Habari mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Amka Mtanzania? Ni matumaini yangu kuwa hujambo na unaendelea vizuri.  Karibu sana rafiki tuweze kujifunza wote kwa pamoja kwani leo ni siku bora na ya kipekee sana kwenye maisha yetu. Leo ndiyo siku ya ushindi kwenye maisha yako hivyo tumia vizuri muda wako ili kukamilisha ushindi unaotaka.

 

Changamoto kubwa inayowaumiza watu wengi kushindwa kufurahia maisha ni maumivu ya nafasi. Kwa kweli watu wengi wamejeruhiwa, nafsi nyingi zimeumizwa, nafsi nyingi zina majeraha ya moyo, nafsi nyingi zina maumivu, nafsi nyingi zimebeba mizigo. Changamoto nyingine inayowatawala watu katika jamii yetu ni wivu na chuki inayopelekea watu kuishi maisha ambayo hayana maana wala thamani hapa duniani.

Familia nyingi si salama, ndoa nyingi, si salama, mahusiano mengi si salama hii ni kuanzia mahusiano ya kiujirani, ndugu, jamaa na hata marafiki na nk. Baada ya kuona na kufanya tafiti katika jamii nikagundua kuwa nafsi nyingi za watu zinasumbuliwa na majeraha mbalimbali ya moyo, maumivu ya ndani, wivu, chuki na uchungu uliombika ndani ya moyo. Hivyo basi, kwa kuwa nafsi nyingi za watu zina matatizo hivyo nikaona ni vema na haki kuandaa kitabu kitakachokwenda kutibu nafsi za watu wengi.

Huu ni wakati wa kutua mizigo yetu tuliyonayo moyoni, ni wakati wa kutua mitungi tuliyobeba moyoni na kuishi maisha huru yenye furaha na amani. Tunaishi na jamii ya watu wenyewe visirani, wivu, kulalamika na kulaumu kwa hiyo, kama utakua hujajua jinsi ya kuishi na watu hawa kwenye maisha yako hakika utapata taabu. Kuna watu tabia zao ni kupenda kuona mwingine anapata shida hiyo yeye ndiyo furaha yake. Matatizo ni ya nafsi ni mengi yanayowakabili watu na wanatembea nayo na kuyajaza moyoni huku uchungu ukiendelea kuwa tafuna.

SOMA; Mambo Mawili (2) Ya Msingi Ya Kuzingatia Katika Msamaha Wa Kweli.

Ndugu msomaji, ndipo niliposukumwa kuandika kitabu cha kwa nini msamaha kwa msaada wa 
Mungu na hatimaye kukikamilisha kuandika kitabu hiki. Kitabu cha KWANINI MSAMAHA yaani WHY FORGIVENESS ni kitabu maalumu kwa ajili ya kila mtu aliye na majeraha ya nafsi  au maumivu ya moyo na kushindwa kufurahia maisha.  Hivyo kitabu hiki kina kwenda kutibu mioyo ya watu iliyokuwa imekufa na kuwa hai kupitia msamaha wa kweli kila mtu atakwenda kupata uponyaji wa nafsi kupitia msamaha wa kweli.

Rafiki, tunaalikwa kusamehe saba mara sabini hii ina maana kwamba kama wewe ni binadamu basi, unaalikwa kusamehe kila siku ya maisha yako. Bila msamaha basi maisha ya binadamu yatazidi kuwa machungu  na nafsi nyingi  zitaendelea kuteseka lakini mwenyezi Mungu ambaye yeye ndiye mwasisi wa msamaha anatualika kuweza kusameheana kila siku ili nasi tuweze kusamehewa. Tunaalikwa kusamehe ili maisha yaende, ili mambo mengine yaende na tusamehe kwa faida yetu sisi wenyewe. Kupitia msamaha wa kweli utakwenda kurudisha uhusiano wako wa awali ambao ulikuwa umevunjika.

SOMA; Hivi Ndivyo Utakoweza Kuishi Na Mtu Wa Aina Yoyote Ile Kwa Furaha Na Amani – 2

Kwa hiyo, kwa nini kitabu hiki cha KWANINI MSAMAHA? Kupitia kitabu hiki cha kwa nini msamaha kina sura kumi na saba ambapo kila sura kuanzia sura ya kwanza mpaka ya mwisho kinakupa mafundisho muhimu juu ya msamaha.  Kwa mfano, sura ya kwanza utajifunza yafuatayo;

  • Msamaha ni nini
  • Sura ya pili, utajifunza aina za msamaha
  • Sura ya tatu utajifunza mambo mawili muhimu ya kuzingatia katika msamaha wa kweli
  • Sura ya nne utajifunza kwa nini Kusamehe siyo kuvumilia au kusahau?
  • Sura ya kumi na mbili utajifunza chanzo kikuu cha maumivu ya ndani tunayopitia kwenye maisha yetu.
  • Kumi na tatu utajifunza chanzo kikuu cha wivu, matokeo yake na jinsi ya kuepuka.


Hizi ni baadhi tu ya sura ambazo nimekushirikisha vionjo vyake hapa na utakapojipatia nakala yako utajifunza yote muhimu kupitia kitabu hiki cha kwa nini msamaha.
Jinsi ya kukipata kitabu hiki;

Kitabu hiki cha Kwanini Msamaha  kimeandikwa kwa lugha nzuri na rahisi ya Kiswahili, hivyo basi kitakuwa kinapatikana kwa mfumo wa nakala tete yaani soft copy na baadaye kitapatikana katika mfumo wa hard copy. Kitabu hiki kitakufikia popote pale ulipo duniani na utaweza kukisoma kitabu hiki kupitia simu yako ya mkononi, tablet na hata kompyuta.

Kitabu hiki kitapatikana kwa bei ya shilingi elfu tano, na utatumiwa kwa njia ya barua pepe yaani email yako, kama huna email hakikisha una email, au kwa njia ya wasapu na telegram utaweza kutumiwa kitabu hiki na kukufikia hapo ulipo.

Ndugu msomaji, kuhakikisha hukosi nakala yako ya kitabu hiki cha kwa nini msamaha unaalikwa kutuma pesa ya shilingi elfu tano (5000) kwa njia ya mpesa 0767101504, na tigo pesa au airtel money 0717101505. Baada ya kutuma malipo hakikisha unatuma ujumbe  kwenye namba uliyotuma pesa na email yako na jina la kitabu na utatumiwa mara baada ya kutuma pesa yako. 

Majina yatatokea DEOGRATIUS KESSY unapotuma pesa kupitia simu yako.

MUHIMU; pata kitabu hiki kwa bei ya ofa kabla ya mwezi huu kuisha baada ya hapo bei itabadilika hivyo wahi mapema ujipatie nakala yako kwa bei ya ofa ya shilingi elfu tano tu, hakika hutojutia thamani ya maarifa utakayoyapata kwani ni zaidi ya shilingi elfu tano.

Mwisho, karibu sana rafiki tuweze kutanua wigo wa maarifa kwani hakuna  mtu maskini duniani bali kuna akili maskini na akili maskini ndiyo chanzo cha matatizo mengi kwenye maisha yetu. 

Nakutakia kila la heri rafiki yangu na kumbuka unaponunua kitabu unachangia kazi za mwandishi na gharama za kuendeshea mtandao ili uendelee kupata mafunzo mbalimbali kama unayoendelea kupata kupitia mtandao huu.

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com, kessydeo@mtaalamu.net au unaweza kutembelea tovuti yake, www.mtaalamu.net/kessydeo ,www.actualizeyourdream.blogspot.com kujifunza kila siku. Asante sana.