatua Leo.

Mwaka mpya mambo mapya….
Hii ni kauli ambayo utaisikia kwa wengi na wewe mwenyewe pia utaitoa sana kwa siku hizi za mwanzo wa mwaka. Kauli hii pia itaandamana na maazimio mengi kwa mwaka huu 2016.

 
Lakini unajua ni kitu gani kitatokea baada ya mwezi mmoja kuisha?
Utakuwa umeshasahau maazimio uliyoweka, utakuwa umesharudi kwenye maisha yale yale ambayo umezoea kuishi miaka ya nyuma na hakuna mabadiliko makubwa utakayoweza kuyaona kwenye maisha yako.
Halafu kitapita kipindi cha ukimya, kama miezi kumi hivi, ukiendelea kufanya kwa mazoea, ukiendelea kuteseka na maisha ambayo huyafurahii, mpaka inapofika novemba 2016, hapa sasa unaanza kupata matumaini mengine mapya. Unajiambia mwaka huu haukuenda vizuri sana kwangu, ila ngoja uishe, hio utakaoanza, nitahakikisha nabadilika kabisa. 2017 itaanza tena na utarudia huo mzunguko, si ndio umekuwa unafanya hivyo miaka mingi iliyopita?
Sasa hapa kuna swali moja la msingi, je unataka kuendelea na mzunguko huo ambao hauzalishi chochote kwako? Yaani ni mzunguko sawa na mbwa anayekimbiza mkia wake, atachoka sana lakini hataweza kuukamata.
Kama jibu ni ndio umeridhika na mzunguko huo na unataka kuendelea nao basi nikutakie kila la kheri na unaweza kuishia hapa kwa leo.
Kama jibu ni hapana, hutaki tena kuendelea na mzunguko huo, umechoka na maisha hayo ambayo huyapendi, basi karibu sana kwani kuna njia bora ya wewe kuweza kuondokana na mzunguko huo unaokupotezea muda.
Njia ya uhakika ya kuwa na mwaka bora 2016.
Karibu kwenye njia ya uhakika ya kuhakikisha mwaka 2016 unakuwa mwaka bora sana kwako. Kupitia njia hii utaepuka makosa yote ambayo umekuwa unafanya kila mwaka na yanakuzuia kufikia mafanikio unayotarajia.
Njia hii ni kupitia semina ya 2016 NI MWAKA WANGU WA UBORA WA HALI YA JUU. Hii ni semina ambayo itakupatia mafunzo na maarifa ya kuweza kuweka malengo makubwa na ambayo lazima utayafikia.
Kupitia semina hii utaweka malengo ambayo ni muhimu kwako, utayachambua vizuri kuhakikisha unayajua nje ndani na utajiandaa kwa changamoto zozote zinazoweza kujitokeza.
Kupitia semina hii pia utayajua na kuweka malengo matano muhimu sana kwenye maisha yako ili uweze kuwa na maisha bora, unayoyafurahia na yenye mafanikio.
Semina hii inatolewa kwa njia ya mtandao, kupitia email na wasap. Hivyo unaweza kushiriki semina hii popote pale ulipo duniani. Huhitaji kuondoka na kwenda sehemu nyingine, bali unahitaji kutenga muda wako wa siku, hasa asubuhi kufuatilia mafunzo na kufanyia kazi hatua hizi za kuweka malengo bora sana kwako.
Ada ya kushiriki semina hii ni tsh elfu 20 (20,000/=) na ili uweze kupata nafasi ya kushiriki semina hii tuma ada hiyo kwenye namba zifuatazo. Mpesa 0755 953 887 na tigo pesa au airtel money tumia 0717 396 253.
Ukishatuma ada hiyo ya semina, fungua maandishi haya na jaza fomu kwa kuweka taarifa zako. Pia unaweza kutuma ujumbe kwenye moja ya namba hizo kueleza kwamba umelipia ada ya semina ukiambatanisha majina na email yako.
Chukua hatua leo za kujiunga na semina hii muhimu sana ambayo hutakuja kuisahau kwenye maisha yako. mwisho wa kujiunga ni kesho tarehe 02/01/2016 na semina itaanza rasmi tarehe 04/01/2016 na itaendeshwa kwa siku kumi, masomo yatatolewa kila siku.
Hakikisha hukosi nafasi hii ya kipekee sana ya kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi. Shiriki semina hii na uufanye mwaka 2016 kuwa mwaka bora sana kwako.
Lipa ada na ujaze fomu leo, kabla nafasi hazijajaa au muda kuisha.
Nakukaribisha sana kwenye semina hii kubwa na ya kipekee.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani.
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

One thought on “Imebaki Siku Moja Ya Wewe Kuweza Kuufanya Mwaka 2016 Kuwa Mwaka Bora Sana Kwako. Chukua Hatua Leo.

Add yours

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: