Njia Tatu (3) Za Kukuza Biashara Ili Kupata Faida Kubwa.

Uhali gani mpenzi msomaji wa makala hii ya AMKA MTANZANIA? Ni matumani yangu umzima wa afya tele na pia kama haupo vizuri kiafya basi usijali kwa uweza wa mwenyezi  Mungu utapona na kuendeleza kulisukuma gurudumu hili la mafanikio. Karibu sana katika siku ya leo kujifunza.
Katika somo letu la leo kama linavyoeleza hapo juu tutaangalia ni hatua gani ambazo endapo utazifanya zinaweza kukusaidia kukuza biashara yako ambayo unaifanya au una mpango wa kuifanya. Matumaini yetu makubwa katika kufanya biashara ni kuona tunapata faida kubwa.
Lakini matumini hayo hugeuka ghafla na kujikuta tunaacha kufanya biashara hii, mara na kuanza biashara nyinyine huku tukiamini kufanya hivi ni kuzikwepa changamoto. Ndugu msomaji  naomba nieleweke vizuri hapa ,sina maana ya kwamba kufanya biashara nyingine na kuiacha biashara  ya mwanzo ni kosa la hasha sio kosa  ila tatizo ni kuhama na mtazamo uleule wa biashara ya mwanzo  kuutumia kwenye biashara mpya na kujikuta huupati faida kama ulivyokuwa ukitarajia hapo awali.
Kuna biashara hasa hizi ndogondogo huwa tunaziona zipo vilevile siku zote. Huenda ukawa ni wewe mhusika wa biashara hiyo au kuna mtu na jamaa,ndugu au rafiki ambaye huwa unamuona akiwa katika hali hiyo,nitakachokieleza katika makala hii utaweza kumshirikisha pia mwingine ili kiweze kumsaidia.
Zifutazo ndizo hatua (3) za kukuza biashara ili kupata faida kubwa;
1.Panga malengo na mipango ya biashara.
Hili ni jambo la msingi kuweza kulizingatia. Kama wewe ni mfanyabiashara au unataka kuwa mfanyabiashara unaweza ukapanga malengo na mipango ya kuweza kuiendesha biashara yako ili kuweza kupata faida kubwa zaidi. Malengo na mikakati yako lazima uyaandiike vizuri na uyatekeleze pia.Unaweza ukapanga malengo na mipango ya mauzo katika mwaka kwa mfano  unaweza kupanga kwa mieze mitatu mitatu.
Kwa mfano unafanya biashara fulani lazima upange labda kila baada ya miezi mitatu uuze milioni tatu au zaidi na kama juu ya mpango na malengo usipokamilika unaweza ukafanya tathimini ni wapi ulipokesea? ili urekebishe ili miezi ijayo uweze kufikia malengo yako. Pia unaweza ukafanya taathimini  kama utakuwa umewajiri watu katika biashara yako kwa kujiuliza je wana mchango wowote katika kukuza biashara? Au wao ndio sababu ya wewe kushindwa?
Pia katika kupanga malendo na mipango juu ya biashara yako lazima upange juu ya muda wa kufanya biashara.Katika hili lazima ujiulize je biashara yako ni ya msimu? Kwa mfano wewe ni unafanya biashara ya kuuza makoti lazima ujue ni misimu ipi ni ya baridi kwani uhitaji wa wateja juu ya bidhaa hii ndio huwa wengi zaidi.Vilevile lazima upange ni jinsi gani utakavyochangamana na wateja ili kuweka mahusiano ya karibu na wateja wako.
TAFUTA NAMNA YA KUKUZA WATEJA WAKO.
2.Tazama ni wapi unakosea na kufanya marekebisho.
Mara nyingi changamoto katika biashara yeyote ile lazima zijitokeze.Hakuna binadamu ambaye amekamilika kokosea ni shemu ya mafanikio ya kibiashara hivyo usiogope pindi changamoto zinapojitokeza na pindi tunapokosea ndipo tunapojifunza zaidi. Inawezekana biashara yako haileti faida kutoka na wafanyakazi wako na vitu vingine jaribu kufanya uchunguzi wa kina na kuvirekebisha.
Ewe mpenzi msomaji wa makala hii ili kukuza biashara ni lazima ufanye tathimini ni mipango ipi inakuletea faida katika biashara? kwani hiyo ndiyo njia sahihi ya kuuzingatia. Kwani sio kila mipango unayopanga huleta faida.
3.Tambua namna ya kuongeza wateja.
Hii ni hatua nyingine pia ya kuzingatia. Inawezekana wewe ni mfanyabiashara mdogo au mkubwa au unatamani kuwa miongoni mwa wafanyabiashara tambua ya kwamba kuna baadhi ya biadhaa mteja akizinunua anaweza kukaa muda mrefu bila kununua tena mfano wa biashara hiyo ni magari,samani na vitu vingine. Katika hili jaribu kujenga mahusiano mazuri na wateja pia jaribu kuwa na kumbukumbu nzuri na wateja ili watakapokuja siku nyingine uweze kuwakumbuka.
Unaweza ukawa unawatumia wateja wako juu ya ujio mpya wa bidhaa, mabadiliko ya bei ili wakija kununua bidhaa wasishangae pia unaweza kuwaambia asante kuwa miongoni mwa wateja wako wazuri kwa kufanya hivi ni njia nzuri ya kuongeza wateja. Hivo kama utafanya hivi wateja hao hao ndio watakao kufanya upate wateja wapya kutokana na ukarimu na nidhamu uliyo nayo juu yao.
Pia unaweza kuongeza wateja kwa kutaangaza bidhaa yako kupitia njia mbali kama vile vyombo vya habari na mitandao mingine ya kijamii njia hii pia itafanya uongeze wateja pia. Fahamu ya kwamba kumpata mteja mpya ni kazi katika biashara yako ni ngumu hivyo hakikisha mteja/wateja ulionao hauwapotezi.
AMKA MTANZANIA inakutakia kila la kheri katika safari yako yako ya kuelekea kwenye mafanikio katika biashara yako.
Makala hii imeandaliwa na Afisa mipango na mendeleo; Mr. Benson o. Chonya, unaweza kuwasiliana naye kwa +255 (0) 757 909 952.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: