Karibu kwenye kipengele hiki ambapo tunakumbushana mambo muhimu kuhusu maendeleo na mafanikio ya biashara zetu.
Leo tutagusia na kukumbushana eneo hili muhimu sana la biashara yako ambalo ni wateja.
Na kuna kitu kimoja muhimu sana unatakiwa kukumbuka mara zote, ya kwamba mteja yupo sahihi mara zote.
Inapotokea hali yoyote ya kutokuelewana kati yako wewe na mteja wako, basi jua ya kwamba mteja yupo sahihi. Hata kama una uhakika kabisa ya kwamba makosa ya mteja ndiyo yamepelekea hali hiyo, bado yeye anabaki kuwa sahihi.
Kwa nini mteja yupo sahihi mara zote?
Kwa sababu mteja ana nafasi kubwa ya kuchagua, na anaweza kuamua kununua kwako au kununua kwa mfanyabiashara mwingine kama wewe ambao wapo wengi sana.
Na kwa kuwa biashara za sasa karibu kila mtu anafanya, basi unahitaji kuwa makini sana na mahusiano yako na wateja wako.
Inapotokea hali yoyote ya kutokuelewana baina yako na mteja wako, badala ya kutaka kubishana, au kumwonesha amekosea, tafuta kujua ni kipi hasa kinaendelea kisha pendekeza suluhisho ambalo litakuwa bora kwenu wote, mteja apate kile anachotaka na wewe uuze kile unachouza.
Ukitaka kubishana na mteja, kumwonesha kwamba yeye ndiye mwenye makosa, mara zote yeye ndiye atakayeshinda. Kwa sababu hata kama utamshinda kwa kumwonesha amekosea, atakachofanya ni kutokuja tena kwenye biashara yako. na kwa dunia hii ya utandawazi, ana nafasi ya kuwaambia wengine pia nao wasije kwenye biashara yako.
Hivyo jua mteja mara zote yupo sahihi, na hujui hili ili kukubali akunyanyase, bali ujue ni jinsi gani ya kuboresha mahusiano yako na wateja wako na mwisho wa siku wote mfaidike.
Kila la kheri kwenye ukuaji wa biashara yako.
Kwa lolote ambalo ungependa tuliandikie hapa kwa ufupi weka kwenye maoni hapo chini.
TUPO PAMOJA.
asante coach kwa makala kuhusu MARA ZOTE MTEJA YUKO SAHIHI.mimi nina biashara ya MPESA sasa baadhi ya wateja wanataka uwasaidie kutoa pesa kwenye simu zao kwa kuwa hawafahamu kutoa wao wenyewe.baadhi tunawaelekeza na wanaelewa then wanatoa wenyewe.lakini wengine hawaelewi kabisa,hivyo unashindwa kumuhudumia kwa kuwa sheria hairuhusu kushika simu ya mteja na kutoa hela badala yake.sasa wateja wasioelewa wanakasirika sana na kuona kama uwatendei haki!!sasa hapa ni mimi au mteja yupo sahihi?
LikeLike
Karibu Elizabeth,
Kwa changamoto hii, ni vyema kuendelea kuwaelewesha wateja jinsi ya kufanya wao wenyewe.
Na waambie kabisa ya kwmaba utaratibu ndio unakutaka hivyo. Na pia nenda mbali zaidi kuwamabia sio vigumu na pia ni kwa usalama wao wenyewe. Mwambie kama akiend akw amtu ambaye siyo mwaminifu anaweza kuibiwa, hivyo ni bora akubali umwelekeze na siku nyingine ataweza kufanya mwenyewe bila ya maelekezo.
Tatizo kubwa ni kwamba watu huwa wanapend akutafuta njia rahisi na ya mkato, lakini ukiwaelewesha vyema na kuwaonesha ni jinsi gani hilo linakuwa na faida kwao, wataelewa na kufurahia.
Kila la kheri.
LikeLike
Ahsante coach. nikweli mteja yupo sahihi mm Nina changamoto iliyonikuta. kuna mteja nilimhudumia vizuri tu akaondoka na bidhaa kisha kukaa nayo siku kama tatu hivi. ya NNE anarudi na bidhaa anasema nimempa mbovu hivyo nimbadilishie. hapo mm binafsi nilishindwa kufanya hivyo ikabidi aondoke nayo hivyo hivyo japo hakulidhika. sasa katika mazingira hayo usahihi Wa mteja hupo kweli?
LikeLike
Habari Selemani,
Hiyo ni changamoto kubwa, na hapo ndipo unapohitaji kutumia busara zako kufanya mamauzi sahihi.
Kwanza unaweza kuangalia uhalali wa madai ya mteja, je ni kweli ilikuwa mbovu, je wakati anachukua hamkuangalia kama ni nzima au sio nzima. Kama mliangalia na wote mkaridhika basi huenda ameharibu yeye. Ila kama hamkuangalia hapo na wewe umechangia.
Kufanya maamuzi sahihi unaweza kuangalia gharama utakayoingia wewe kama utaamua kumpa nyingine, kama siyo kubwa sana unaweza kufanya hivyo, kama ni kubwa unaweza kumwambia utampa kwa bei nusu.
Kwa vyovyote vile fanya mazungumzo na mteja huyo sio kwa hali ya kujitetea kwamba kosa ni lake, bali kwa hali ya kuangalia tunatatuaje hili, na nina hakika mtaishia vizuri sana na kila mtu ataridhika na atakuw amteja wa kudumu kwako.
Ukikazana kufanya yeye aonekane ndio ana makosa, hata kama ni kweli, bado inaweza isiwe na msaada mkubwa kwako. Hujui ni wangapi atakaoenda kuwaambia kuhusiana na hali hiyo. Na mbaya zaidi ataenda kuwaambia uongo, unaomfanya yeye asionekane mwenye kosa.
Haya ni maamuzi unayohitaji kufanya kw akufikiri kwa kina, yanaweza kukugharimu kiasi fulani, ila yataimarisha sana biashara yako.
Kila la kheri.
LikeLike