Maswali Na Majibu Yenye Ufafanuzi Wa Kina Kuhusu Semina Ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA.

Habari za leo rafiki?

Kama ambavyo nimekuwa nakupa taarifa kwa muda sasa, wiki ijayo yaani tarehe 03/07/2017 tutaanza semina yetu ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA. Hii ni semina muhimu kwa kila mtu ambaye anataka kujijengea msingi wa kifedha, kuondoka kwenye umasikini na kufikia utajiri. Mwisho wa kujiunga na semina hii ni kesho tarehe 30/06/2017. Hivyo kama mpaka sasa hujajiunga, umebakiwa na siku moja tu. Maelezo ya kujiunga yapo chini mwa makala hii, lakini kama hutafika chini basi tuwasiliane moja kwa moja kwa simu 0717396253.Kwenye makala hii ya leo ninakwenda kujibu baadhi ya maswali ambayo wengi wamekuwa wananiuliza kuhusu semina hii. Na nitakupa ufafanuzi wa kutosha ili uweze kuchukua hatua sahihi, usije ukakosa semina hii na ukajutia baadaye.

Swali; napenda sana kushiriki semina hii, ila hali yangu siyo nzuri kifedha, siwezi kulipia ada.

Jibu; Pole sana kwa changamoto hiyo ya kukosa fedha, ni hali ngumu kwa kweli. Lakini pia nikupe habari njema ambazo zitakuwezesha wewe kuondokana na hali hiyo. Angalia rafiki, upo hapo ulipo kifedha, kwa sababu hujapata msingi muhimu wa kifedha. Hujapata elimu ya fedha hasa, ambayo itakuwezesha wewe kuizuia hata elfu moja inayopita kwenye mikono yako iweze kukuzalishia. Kama ungeipata elimu hii mapema, leo usingekuwa na sababu hii.

Hivyo kukosa kwako fedha ya kujiunga, ndiyo sababu namba moja kwa nini unapaswa kujiunga. Hivyo pambana uwezavyo kwa siku hii moja iliyobaki, upate elfu 50 ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA ili ushiriki semina. Ikiwezekana omba kwa watu wa karibu kwako, au uza kitu ambacho hujatumia kwa mwaka mzima, ili usikose semina hii bora sana kwako.

Au unaweza usishiriki na ukaendelea na hali yako ya kifedha uliyonayo sasa. Uzuri wa maisha ni tunapata kile tunachochagua, hivyo rafiki yangu, chagua kwa umakini sana.

Swali; nipo eneo ambalo halina mtandao na hivyo nitayakosa masomo.

Jibu; semina hii inaendeshwa kwa njia ya mtandao kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA. Unachopaswa kufanya ili usiyakose masomo haya ni kuhakikisha umejiunga mpaka kufikia kesho, kwa kulipa ada, halafu ukishawekwa kwenye kundi usijitoe. Kwa njia hiyo siku yoyote utakayopata mtandao, utaweza kupokea masomo yote na kufuatilia. Pia nitakupa nafasi ya kuuliza maswali yako wakati unapokuwa na mtandao.

Kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA tupo na watu wengi ambao wanafanya kazi maalumu vijijini sana, ambao mwisho wa wiki pekee ndiyo wanapata mtandao. 

Wanatumia nafasi hiyo kupakua masomo yote na wakirudi kijijini wanayapitia wiki nzima, na kuyafanyia kazi. Maswali yao wanayaandaa na wanapofika tena kwenye intaneti wanayatuma.

Hivyo usihofu hata kama utakuwa mbali kiasi gani, mimi nitahakikisha unapata masomo haya na kupata thamani yote kwa uhakika.

Swali; kwa nini usiandae kitabu na kutuuzia wale ambao hatuwezi kushiriki semina?

Jibu; kitabu nitaandaa, lakini itachukua muda, labda kitatoka mwaka kesho, kwa sababu kwa sasa kuna vitabu kama vitatu vipo njiani vinakuja, na nitakuwa na semina nyingine baadaye mwaka huu.

Lakini muhimu zaidi ni hili, kitabu hakitakuwa na thamani kubwa kama hii ya semina, kwa sababu huenda utajifunza yale yale, lakini kwenye semina unayafuatilia hatua kwa hatua. Kwenye kila hatua kuna kazi ya kufanya nitakupa, ambapo utaifanyia kazi na kuleta mrejesho. Pia kwenye semina kuna wakati wa maswali na majibu kwa kila siku ya mafunzo. Unaweza wewe ukawa huna swali, lakini maswali ya wengine yakakuwezesha kujifunza zaidi.

Na muhimu zaidi, ni wakati ambapo tunaweza kuwasiliana moja kwa moja kwenye kila jambo nitakalokushirikisha.

Thamani kubwa zaidi ni kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA kwa mwaka mzima. 

Kila siku utaendelea kujifunza mambo mazuri sana kuhusu mafanikio. Hiyo ni thamani ambayo huwezi kuipata kwa kitabu pekee.

Hivyo nakushauri sana, jiunge na semina mapema, ili upate thamani hizi.

Swali; kwa wale ambao hatuwezi kulipia ada kamili, yaani elfu hamsini, kwa nini usituruhusu tukalipa labda elfu 20 na kupata semina tu kisha tukaondoka na tusiwe kwenye kundi kwa mwaka mzima?

Jibu; kwanza kabisa semina hii ni kwa ajili ya wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, ni moja ya matunda ya kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA, ambapo kwa mwaka unapata fursa ya kushiriki semina mbili za njia ya mtandao, na semina moja ya kuhudhuria. Hivyo unapaswa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA ili kufaidi hilo.

Pili, na muhimu zaidi, nataka nikufuatilie baada ya semina. Kwa sababu kama nilivyokuambia, kuna mambo ya kufanyia kazi kwenye hii semina, siyo kusoma tu na kuendelea na yako. Kuna vitu lazima uvifanyie kazi. Na kuna mambo matatu muhimu ambayo nitamfuatilia kila mwanachama kuhakikisha anayafanya, au aondoke kwenye kundi. Mambo hayo ni kuwa na uwekezaji, kuwa na biashara (hata kama ameajiriwa), na kuendelea kujifunza kila siku, angalau kusoma kitabu kimoja kila mwezi. Atakayefanya chini ya hapo, ataondoka kwenye KISIMA CHA MAARIFA, na ada aliyolipa nitamrudishia.

Hivyo njoo kwenye KISIMA rafiki, sababu zote zinazokuzuia zitayeyuka zenyewe.

Swali; ada ni kubwa, kwa nini usipunguze.

Jibu; ada unayolipa ni ya mwaka, yaani kama unalipa ada mwezi wa sita mwaka 2017 ni mpaka mwezi wa sita mwaka 2018. Hii ni ada ya miezi kumi na mbili, hivyo ukigawa ni chini ya elfu tano kwa mwenzi, ukigawa kwa siku ndiyo kabisa kama shilingi mia moja na thelathini hivi.

Hivyo ukisema ni kubwa rafiki, labda uniambie unalinganisha na nini?

Kingine naelewa wengi wanasema kuwa nayo elfu 50 kwa wakati mmoja ni ngumu. sasa hilo ndiyo nataka nikufundishe namna ya kuweka elfu moja moja, mpaka ifike elfu 50 na zaidi bila ya kutumia, hata kama unapata shida kiasi gani.

Swali; kwa nini usiweke ada watu wakalipa kwa mwezi?

Jibu; tulishajaribu hiyo, ni usumbufu kwa kila mtu, kila mara kutoa na kurudisha watu inakuwa usumbufu mkubwa. Lipa ya mwaka na uwe na uhakika wa kujifunza mwaka mzima, baada ya hapo utajitafakari kama uendelee au la.

Swali; sijawahi kushiriki semina hizi za mtandao, sina uhakika kama nitapata thamani inayoendana na ada ninayolipa.

Jibu; karibu sana ushiriki semina hii, maana umeshapitwa na mengi na kama utaendelea na msimamo wako huo, utaendelea kukosa mengi. Sasa hivi mtandao unaathiri kila sehemu ya maisha yetu, hivyo unachopaswa kufanya ni kuangalia unautumiaje kwa manufaa yako.

Kuhusu kuwa na wasi wasi iwapo fedha unayolipa itakuletea thamani kweli, nakupa siri ya kuweza kushiriki semina hii BURE KABISA. Unachofanya, ni kulipia ada ya kushiriki semina, unashiriki semina, halafu tunapofika mwisho, kama hujapata thamani uliyokuwa unategemea, unaniambia na ninakurejeshea ada uliyolipa, bila ya kukuhoji swali lolote.

Naweka nguvu, juhudi na maarifa makubwa sana kwenye kila ninachofanya. Kwa mfano kwa wiki hizi mbili za kuelekea kwenye semina, kila siku nasoma kitabu kimoja mwanzo mpaka mwisho kinachohusu fedha. Nafanya utafiti wa kutosha kuhakikisha nakupatia kitu kinachokusaidia. Nimekutana na watu wa BIMA, watu wa MABENKI kujua kwa kina kuhusu huduma za kifedha wanazotoa. Yote hayo ni kuhakikisha wewe rafiki yangu, unapata kitu ambacho siyo tu utafurahia kukisoma, bali pia utaweza kukifanyia kazi.

Hivyo nakukaribisha ushiriki semina hii, upime mwenyewe, na ukiona hujapata cha kukusaidia, nijulishe na ada uliyolipa nakurejeshea. Nilishakuambia tena, hii ni kazi ambayo nimechagua kuifanya kwa miaka yangu yote. Najua kitu pekee kitakachoniwezesha kwenye miaka yote hiyo ni ubora wa kile ninachofanya, hivyo najali sana ubora wa mafunzo ninayokuandalia.

Rafiki, hayo ni maswali ambayo yamekuwa yanaulizwa na wengi ambao mpaka sasa hawajajiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kama wewe ni mmoja wa watu hawa, ambao bado hawajajiunga kwa sababu yoyote, jiunge leo. Na kama una swali unalo na sijalifafanua hapo, tafadhali tuma moja kwa moja kwa njia ya wasap namba 0717396253 na nitakujibu. Usitume swali kwenye email, ninaweza kuchelewa kuliona kwa sababu email huwa ni nyingi, nikaja kukujibu kesho wakati muda wa kujiunga utakuwa umepita.

Chukua hatua leo rafiki, hii ni fursa ya kipekee ambayo haitajirudia tena.

Rafiki, kama bado hujajiunga, tuma ada yako leo, tsh 50,000/= kwa namba 0755 953 887 au 0717396253 kisha tuma ujumbe kwenye wasap namba 0717 396 253 na nitakuweka kwenye kundi la semina. Kumbuka imebaki siku moja pekee. Usikose nafasi hii nzuri, chukua hatua leo.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: