Rafiki yangu mpendwa,

Siku ya leo ni siku muhimu sana kwa kila mmoja wetu. Ni siku ambayo tumepata nafasi nyingine nzuri ya kwenda kuweka juhudi kubwa kwenye chochote ambacho tunafanya ili kuweza kupata matokeo bora sana.

Karibu kwenye makala ya ushauri wa changamoto ambapo tunashauriana mambo muhimu ya kufanya pale mtu unapokuwa umekwama na kukwama huko kunakuzuia kufikia malengo yako.

Kwenye makala ya leo tutaangalia hatua muhimu za kuchukua pale biashara inapokuwa haitoki au kujiendesha kwa hasara. Lakini kabla hatujaangalia kipi cha kufanya, kwanza tupate maoni ya msomaji mwenzetu aliyetuandikia kuomba ushauri kwenye hili;

Naomba ushauri nilikua namfanyia mtu kazi ya duka kwa muda wa miaka 6 ila biashara haikuwa nzuri, kaamua kuniachia chumba na kunipa mtaji 15,000,000 ili nizungushe lakini hali imegoma biashara haitoki nimebadili biashara ya furniture nayo ndio kabisa mtaji wote umeishia hapo yaani sina hata hela ya kumrudishia na ananisumbua sana nimpe pesa yake yaani natamani hata kujiua ila yeye binafsi hanidai kamuchia mwanamke anidai yaani natamani kuchukua maamuzi magumu. Je nifanyeje? – Edward K. M.

Kwako Edward na marafiki wengine ambao mnapitia changamoto ya namna hii, ambapo biashara imegoma kutoka na inajiendesha kwa hasara. Kila biashara huwa ina changamoto zake, hivyo kujiandaa vyema na kujua hatua zipi muhimu kuchukua mambo yanapokuwa magumu, inasaidia kuondokana na changamoto na kuikuza biashara yako.

Zifuatazo ni hatua muhimu za kuchukua ili kuokoa biashara ambayo inajiendesha kwa hasara na haitoki.

Moja; UZA.

Fedha ndiyo damu ya biashara na mauzo ndiyo njia pekee ya kuingiza fedha kwenye biashara. Kila biashara yenye matatizo, ukiangalia kwa kina, mambo yote yanaanzia kwenye mauzo. Hivyo eneo la kwanza kufanyia kazi kwenye ukuaji wa biashara yako ni kwenye mauzo.

Unaposema kwamba biashara haitoki, maana yake mtu huuzi, unaposema biashara inapata hasara, maana yake haiuzi vya kutosha, au mauzo hayawezi kukidhi matumizi ya biashara.

Hivyo hatua ya kwanza ni kuhakikisha umeuza. Unahitaji kuwafikia wateja wapya na wateja wengi zaidi. Usiendeshe biashara kwa mazoea kwamba kwa sababu ipo basi watu watakuja. Au kwa sababu watu walishanunua kwako basi wataendelea kununua kwako.

Endesha biashara yako kwa kutafuta masoko muda wote, kila wakati hakikisha kuna wateja wapya wanaifahamu biashara yako.

095a5b996f7db11bfe3b1d93a17b444b.0

Mbili; USITUMIE MTAJI WA BIASHARA.

Mkulima yeyote mwenye akili timamu na anayejua anafanya nini na maisha yake, hata njaa iwe kali kiasi gani kwake, hawezi kula mbegu. Kwa sababu anajua akila mbegu atapooza njaa ya leo pekee, lakini atakuwa amepoteza kitu kikubwa sana kwa ajili ya baadaye.

Kadhalika mfanyabiashara mwenye kujua wapi anakwenda na biashara yake, hawezi kutumia mtaji wa biashara yake kama matumizi yake ya maisha. Sasa ni rahisi kusema hutumii mtaji. Ninachotaka kukuambia ni kwamba, kama biashara haipati faida, basi fedha yoyote unayoitoa kwenye biashara kwa ajili ya matumizi ni kwamba unatumia mtaji, unakula mbegu na unajiharibia kwa maisha ya baadaye.

Kama biashara haina faida, usitoe hata senti moja kwenye biashara yako kwa ajili ya matumizi. Utajua utaishije, kama utalala njaa, kama hutanunua nguo, kama utakula vyakula vya ajabu kwa kipindi fulani ni sawa, lakini usile mtaji.

Kama ulianza biashara na mtaji wa milioni 15, lakini sasa ukipiga hesabu hata huo mtaji haufiki tena, jibu rahisi ni kwamba ulichokuwa unafanya ni kula mtaji, na hakuna biashara inayoweza kupona kama mtaji unaliwa.

Ili kujua kama biashara inajiendesha kwa faida au hasara, unahitaji kuwa na hesabu za fedha kila wakati, kila siku, kila wiki, kila mwezi na kila mwaka. Kuwa na hesabu hizi na kama hakuna faida, angalia namna nyingine ya kuendesha maisha yako na siyo kula mtaji wa biashara.

Tatu; ELEWANA VIZURI NA UNAOSHIRIKIANA NAO.

Ushirika na ubia kwenye biashara ni kitu kizuri, kwa sababu mnakusanya rasilimali pamoja kwa matumizi ya biashara. Wewe unaweza kuwa na wazo na muda, lakini huna fedha. Mwingine ana fedha na wazo lakini hana muda. Mkikutana na kupanga vizuri mnaweza kuanza biashara.

Sasa mambo yanapokwenda vizuri, biashara inapata faida kila mtu anafurahia na kila mtu ananufaika. Lakini mambo yanapokwenda vibaya, biashara ikawa inapata hasara, lazima apatikane mtu wa kulaumiwa, na mara nyingi ni yule anayetumia muda mwingi kwenye biashara hiyo.

Ni muhimu sana mkawa na makubaliano mazuri na wale unaoshirikiana nao kwenye  biashara. Kila mtu ajue wajibu wake ni upi na ategemee nini kwenye biashara. Mtu yeyote unayeshirikiana naye kwenye biashara, kama faida inamnufaisha, basi hasara pia inapaswa kumhusu, na hilo lazima liwe kwenye makubaliano yenu. Kwamba kila mmoja wenu atakazana kadiri ya uwezo wake ili biashara iende vizuri, lakini inapopatikana hasara isiwe mzigo wa mtu mmoja.

Lakini kama walichokupa wale unaoshirikiana nao ni mkopo, basi huna budi kulipa. Hivyo utahitaji kukaa nao chini, kuwaeleza hali halisi ya biashara, kuwaeleza mpango ulionao na jinsi utakavyowalipa kidogo kidogo. Mkishakubaliana kwenye malipo, weka juhudi kwenye biashara yako ili uweze kulipa deni. Dawa ya deni ni kulipa, na kadiri unavyolipa mapema, ndivyo unavyokuwa huru kufanya yale muhimu kwako.

Hizo ndiyo hatua tatu muhimu za kuchukua ili kuinusuru biashara yako isiendelee kupata hasara na hata kufa. Ni imani yangu utachukua hatua ili kuweza kukuza zaidi biashara yako.

Je unataka kuikuza biashara yako zaidi? Je unataka kupata faida kwa zaidi ya asilimia 50 kwa mwaka? Kama jibu ni ndiyo, basi endelea kusoma hapo chini;

HABARI NJEMA KWA WAFANYABIASHARA WOTE.

Nimeandaa semina ya biashara inayokwenda kwa jina; NJIA TANO ZA KUKUZA BIASHARA YAKO, Ongeza Faida Kwa Zaidi Ya Asilimia 50 Ndani Ya Mwaka Mmoja.

Hii ni semina ambayo kila mfanyabiashara, na hata mfanyabiashara mtarajiwa atajifunza jinsi ya kuongeza faida kwenye biashara yake kwa zaidi ya asilimia 50 ndani ya mwaka mmoja.

Watu wengi wamezoea faida kuwa asilimia 10 na ikizidi sana asilimia 20 kwa mwaka. Kwenye semina hii unakwenda kujifunza mbinu 50 ambazo unakwenda kuzifanyia kazi kwenye biashara yako na faida itaongezeka kwa zaidi ya asilimia 50.

Semina hii utajifunza kwa namna ya kuchukua hatua, hivyo haitakuwa ya kujua tu, bali utakuwa na kila hatua ya kuchukua.

MAELEZO ZAIDI YA SEMINA HII NI KAMA IFUATAVYO;

Katika semina hii muhimu sana kuhusu biashara, tutakwenda kujifunza yafuatayo;

UTANGULIZI; Umuhimu wa biashara na ukuaji wa biashara kwenye zama tunazoishi sasa, maeneo matatu muhimu sana kwenye ukuaji wa biashara yako.

NJIA YA KWANZA; WATEJA TARAJIWA, njia 10 za kuwafikia wengi zaidi na biashara yako.

NJIA YA PILI; KIASI CHA WATEJA TARAJIWA WANAOKUWA WATEJA HALISI, njia 10 za kuwashawishi wanaoijua biashara yako kuwa wateja.

NJIA YA TATU; IDADI YA MIAMALA AMBAYO MTEJA MMOJA ANAFANYA, njia 10 za kuongeza idadi ya miamala mteja anayofanya.

NJIA YA NNE; WASTANI WA FEDHA ANAYOLIPA MTEJA, njia 10 za kuongeza wastani wa malipo anayofanya mteja kwenye biashara yako.

NJIA YA TANO; KIASI CHA FAIDA KWENYE KILA UNACHOUZA, njia 10 za kuongeza kiasi cha faida kwenye kila unachouza.

HITIMISHO; KANUNI SAHIHI YA KUTUMIA ILI KUKUZA BIASHARA YAKO KWA KUONGEZA FAIDA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 50 KWA MWAKA.

Njia hizi tano za kukuza biashara zinategemeana, na kama ambavyo tutajifunza kwenye semina hii inayokuja, zote zinafanyika kwa pamoja na siyo kwamba unachagua njia moja na kuacha njia nyingine.

Nikukaribishe sana rafiki yangu kwenye semina hii ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, ni semina ambayo imekuja wakati sahihi kwako kwa sababu kila biashara zina changamoto na kipindi hichi, changamoto zimekuwa nyingi zaidi.

Semina hii itafanyika kwa njia ya mtandao, kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo unaweza kushiriki semina hii ukiwa popote pale, bila ya kuhitajika kusafiri au kuacha shughuli zako. Unachohitaji kufanya ni kutenga muda kwenye siku yako ya kufuatilia masomo haya na kisha kufanyia kazi.

Semina hii nzuri itafanyika mwezi julai 2018, itafanyika kwa siku saba, kuanzia tarehe 05/07/2018 mpaka tarehe 11/07/2018. Hizi zitakuwa ni siku saba za kujifunza mambo ambayo yataifanya biashara yako iweze kukua kwa kiasi kikubwa sana.

Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii unahitaji kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Ukishakuwa mwanachama huhitaji kulipa gharama za ziada kushiriki semina hii.

Kama bado hujawa mwanachama, unapaswa kulipa ada ya mwaka ya KISIMA CHA MAARIFA, ambayo kwa sasa ni shilingi elfu hamsini (50,000/=). Hii ni ada ya mwaka mzima, ambayo inakupa nafasi ya kuendelea kujifunza kila siku kwa mwaka mzima tangu ulipolipia.

Ili kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma ada, tsh 50,000/= kwa MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/ AIRTEL MONEY 0717 396 253 majina yatakuja AMANI MAKIRITA.

Ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye majina yako kamili na email yako kisha utaunganishwa kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA na kuendelea kupata mafunzo.

Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii, inabidi uwe umejiunga na KISIMA CHA MAARIFA kabla ya tarehe 05/07/2018. Hivyo mwisho kabisa wa kujiunga ili unufaike na semina hii vizuri itakuwa tarehe 03/07/2018

Karibu sana kwenye semina ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, uondoke na vitu vya kwenda kufanyia kazi kwenye biashara yako ili iweze kukua kwa kiasi kikubwa na uweze kufikia malengo makubwa uliyojiwekea kwenye maisha yako.

Nakutakia utekelezaji mwema wa yale ambayo umejifunza,

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

TOA CHANGAMOTO YAKO USHAURIWE

Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog