Hivi Ndivyo Unavyopoteza Fedha Kila Siku Bila Ya Wewe Mwenyewe Kujua.

Habari za leo rafiki yangu?

Napenda kuchukua nafasi hii kukufahamisha kwamba semina yetu ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA ambayo ilifundishwa kwa njia ya mtandao, kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, imemalizika vizuri sana.

Imekuwa ni moja ya semina bora sana kwangu kuwahi kufanya, na pia imekuwa semina bora kwa washiriki wote. Kila aliyeshiriki yapo mambo mazuri sana aliyojifunza.

Kitu kikubwa sana ambacho kila mshiriki wa semina alijifunza, ni kuhusu maeneo mbalimbali ambayo kila mtu anapoteza fedha. Baada ya somo la matumizi madogo madogo, wengi walienda kuomba statement kwenye benki zao, na hapo ndipo walipoona jinsi gani wanapoteza fedha. Ukweli ni kwamba, kila mmoja wetu, kuna namna anachagua kupoteza fedha, bila hata ya yeye mwenyewe kujua. Ndiyo, hata wewe hapo ulipo sasa, kuna fedha unapoteza bila hata ya kujua.

Nachukua nafasi hii kuwashukuru wasomaji wote ambao walishiriki semina hii, wameweza kupata maarifa sahihi kuhusu fedha.

Leo mimi sitakuandikia mengi, bali nitakupa sehemu ndogo ya ushuhuda wa walioshiriki kwenye semina hii ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA.

Soma ushuhuda huu kisha mwisho nitakupa mpango mzuri wa kujifunza kama ulikosa semina hii.

Habari za jioni coach. Binafsi nimejifunza mengi sana kwenye semina hii kubwa kuliko yote ambalo Kwangu lilikuwa geni kabisa ni juu ya kutenga mafungu ya kipato na pia suala la kubana matumizi hizo mbili ni elimu mpya kabisa nilikuwa naishi tu kama ng’ombe bila kuwa na utaratibu. Jambo lingine ambalo nimefaidika sana ni kuandika matumizi yoyote ya hela ninayofanya na pia kuwa na kijitabu cha kumbukumbu ya jambo lolote ninalopanga kufanya au ninalosikia lenye manufaa

Barikiwa sana – Elisha Mwambapa

Kocha kwanza kabisa namshukuru Mungu wa mbinguni kwa kunipa uhai na kuniwezesha kunikutanisha na mtandao wako wa KISIMA CHA MAARIFA, kweli nikiri ni kisima cha maarifa, jina limesanifu kilichomo. Ushuhuda wangu kuhusu semina hii iliyopita iliyokuwa inahusu KUIFAHAMU MISINGI YA KIFEDHA ILI KUWA NA UHURU WA KIFEDHA, imenisaidia sana kwa kunipa maarifa ambayo nilikuwa sina kabisa, yawezekana isingekuwa kisima cha maarifa nisingeyapata mahali popote, Maana binadamu wengi ni wanafiki pale linapokuja swala la mafanikio ya kifedha, wengi hawasemi ukweli, Ila kupitia hii semina nimekutana na mtu mmoja anayesema ukweli kuhusu maisha ya mafanikio hasa ya KIFEDHA, anaitwa Makirita Aman, Hakika kocha umenifunza mengi sana… haswa swala la matumizi na mapato, nilikuwa sijui kuwa matumizi madogo madogo usipoyaandika hutajua pesa imeishaje! Kweli nimeanza kuandika sasa hivi nimeshaanza kuona pesa zangu zilikuwa zinapotelea wapi… MATUMIZI yalikuwa makubwa kuliko MAPATO, halafu bila kufahamu najifariji kuwa nina kipato, kumbe hakuna. Yaani kocha ni mengi sana nimejifunza kama kuweka akiba, dharura, n.k nilikuwa siweki hapo kabla, Naahidi kufanyia Kazi niliyojifunza kwa vitendo km nilivyoanza sasa hivi. Asante sana kwa semina, na ninaahidi semina mubashara( ana kwa ana) nitakuja kama itakuwepo. ASANTE, Ni mimi FUTUREBILLIONAIRE, Deus Yegera Mashauri.(dy)

Namshukuru mwalimu kwa semina hii ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA. Hii ni elimu ambayo kila mtu anapaswa kuipata bila kujali level yake ya elimu kutaaluma. Kuna mengi nimejifunza, mengine ni mapya na mengine sio mapya. Hata yale ambayo sio mapya, cha ajabu ni kuwa sikuwahi kuyafanyia kazi. Kabla ya semina hii kuisha kuna ambayo tayari nimeishayafanyia kazi. Majibu ya changamoto nyingi tunazoziona kila siku yamo ndani ya semina hii. Nashauri kila atakayekutana na ujumbe huu ayapate maarifa haya bila kusita. Mwalimu wa semina hii ana kiwango cha juu cha nidhamu ambacho sijawahi kukiona kwa mtu mwingine yeyote na kuna kitu cha ziada cha kujifunza mbali na maudhui ya semina yenyewe. – Mtabazi Geofrey Sahini.

Asante sana kocha kwa semina hii nzuri sana. Pamoja na kuwa na umri mkubwa, elimu nzuri na kubahatika kuhudhuria semina nyingi, kwa kweli hii ni ya kipekee kabisa. Maandalizi bora kabisa, na mada safi. Kuhusu bajeti kwa mfano, nilikuwa najidanganya kuwa iko kichwani. Baada ya kugawa kipato na kuandika matumizi yote nimejishangaa nilivyojidanganya na kupata hasara kubwa. Nimenufaika na kutotembea na pesa nyingi mfukoni. Kumbe nilikuwa natumia hela ovyo sana. Kuhusu masharti ya kubaki kisimani… Hapo ndipo penyewe… itabidi kwa namna yeyote nibaki maana bila hii chemchem mimea yangu yote niliyopanda itanyauka. – Mary Materu

Hii ni sehemu ndogo ya shuhuda za washiriki wa semina hii rafiki. Watu wamejifunza mengi na wameshaanza kuyafanyia kazi, hasa kwenye eneo la kipato na matumizi. Watu wengi wameona jinsi wanavyopoteza fedha nyingi bila ya wao kujua.

Ukweli ni kwamba, pamoja na kulalamika kwamba huna fedha, kuna fedha nyingi unazipoteza hapo ulipo sasa. Kila mtu, hata asiye na fedha za kutosha, kuna fedha anapoteza kila mwezi. Na siyo chini ya elfu kumi, wengine wanaenda mpaka laki moja.

NAFASI NZURI YA KUPATA MASOMO HAYA KAMA HUKUWEZA KUSHIRIKI.

Wakati masomo haya yanaendelea, washiriki wengi walikuwa wakisema haya ni masomo muhimu sana ambayo kila mtu anapaswa kuyapata. Waliona namna yanawafungua wao, na kutamani yaweze kuwafungua wengine pia ili nao watoke kwenye giza na vifungo vya madeni na changamoto za kifedha.

Hivyo nimefikiri kwa kina ni namna gani wale waliokosa semina hii kwa sababu mbalimbali wanaweza kupata masomo haya na yakawasaidia. Hivyo upo mpango ambao nimeandaa, wa kuhakikisha kila mtu anaweza kupata mafunzo haya na yakamsaidia. Nipo katika hatua za mwisho za kuweka sawa mfumo huo wa mafunzo. Kwenye makala nitakayotuma alhamisi nitawajulisha kuhusu hilo.

Ila kwa sasa, kama ulikosa semina hii, na ungependa sana kuyapata mafunzo haya ya semina ili uweze kujijenga vizuri kifedha, jibu email hii au nitumie email kwenye amakirita@gmail.com ukiniambia kamba ulikosa mafunzo haya na sasa upo tayari kuyapata. Karibu sana.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: