Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Amka Mtanzania? Ni matumaini yangu kuwa hujambo na unaendelea vizuri. Hongera sana rafiki kwa zawadi ya siku hii ya leo kwani kuamka salama ni ushindi mkubwa katika maisha yako hivyo tumia ushindi huo wa uhai kuacha alama siku hii ya leo kumbuka kuwa maisha ni muda. Kumbuka kuiendea siku hii ya leo kwa misingi yetu ya Amka Mtanzania ya nidhamu, uadilifu na kujituma.

Rafiki, napenda kutumia nafasi hii kukualika tena siku hii ya leo katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja yale mazuri niliyoweza kukuandalia siku hii ya leo. Kwa namna ya pekee rafiki yangu, nakusihi sana tusafiri pamoja hadi mwisho wa somo letu la leo ambapo leo tutakwenda kujifunza tapeli anayetapeli watu wengi katika maisha ya watu. Je unamjua tapeli huyo? Karibu tujifunze.

Rafiki, tunaishi katika zama za mambo mengi na kila kukicha mambo mengi yanazidi kuongezeka. Licha ya kuwa na mambo mengi ya kufanya ambayo yako kabisa ndani ya uwezo wetu lakini amejitokeza adui mwingine ambayo anaingilia kati ili kutunyang’anya ushindi lakini pia kutuzuia sisi kusonga mbele.

Watu wengi wamejuta na kulizwa na huyu adui. Ni adui mbaya kwa sababu ameharibu ndoto nyingi za watu wengi na licha tu ya kuharibu lakini amesababisha ongezeko la viporo vingi vya majukumu katika maisha yetu ya kila siku. Watu wengi wanashindwa kufanya mambo mengine mapya kwa sababu ya kumruhusu huyu adui amtawale katika maisha yake.

Procrastination-04-despair

Tumekuwa tunaishi na tapeli ambaye tumemfanya kuwa rafiki wa kujiridhisha pale tunapohisi tumechoka kufanya kitu fulani. Watu wengi wanamwalika tapeli huyu katika maisha yao na ubaya wa tapeli huyu hawezi kukuacha salama kama umemkaribisha katika maisha yako. Ananyang’anya ushindi wa watu wengi, watu wanashindwa kutimiza wajibu wao kwa wakati kwa sababu ya huyu tapeli.

SOMA; Hiki Ndiyo Kitu Kinachosababisha Kuona Maisha Yako Ni Magumu Na Hayana Maana.

Mpendwa msomaji, huenda nimekuacha njia panda katika fikara yako je huyo tapeli ni nani anayefanya yote haya katika maisha yetu? Tapeli huyo anayeharibu maisha ya watu wengi kwa kuendelea kuwatapeli kila siku katika maisha yao siyo tapeli miwngine bali BAADAYE. Baadaye amekuwa ni sumu wa maendeleo katika maisha yetu na imekuwa ndiyo njia ya wavivu wengi kukimbilia huko na kusarenda maisha yao kwa tapeli huyo.

Ni wazi kabisa watu wengi wamekuwa wakijidanganya katika maisha yao kwa kumwalika tapeli huyu katika maisha yao. Baadaye imekuwa ni kama kimbilio la watu waliokosa nidhamu binafsi katika maisha yao. Watu wanashindwa kutumia falsafa ya kufanya sasa na hivyo wanachoona ni kumwachia nafasi tapeli wa baadaye ili amtapeli. Na huwa sisi wenyewe ndiyo tunamruhusu tapeli huyu aweze kututapeli katika maisha yetu. Kama sisi tukikataa na kuamua kufanya sasa yale majukumu yetu ambayo tunapaswa kuyatimiza basi tapeli huyu anakuwa hana nafasi tena katika maisha yetu.

Ni wangapi wanaahirisha mambo yao kila siku na kuamua kumpa ushindi tapeli huyu wa baadaye. Tunashindwa kufanya mambo mengi kwa sababu ya kutawaliwa na huyu tapeli. Uzuri wa huyu tapeli ukisha mwambia hapana kubwa hawezi kukusogelea hata kidogo na atakuwa anakuogopa kabisa. Nguvu na uwezo wa kumkataa upo ndani yako wenyewe wala huhitaji mtaji wa pesa bali ni mtaji mkubwa wa kumkabili tapeli huyu ni kuwa na nidhamu ya kufany sasa. Hakuna sababu juu ya tapeli huyu na wale wote waliokosa nidhamu binafsi basi baadaye ndiyo mteja wao mzuri.

Hatua ya kuchukua leo, kaa chini ujiulize je ni mambo mangapi umeharibu kwa kumwalika tapeli huyu mkubwa wa baadaye? Tokea uanze kutapeliwa na huyu baadaye umepata faida gani chanya? Kama hakuna faida yoyote ya huyu tapeli kwanini sasa unaendelea kukaa naye? Basi leo chukua hatua ya kumpa talaka ukiona baadaye anaanza kukusogelea mpe kadi nyekundu mwambie hapana kwa kumwalika rafiki yako wa sasa ambaye ni fanya sasa.

SOMA; UCHAMBUZI WA KITABU; Procrastinate On Purpose (Ruhusa Tano Za Kujipa Ili Kuzidisha Muda Wako).

Kwahiyo, kama tunataka kupata matokeo mazuri katika maisha yetu tukubali kwanza kuishi sasa na kufanya yale yote ambayo tunayoweza kufanya sasa. Baadaye waachie watu ambao hawana nidhamu katika maisha yao, ambao wameruhusu kutapeliwa katika maisha yao na wamezoea kulipa gharama kubwa ya kutapeliwa kwa kuwa na majukumu mengi kupita maelezo. Nitafanya baadaye ni kikwazo katika jamii yetu ya leo.

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com, kessydeo@mtaalamu.net  au unaweza kutembelea tovuti yake, www.mtaalamu.net/kessydeo ,www.actualizeyourdream.blogspot.com kwa kujifunza zaidi kila siku. Asante sana.