Huu ndiyo ule wakati wa kudanganyana na kujidanganya wewe mwenyewe. Tumekuwa tunaona sinema hii kila mwisho wa mwaka na mwanzo wa mwaka. Ambapo watu wanaanza kukumbushana malengo ya mwaka unaoisha na kuhamasishana kuweka malengo ya mwaka unaoanza. Nasema ni wakati wa kudanganyana kwa sababu mpaka mwezi wa kwanza unaisha, asilimia 90 ya watu hawakumbuki tena malengo waliyojiwekea kwenye mwaka huo. Wanakuwa wamerudi kwenye maisha yao waliyozoea na mambo yanakwenda kwa mazoea.
Ndiyo maana mimi nimekuambua wewe rafiki yangu, mwaka huu mpya 2017 usiweke malengo. 

Yaani ukijaribu tu kuweka malengo, basi umejipoteza na mwaka huu mzuri unaokuja umeamua kuupoteza. Zipo sababu nyingi kwa nini nakwambia usiweke malengo, na ipo njia bora zaidi ya kufanikiwa bila ya kutumia malengo. Yote haya tutajifunza na kujadili kwa kina kwenye semina ya mwaka 2017 itakayoendeshwa kwa njia ya mtandao wa wasap kuanzia tarehe 04/01/2017. Ili kushiriki semina hii unatakiwa kulipia ada ya mwaka ya KISIMA CHA MAARIFA ambayo ni tsh 50,000/= na utashiriki semina hii, semina nyingine moja na kila siku utapata mafunzo na hamasa. Kwa maelezo zaidi kuhusu semina hii bonyeza maandishi haya.

Sasa kuna wengi ambao ni wageni wa maisha ya mafanikio, ambao hawajawahi kuyaendesha maisha yao kwenye misingi ya mafanikio. Hivyo hawawezi kuelewa baadhi ya mambo ambayo tunayajadili tunapochagua mwaka kuwa wa mafanikio.

SOMA; PROSPERITY ON PURPOSE (Mwongozo wa kuishi maisha ya mafanikio makubwa).

Pia wapo wengine wengi ambao hawatashiriki semina hii ya kipekee kwa mwaka 2017. Kwa sababu mbalimbali watakosa maarifa haya yatakayokwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yetu kwa mwaka 2017.

Kwa kuwa wasomaji wote ni marafiki yangu, sipendi kuwaacha hivi hivi. Napenda kuwashirikisha mambo matatu tu ambayo unahitaji kwenda kufanya kwa mwaka 2017 ili uwe mwaka wa mafanikio kwako. Najua yapo mengi sana unaweza kuwa unapanga sasa, labda kujenga, kununua gari, kuoa au kuolewa na mengine mengi.

Lakini mimi rafiki yako nakuambia, kama bado hujaweza kuyasimamia maisha yako vizuri, tupa hayo yote mbali na fanya mambo haya matatu tu. Yaani mwaka mzima 2017 jipime kwenye mambo haya matatu.

Moja; anzisha au kuza biashara yako.

Kama mpaka sasa huna biashara, unajidhulumu, unajinyima na hujitendei haki. Tunaishi kwenye dunia inayoenda kasi sana, ambapo chochote mtu anachotegemea kama njia ya kipato, kama hukidhibiti mwenyewe unajiweka kwenye hatari. Tunaona namna ambavyo wahitimu ni wengi kuliko uwezo wa serikali na taasisi kuajiri. Tunaona namna ambavyo ajira zinazidi kubanwa na kubanwa na kubanwa, kipato kidogo kazi nyingi.

SOMA; Kama Unafikiri Mafanikio Yako Hivi Tu, Tayari Umeshapotea.

Hivyo kama huna biashara, lazima mwaka 2017 uanzishe biashara. Ndiyo umenisikia vizuri nimekuambia ni lazima kwa sababu si wewe mwenyewe umechagua kuishi maisha ya mafanikio? 

Kama hutaki basi achana na haya ya kufikiria maisha ya mafanikio. Lakini kama unayataka mafanikio, huna namna, anzisha biashara.

Kama tayari una biashara hongera sana, upo kwenye njia sahihi ya kushika hatamu ya maisha yako. Sasa ikuze biashara yako, mwaka 2017 wafikie wateja wengi zaidi, toa huduma bora zaidi na fungua masoko mapya zaidi. Angalia namna unavyoweza kuikuza biashara yako zaidi mwaka 2017.

Mbili; anza kuwekeza.

Kama nilivyosema kwenye biashara, unahitaji kuwekeza, kama mpaka sasa huwekezi, unafikiria nini wakati ukiwa na miaka 70, 80 na hata 90? Unafikiri utaweza kuendelea kufanya kazi au biashara unayofanya sasa mpaka ukiwa na miaka 70, au 80? Kama unafikiri sawasawa najua unajua ni kitu hakiwezekani. Sasa hebu niambie unafikiri utakuwa unaishije wakati huo kama ukiwa hai? Tafadhali usijidanganye kwamba watoto wako watakuangalia, kwa sababu labda umewasomesha na mengine kama hayo. Huna mkataba na mtu yeyote kwamba atakuwa anakuangalia ukiwa mzee. Na pia huna uhakika kama nao watakuwa wameweza kuyasimamisha maisha yao vizuri.

Hivyo jambo la busara kufanya, kama unayafikiria maisha ya mafanikio, ni kuanza kuwekeza sasa. Ndiyo anza kuwekeza sasa. Usiniambie kipato chako ni kidogo ndiyo maana huwekezi. 

Anza kuweka akiba ya shilingi elfu moja, weka kila siku na ikishafika kiasi fulani unachoweza kuwekeza, wekeza. Unaweza kuwekeza kwenye hisa, vipande, ardhi, biashara na mengine mengi. Anza kuweka akiba kwa ajili ya uwekezaji, na kama utahitaji elimu ya ziada juu ya uwekezaji, rafiki yako nipo, karibu tushauriane. Lakini usije kwangu sasa ukiwa na mawazo, utapoteza muda wako na wangu pia, kwa sasa weka akiba maalumu ya uwekezaji, halafu ikishafika kiasi fulani, labda kwa kuanzia kabisa laki moja, na hujui uwekeze wapi, hapo unaweza kuja kwangu na tukazungumza.

Anza kuwekeza, kadiri unavyoanza mapema ndivyo unavyotengeneza uhuru wa maisha yako.

Tatu. Jifunze kila siku. Soma. Sikiliza na tafakari.

Kama ulishangilia sana siku uliyohitimu masomo, ukiamini kwamba umemalizana na habari za kusoma, nikupe pole. Ule ulikuwa ni mwanzo tu, kitu kinachoitwa kusoma na kujifunza, ni kitu kinachopaswa kufanywa kila siku. naomba nirudie kwa herufi kubwa KILA SIKU. Na hivyo mwaka 2017 hiki ni kitu unachokwenda kufanya kila siku. isipite siku hujasoma kitabu na hujajifunza kitu kipya kuhusiana na biashara unayokwenda kuanzisha mwaka 2017. Chagua mitandao utakayokuwa unaisoma kila siku, AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA iwe ya kwanza kwa sababu mwaka 2017 nitahakikisha unapiga hatua kubwa sana, kupitia maarifa nitakayokuwa nakushirikisha.

Njia moja ya kukuwezesha kufanya yote haya.

Ipo njia moja ya kukuhakikishia wewe kuweza kufanya mambo haya matatu.

Kwa njia hii utapata biashara unayoweza kuanza kufanya, hata kama bado upo kwenye ajira.

Utajifunza kuhusu uwekezaji unaoweza kufanya, zipo aina nane za uwekezaji, mifereji nane ya kipato unayopaswa kuwa nayo.

Na pia utakuwa umejifunza mengi kuhusu usimamizi na uendeshaji bora wa biashara yako. 

Kuanzia matumizi ya muda, kuajiri na hata kushirikiana na wengine kwenye biashara.

Njia hiyo ni kusoma kitabu nilichoandika, kinaitwa BIASHARA NDANI YA AJIRA, Jinsi ya kuanzisha na kukuza biashara yako. Kitabu kinauzwa tsh 10,000/= na kama upo mkoani unatumiwa popote ulipo kwa kulipia tsh 15,000/=

Kitabu kinapatikana kwa mawakala wafuatao;
Mwanza; 0719756365
Mtwara 0784503076
Kyela 0759051543
Zanzibar 0714312924
Songea 0782744713
Njombe 0769761297
Mbeya 0756473764
Morogoro 0755848391.

Dar na mikoa mingine isiyo na wakala 0654426721.
Piga simu sasa kwa wakala aliye karibu au kwa wakala wa dar kama mkoa wako hauna wakala ili uweze kupata kitabu hiki.

Kumbuka; mwaka 2017 hakuna kuweka malengo. Karibu kwenye semina yetu ya mwaka 2017 au fanya hayo matatu niliyokushauri hapo juu.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.