Rafiki yangu mpendwa,

Biashara ni ngumu lakini wapo ambao wamechagua kuzifanya kuwa ngumu zaidi.

Yapo makosa ambayo wafanyabiashara wengi wamekuwa wakiyafanya, na yanapelekea biashara zao kuwa ngumu sana.

Iko hivi rafiki, kwenye biashara, fedha ni matokeo ya kufanya kitu sahihi. Yaani kama unafanya kitu sahihi, kama una bidhaa na huduma sahihi, ambayo watu wanaihitaji na unawapatia kwa njia ambayo wanaweza kuitumia, basi unapaswa kupata fedha.

Kama upo kwenye biashara na hupati fedha, basi kuna kitu unakosea, kuna kitu ambacho hufanyi kwa usahihi na hicho ndiyo kinakurudisha nyuma.

Lipo kosa moja ambalo wafanyabiashara wengi wamekuwa wanafanya kwa wateja wao, na limekuwa linachangia wao kukosa wateja wa biashara hizo na hivyo kukosa kipato kizuri.

Unapochagua

Kosa hilo ni kuhangaika na wateja ambao siyo sahihi kwa biashara yako.

Rafiki, kila biashara ina wateja sahihi kwa biashara hiyo, na hakuna biashara ambayo mteja anaweza kuwa kila mtu. Hata kama unauza maji ambayo yanatumika na kila mtu, bado siyo kila mtu atakuja kununua maji unayouza. Na hata ukiyauza kwa bei ya punguzo, hata ungeyatoa bure kabisa, bado siyo wote wangehangaika nayo.

Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakifikiria kwamba wanahitaji kumshawishi kila mtu anunue kile wanachouza. Hivyo wanapoteza nguvu nyingi kwenye kuwashawishi watu kununua, nguvu ambazo kama wangezitumia vizuri kwa wateja sahihi, wangeweza kuwapa thamani kubwa zaidi.

Lazima ujue na ukubali kwamba watu wengi hawatakuwa wateja wa biashara yako, hata kama kwa nje unaona wanaihitaji, hawatakuwa tayari kulipia kupata unachouza. Hivyo kukazana kuhangaika na kila mtu, ni njia ya uhakika ya kushindwa kwenye biashara yako.

Unahitaji kuwajua wale wateja ambao wana uhitaji hasa wa kile unachouza, wenye uwezo wa kukilipia na ambao wapo tayari kulipia kukipata. Hawa ni wale ambao wana uhitaji mkubwa, au wana maumivu makubwa kiasi kwamba kwao kulipia kile unachotaka walipie ni maumivu madogo kuliko yale wanayoyapata kwa kutokulipia.

Unahitaji kuamua kwa dhati juu ya hilo, ili kuiweka biashara yako kwenye mfumo ambao utahangaika na wale ambao wanahusika.

Usikazane kukimbizana na kila mtu, na watu wengi watakuja kwako na maoni mengi kuhusu biashara yako, wapo watakaokuambia bei ni kubwa, lakini hata ungepunguza bei bado hawatanunua. Wapo watakaokuambia uongeze kitu fulani wakati hawajawahi hata kununua.

Ukishajua kile hasa unachotoa, na matatizo au changamoto za wengine ambazo unatatua, kinachofuata ni wewe kuwatafuta wateja sahihi wa biashara yako. Acha kukimbizana na kila mtu kwenye biashara yako, acha kuifanya biashara yako imfae kila mtu.

Kwa kufanya haya tunayojifunza, utatengeneza aina ya watu ambao watakuwa wakosoaji wakubwa wa biashara yako. Wapo watakaokuambia unafanya makosa makubwa, wapo watakaokuambia unapoteza fedha nyingi, lakini unahitaji kuwaangalia je wao ni fedha zipi wanazopata ambazo wewe hupati kabla hujakimbilia kupokea ushauri wao.

Muda wako una ukomo, nguvu zako zina mwisho hivyo unahitaji kuwa makini kwa namna unavyotumia rasilimali hizo mbili kwenye biashara yako. Zitumie kuhakikisha unawafikia watu sahihi, unawasaidia kutatua matatizo na changamoto wanazopitia na kuhakikisha maisha yao yanakuwa bora.

Hayo muhimu yakishakuwa sawa, unachohitaji kukazana ni kuwafikia watu sahihi, wale wanaojali, wale wanaoweza kulipia na wapo tayari kufanya hivyo.

Watu wengi hawataendana na biashara unayofanya, lakini wapo wachache ambao wataielewa na watakuwa tayari kulipia na kuwa wateja. Ni jukumu lako kama mfanyabiashara kuwajua hao wachache muhimu na kuweka juhudi kuyafanya maisha yao kuwa bora.

Rafiki yangu, je ungependa kupata wateja zaidi ambao ni sahihi kwa biashara yako? Je ungependa kuongeza faida zaidi kwenye biashara yako? Ninazo habari njema sana kwako rafiki yangu.

HABARI NJEMA KWA WAFANYABIASHARA WOTE.

Nimeandaa semina ya biashara inayokwenda kwa jina; NJIA TANO ZA KUKUZA BIASHARA YAKO, Ongeza Faida Kwa Zaidi Ya Asilimia 50 Ndani Ya Mwaka Mmoja.

Hii ni semina ambayo kila mfanyabiashara, na hata mfanyabiashara mtarajiwa atajifunza jinsi ya kuongeza faida kwenye biashara yake kwa zaidi ya asilimia 50 ndani ya mwaka mmoja.

Watu wengi wamezoea faida kuwa asilimia 10 na ikizidi sana asilimia 20 kwa mwaka. Kwenye semina hii unakwenda kujifunza mbinu 50 ambazo unakwenda kuzifanyia kazi kwenye biashara yako na faida itaongezeka kwa zaidi ya asilimia 50.

Semina hii utajifunza kwa namna ya kuchukua hatua, hivyo haitakuwa ya kujua tu, bali utakuwa na kila hatua ya kuchukua.

MAELEZO ZAIDI YA SEMINA HII NI KAMA IFUATAVYO;

Katika semina hii muhimu sana kuhusu biashara, tutakwenda kujifunza yafuatayo;

UTANGULIZI; Umuhimu wa biashara na ukuaji wa biashara kwenye zama tunazoishi sasa, maeneo matatu muhimu sana kwenye ukuaji wa biashara yako.

NJIA YA KWANZA; WATEJA TARAJIWA, njia 10 za kuwafikia wengi zaidi na biashara yako.

NJIA YA PILI; KIASI CHA WATEJA TARAJIWA WANAOKUWA WATEJA HALISI, njia 10 za kuwashawishi wanaoijua biashara yako kuwa wateja.

NJIA YA TATU; IDADI YA MIAMALA AMBAYO MTEJA MMOJA ANAFANYA, njia 10 za kuongeza idadi ya miamala mteja anayofanya.

NJIA YA NNE; WASTANI WA FEDHA ANAYOLIPA MTEJA, njia 10 za kuongeza wastani wa malipo anayofanya mteja kwenye biashara yako.

NJIA YA TANO; KIASI CHA FAIDA KWENYE KILA UNACHOUZA, njia 10 za kuongeza kiasi cha faida kwenye kila unachouza.

HITIMISHO; KANUNI SAHIHI YA KUTUMIA ILI KUKUZA BIASHARA YAKO KWA KUONGEZA FAIDA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 50 KWA MWAKA.

Njia hizi tano za kukuza biashara zinategemeana, na kama ambavyo tutajifunza kwenye semina hii inayokuja, zote zinafanyika kwa pamoja na siyo kwamba unachagua njia moja na kuacha njia nyingine.

Nikukaribishe sana rafiki yangu kwenye semina hii ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, ni semina ambayo imekuja wakati sahihi kwako kwa sababu kila biashara zina changamoto na kipindi hichi, changamoto zimekuwa nyingi zaidi.

Semina hii itafanyika kwa njia ya mtandao, kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo unaweza kushiriki semina hii ukiwa popote pale, bila ya kuhitajika kusafiri au kuacha shughuli zako. Unachohitaji kufanya ni kutenga muda kwenye siku yako ya kufuatilia masomo haya na kisha kufanyia kazi.

Semina hii nzuri itafanyika mwezi julai 2018, itafanyika kwa siku saba, kuanzia tarehe 05/07/2018 mpaka tarehe 11/07/2018. Hizi zitakuwa ni siku saba za kujifunza mambo ambayo yataifanya biashara yako iweze kukua kwa kiasi kikubwa sana.

Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii unahitaji kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Ukishakuwa mwanachama huhitaji kulipa gharama za ziada kushiriki semina hii.

Kama bado hujawa mwanachama, unapaswa kulipa ada ya mwaka ya KISIMA CHA MAARIFA, ambayo kwa sasa ni shilingi elfu hamsini (50,000/=). Hii ni ada ya mwaka mzima, ambayo inakupa nafasi ya kuendelea kujifunza kila siku kwa mwaka mzima tangu ulipolipia.

Ili kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma ada, tsh 50,000/= kwa MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/ AIRTEL MONEY 0717 396 253 majina yatakuja AMANI MAKIRITA.

Ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye majina yako kamili na email yako kisha utaunganishwa kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA na kuendelea kupata mafunzo.

Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii, inabidi uwe umejiunga na KISIMA CHA MAARIFA kabla ya tarehe 05/07/2018. Hivyo mwisho kabisa wa kujiunga ili unufaike na semina hii vizuri itakuwa tarehe 03/07/2018

Karibu sana kwenye semina ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, uondoke na vitu vya kwenda kufanyia kazi kwenye biashara yako ili iweze kukua kwa kiasi kikubwa na uweze kufikia malengo makubwa uliyojiwekea kwenye maisha yako.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Rafiki, kama ungependa kujifunza zaidi kupitia mafunzo ninayotoa, karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA. Hii ni blog maalumu inayoenda na kundi maalumu la wasap ambapo kila siku unajifunza na kuhamasika, kila wiki kuna madarasa ya mafanikio na kila mwaka kuna semina tatu nzuri sana kwa mafanikio yako.

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA tuma ujumbe wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA kwa wasap kwenda namba 0717396253 au fungua hapa;  www.kisimachamaarifa.co.tz/kujiandikisha

Kupata huduma za Ukocha; www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha

Kujiunga na Kundi la kusoma vitabu; www.amkamtanzania.com/kurasa

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog