Tupa Sababu Zako Kule…Anza Kutimiza Ndogo Zako Hivi.

Kati ya kitu ambacho kinaua mafanikio yako sana ni sababu ulizonazo. Sina uhakika kama unalijua sana hili, au unafanya makusudi kuleta sababu zako kila wakati kwamba hujachukua hatua kwa sababu hii au ile.
Labda nikwambie hivi, kama umekuwa upo hapa AMKA MTANZANIA kwa muda mrefu, utakuwa unajua moja kati ya kitu ambacho tunapiga vita sana ni kuleta sababu wakati unatafuta mafanikio.
Ila, kama wewe ni mgeni, nikukaribishe karibu kwenye nyumba ya mafanikio, lakini  uelewe kwamba kama unataka kufikia mafanikio, tupa sababu zako kule na anza kuchukua hatua za kutimiza ndoto zako sasa. Nimesema anza kuchukua hatua sasa.
Huhitaji kujiuliza sana kwa nini nakwambia hivyo, kama ni sababu kila mtu anazo, kama ni hayo unayoita matatizo kila mtu anayo kwa sehemu yake, kama unabisha nitafutie ni nani ambaye hana chnagamoto kwenye hii dunia?
Chukua hatua, achana na kila aina ya sababu.

Kila mtu kwenye dunia hii anachangamoto zake, tena za wengine ni kubwa kuliko za kwako. Sasa, dunia au maendeleo hayawezi kusimama eti kwa kigezo cha sababu mbalimbali, hilo haliwezi kutokea.
Ndio maana kama kiu ma hasira yako ni kujenga mafanikio,huna ujanja rafiki yangu, nakwambia tupa sababu zako kule anza kutimiza ndogo  kwa kuchukua hatua. Hutaki kuchukua hatua, naomba nikwambie huwezi kufaniwa.
Nakwambia kama una sababu huwezi kufanikiwa sio kwa sababu sitaki ufanikiwe, au sio kwa sababu mimi nataka kuwa mchawi wa maisha yako, hapana, hautafanikiwa kwa sababu ndiyo kanuni za kimaumbile zilivyo, kanuni hizo hazitaki sababu bali matokeo.
Oooh, labda ulikuwa haujui kitu fulani nikwambie hivi, dunia haijiendeshi kwa bahati mbaya kama unavyofikiri, ipo misingi ya kila kitu. Sasa hutaki kufata misingi hiyo sahau mafanikio na huwezi kupata kama unaenda kinyume.
Hakuna unayehitaji sababu zako hata mmoja, sababu hata ziwe nzuri vipi na hata ukataka kuzitungia nyimbo na kuziwekea ‘remix’ hazina maana yoyote. Tupa sababu zako kule na anza kuchukua hatua kidogo kidogo za kuelekea kwenye mafanikio yako.
Huhitaji kusema sina mtaji, anza na pale ulipo. Huwezi kukimbia tembea, huwezi kutembea tambaa, kikubwa mwendo wako uonekane, kama iko hivyo unaleta sababu za nini, hakuna sababu kinachotakiwa ni vitendo vya kuelekea mafanikio yako..
Huhitaji kumlaumu mtu kwenye maisha yako, huhitaji kuilaumu serikali eti kwa sababu umekosa ajira ndio maana hujafanikiwa. Kama unataka kufanya hayo endelea, lakini mwisho wa siku utakuja kujua sababu zako hazina maana.
Kama ni kweli umeamua kufanya kitu, fanya na anza hata kwa kidogo, ila kubwa kuliko yote ni kwamba, tupa sababu zako kule, tupa lawama zako kule, tupa malalamiko yako kule na anza kuchukua hatua kuelekea kutimiza ndoto zako.
Kwa makala nyingine nzuri za mafanikio na maisha pia tembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kwa ajili ya kujifunza na kuhamasika..
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Email; dirayamafanikio@gmail.com

One thought on “Tupa Sababu Zako Kule…Anza Kutimiza Ndogo Zako Hivi.

Add yours

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: