Rafiki yangu mpendwa,

Leo nina ombi la kipekee sana kwako, ombi ambalo sijawahi kulifanya kwako lakini leo inabidi nilifanye, kwa sababu najua ni kitu muhimu sana kuwahi kutokea kwenye maisha yako.

Ombi langu kwako rafiki yangu ni uniruhusu mimi rafiki yako, nikulipe wewe fedha, ili nikufundishe vitu viwili muhimu sana kwa mafanikio yako. Niko makini sana na ombi hili na ni imani yangu kwamba utakubaliana nalo, maana najua umuhimu wake kwako rafiki yangu.

Kabla sijakushirikisha kwa urefu ombi langu, naomba nikushirikishe kwa ufupi kuhusu mambo haya mawili na jinsi yalivyonisaidia mimi.

Miaka sita iliyopita, nilijifunza vitu viwili muhimu sana ambavyo vimenitoa kwenye shimo na kunifikisha hapa nilipo sasa, na ndiyo vitu viwili vitakavyonifikisha kwenye UBILIONEA na URAIS WA TANZANIA.

Miaka sita iliyopita nilifukuzwa chuo kikuu kabla sijahitimu, hivyo nilijikuta mtaani, sina ujuzi au taaluma yoyote ninayoweza kuitumia kwamba hichi nimehitimu nacho. Na katika kutafakari maisha yangu baada ya tukio lile, niliamua kwamba nitakuwa na maisha ya mafanikio makubwa sana, iwe nitahitimu chuo kikuu au sitahitimu. Niliamua kwamba maisha yangu baada ya pale ni jukumu langu binafsi na sitaruhusu kitu chochote kinizuie mimi kufanikiwa.

Ni baada ya maazimio hayo ndipo nilipoanza kufanya kila ninachoweza kufanya ili maisha yaende. Na moja ya vitu nilivyoanza navyo ni kujifunza kila ninachoweza kujifunza, na siyo tu kuweza, kila nilichokutana nacho kipya kwangu nilijifunza.

Hivyo nikajifunza mambo mengi mno, mno, nilijifunza jinsi ya kuanzisha na kuendesha biashara, nikajifunza jinsi ya kuuza kitu chochote kile, mbinu za kumfanya mtu anunue, nikajifunza jinsi ya kutengeneza tovuti na blogu, nikajifunza jinsi ya kutengeneza picha na video, nikajifunza jinsi ya kutumia mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii kutengeneza kipato. Yote haya nilijifunza, kwa sababu ya udadisi na uhitaji. Hakuna mtu ambaye aliniambia njoo hapa nikufundishe, bali ilikuwa ni mimi naona kipi sijui kisha najifunza.

095a5b996f7db11bfe3b1d93a17b444b.0

Sasa katika kujifunza mengi sana ambayo nilijifunza, nilijikuta nakwenda kwa kasi sana, kitu ambacho wengi hawakuwa wakiamini. Kwa mfano ndani ya muda mfupi niliweza kujifunza kutengeneza tovuti, kitu ambacho mtu baadhi ya wahitimu wa chuo kikuu katika fani hakuweza kufanya kwa kiwango ambacho mimi nilikuwa nafanya.

Kilichoniwezesha kupiga hatua kwenye hayo mengi niliyojifunza ilikuwa ni kuchukua hatua. Kila nilipojifunza kitu kipya, nilianza kukitumia hapo hapo. Sikusema nimejifunza kitu kizuri na nitakuja kukitumia. Bali nilichofanya ni nikijifunza kitu, naanza kukitumia hapo hapo, kabla hata hakijapoa. Na kama ilivyo kwenye vitu vingi unavyojifunza, ukifanyia kazi ndiyo unajua wapi hukuelewa vizuri, na hapo unarudi kujifunza zaidi.

Rafiki yangu, hivi ndiyo vitu viwili ambavyo nimekuwa naviishi kila siku. Kwa mfano watu wengi wamekuwa wakishangaa kwa nini naandika kila siku na siishiwi vitu vya kuandika. Na jibu ni kwa sababu naishi kila siku na najifunza kila siku. Kwa mfano kila wiki nasoma vitabu visivyopungua viwili, na siyo tu kusoma kujifurahisha, au kutimiza idadi, bali kwenye kila kitabu ninachosoma najiuliza kitu gani naweza kufanyia kazi hapa, na naanza kukifanyia kazi mara moja.

Nataka kila kitabu ninachosoma kiweke alama fulani kwenye maisha yangu, kwa sababu mwisho wa siku utasahau kila ulichosoma kwenye kitabu, lakini hutasahau jinsi kilivyobadili maisha yako.

Hii ndiyo nguvu ya kuchukua hatua kwenye kila unachojifunza, maisha yako yanakuwa bora na huishi kwa mazoea. Hata kama utachukua hatua ndogo kiasi gani, bado hutabaki pale ulipo, hasa unapochukua hatua hizo mara kwa mara.

Rafiki, vitu viwili sana ninavyotaka ujue na kufanyia kazi ni hivi;

Moja; maarifa ni muhimu mno, mno, mno. Na hapa nazungumzia maarifa sahihi kwa sababu kuna maarifa mengi ambayo siyo sahihi, na yanawazuia wengi kupiga hatua.

Mbili; kuchukua hatua ndiyo msingi wa maisha bora, maarifa pekee hayatafanya chochote kama hutachukua hatua. Hata ujue kila kitu duniani, kama hutachukua hatua kwenye unachojua, maarifa hayo hayana msaada, sana sana yamekupotezea muda wako.

Hivyo rafiki, kama kuna kitu ambacho hujapata, au kuna mahali ambapo hujafika, majibu yapo kwenye unachojua na hatua unazochukua. Huenda huna maarifa ya kutosha, au maarifa unayo ila huchukui hatua za kutosha.

Sasa kuhusu KUKULIPA ili nikufundishe kwa hakika vitu hivyo viwili, ambavyo tayari nimeshakuambia hapo juu.

Rafiki, kukuambia hivi na hata kujiambia wewe mwenyewe ni rahisi sana. Nawajua maelfu wa marafiki zangu ambao wamekuwa wakijifunza vitu hivi na kuniambia kweli Kocha nimejifunza, lakini miaka inaenda na wapo pale pale. Inapokuja kwenye kuchukua hatua hapo ndipo wengi wanakwama, wanakuwa na sababu, wanakuwa wazembe na wanarudishwa nyuma na wale wanaowazunguka.

Na hapo ndipo ninapotaka nikulipe wewe fedha, ili upate maarifa sahihi na uweze kuchukua hatua pia.

Iko hivi rafiki, mwezi julai 2018 nimekuandalia semina ya kukuza biashara yako na kutengeneza faida kwa zaidi ya asilimia 50. Ni semina ambayo kila anayetaka kufanikiwa kwenye maisha anapaswa kushiriki, ajifunze na kisha achukue hatua kuanzisha na hata kukuza biashara yake ili kufanikiwa zaidi.

Na ili ushiriki semina hii, unahitaji uwe umejiunga na KISIMA CHA MAARIFA, na ili kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, unahitaji kulipia ada ya shilingi elfu 50 (kwa sasa) ambayo ni ada ya mwaka mzima. Yaani ukishalipa elfu 50, unashiriki masomo hayo ya semina, na pia kwa mwaka mzima unaendelea kujifunza kila siku na ninaendelea kukufuatilia kwa kila hatua unayochukua ili kufikia mafanikio unayotaka kufikia.

Sasa ninapotaka kukulipa ni hapa rafiki, nataka ulipie ada ya elfu 50 na ushiriki semina hii ya biashara, kisha ujifunze na uchukue hatua kwenye yale unayojifunza, ambapo nitaendelea kukufuatilia kila mwezi. Kaa mwaka mzima kwenye KISIMA CHA MAARIFA, jifunze kila unachopata, nisumbue kadiri uwezavyo, niulize chochote kuhusu mafanikio yako na nitakujibu mara zote.

Halafu sasa, mwaka unapoisha, fanya tathmini, angalia kabla ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA na baada ya kujiunga, je maisha yako yamekuwa bora zaidi ya yamekuwa hovyo zaidi.

Kama maisha yako yamekuwa bora zaidi basi unalipia ada na kuendelea kuwa mwanachama. Kama maisha yako yamekuwa hovyo zaidi, unachofanya ni kuniandikia tu ujumbe kwamba Kocha mimi maisha yangu yamezidi kuwa mabaya licha ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA na kufanyia kazi yale niliyojifunza. Nitakachofanya, ni kukurudishia elfu 50 uliyolipa, na kama kukuomba samahani, nitakuongezea elfu 50 nyingine. Na sitakuuliza swali la ziada, nitakutumia fedha zako na uendelee na utaratibu mwingine wa maisha yako.

Rafiki niko makini na hili na sikutanii, maana sijawahi kutania inapokuja kwenye kazi zangu. Ninayaamini sana haya maarifa, yamenikomboa mimi mwenyewe na yamewakomboa wengi ninaowajua, waliokuwa kwenye mashimo marefu kuliko hata shimo ambalo wewe upo.

Na ndiyo maana nipo tayari kukulipa kama hayatakusaidia. Maana lengo langu kwenye maarifa haya siyo tu kupata fedha, bali kuhakikisha wewe umefanikiwa, na ukifanikiwa wewe na mimi nitafanikiwa zaidi. Kama ukianzisha biashara yako na ikakua, ukaajiri wafanyakazi utanitaka nije kuwafundisha wafanyakazi wako, hivyo wote tunakua zaidi.

Sasa swali kwa wengi ambao nimekuwa nawaambia hivi ni kama kweli upo tayari kunilipa nijiunge na huduma zako, kwa nini usiniruhusu niingie bure halafu nikiona maarifa ni mazuri nikulipe? Na ninakupa jibu rafiki yangu, jibu ambalo hata kama hutajiunga, litumie kwenye kila unachofanya kwenye maisha yako. Yaani hili jibu tu ambalo ninakupa hapa, linatosha thamani ya ada unayolipa kujiunga.

Iko hivi rafiki, sisi binadamu tunaendeshwa na mfumo mkubwa sana wa kisaikolojia, huwa tunahukumu na kupangilia vitu kulingana na gharama ambayo tumeingia kupata vitu hivyo. Ndiyo maana mtu akifanya kazi ya kumuumiza na akapata fedha, ataitumia vizuri na kwa makini sana. Lakini akiokota fedha, akishinda bahati nasibu au akapata urithi, hali ambazo zinampa mtu fedha nyingi ambazo hajazifanyia kazi, mtu anajikuta anatumia hovyo fedha hizo na mwisho wa siku anabaki hana kitu.

Kadhalika kwenye maarifa, ukipata maarifa ya bure, bila ya kulipa chochote, huyachukulii kwa uzito, unaona ni kitu cha kawaida, hivyo huweki mkazo sana. Lakini kama utalipia, hasa ukilipia fedha nyingi kidogo inayokuuma, utataka uone thamani ya ile fedha yako, hivyo utaweka juhudi kweli.

Hivyo unapolipa elfu 50, ambayo unajua hutaipata mpaka mwaka uishe, utajiambia wacha nifanyie kazi haya maarifa huenda fedha niliyolipa ikarudi.

Hii ndiyo sababu nakutaka ulipie rafiki yangu, ulipie ili ujitoe kufanyia kazi, lakini inapofika mwisho wa mwaka, ukawa hujanufaika kwa namna yoyote ile, niambie na nitakurejeshea mara mbili ya ulicholipa. Yaani huu ni uwekezaji ambao unapata riba kwa asilimia 100, kitu ambacho hakipo zama hizi.

Rafiki, nimalize kwa kukuambia kwamba nimejitoa kufanya kazi hii maisha yangu yote, na kila maamuzi ninayofanya huwa naangalia yana athari gani kwenye kile ninachofanya miaka 50 ijayo, miaka hamsini siyo mitano. Hivyo nikukaribishe sana, twende pamoja kwenye safari hii na nina hakika maisha yako yatakuwa bora sana.

Fanya uwezalo rafiki, omba, uza kitu ulichonacho au kusanya michango kwa jamaa zako upate elfu 50 ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA leo hii na uweze kuyabadili maisha yako. Nakuahidi hili kutoka ndani ya moyo wangu, sitakuangusha, na kama nikikuangusha basi nitakuomba msamaha kwa kukulipa zaidi ya ulicholipia.

vitabu softcopy

Nimalizie kwa kukushirikisha taarifa muhimu ya semina ya kukuza biashara tunayokwenda kujifunza mwezi julai 2018;

HABARI NJEMA KWA WAFANYABIASHARA WOTE.

Nimeandaa semina ya biashara inayokwenda kwa jina; NJIA TANO ZA KUKUZA BIASHARA YAKO, Ongeza Faida Kwa Zaidi Ya Asilimia 50 Ndani Ya Mwaka Mmoja.

Hii ni semina ambayo kila mfanyabiashara, na hata mfanyabiashara mtarajiwa atajifunza jinsi ya kuongeza faida kwenye biashara yake kwa zaidi ya asilimia 50 ndani ya mwaka mmoja.

Watu wengi wamezoea faida kuwa asilimia 10 na ikizidi sana asilimia 20 kwa mwaka. Kwenye semina hii unakwenda kujifunza mbinu 50 ambazo unakwenda kuzifanyia kazi kwenye biashara yako na faida itaongezeka kwa zaidi ya asilimia 50.

Semina hii utajifunza kwa namna ya kuchukua hatua, hivyo haitakuwa ya kujua tu, bali utakuwa na kila hatua ya kuchukua.

MAELEZO ZAIDI YA SEMINA HII NI KAMA IFUATAVYO;

Katika semina hii muhimu sana kuhusu biashara, tutakwenda kujifunza yafuatayo;

UTANGULIZI; Umuhimu wa biashara na ukuaji wa biashara kwenye zama tunazoishi sasa, maeneo matatu muhimu sana kwenye ukuaji wa biashara yako.

NJIA YA KWANZA; WATEJA TARAJIWA, njia 10 za kuwafikia wengi zaidi na biashara yako.

NJIA YA PILI; KIASI CHA WATEJA TARAJIWA WANAOKUWA WATEJA HALISI, njia 10 za kuwashawishi wanaoijua biashara yako kuwa wateja.

NJIA YA TATU; IDADI YA MIAMALA AMBAYO MTEJA MMOJA ANAFANYA, njia 10 za kuongeza idadi ya miamala mteja anayofanya.

NJIA YA NNE; WASTANI WA FEDHA ANAYOLIPA MTEJA, njia 10 za kuongeza wastani wa malipo anayofanya mteja kwenye biashara yako.

NJIA YA TANO; KIASI CHA FAIDA KWENYE KILA UNACHOUZA, njia 10 za kuongeza kiasi cha faida kwenye kila unachouza.

HITIMISHO; KANUNI SAHIHI YA KUTUMIA ILI KUKUZA BIASHARA YAKO KWA KUONGEZA FAIDA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 50 KWA MWAKA.

Njia hizi tano za kukuza biashara zinategemeana, na kama ambavyo tutajifunza kwenye semina hii inayokuja, zote zinafanyika kwa pamoja na siyo kwamba unachagua njia moja na kuacha njia nyingine.

Nikukaribishe sana rafiki yangu kwenye semina hii ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, ni semina ambayo imekuja wakati sahihi kwako kwa sababu kila biashara zina changamoto na kipindi hichi, changamoto zimekuwa nyingi zaidi.

Semina hii itafanyika kwa njia ya mtandao, kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo unaweza kushiriki semina hii ukiwa popote pale, bila ya kuhitajika kusafiri au kuacha shughuli zako. Unachohitaji kufanya ni kutenga muda kwenye siku yako ya kufuatilia masomo haya na kisha kufanyia kazi.

Semina hii nzuri itafanyika mwezi julai 2018, itafanyika kwa siku saba, kuanzia tarehe 05/07/2018 mpaka tarehe 11/07/2018. Hizi zitakuwa ni siku saba za kujifunza mambo ambayo yataifanya biashara yako iweze kukua kwa kiasi kikubwa sana.

Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii unahitaji kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Ukishakuwa mwanachama huhitaji kulipa gharama za ziada kushiriki semina hii.

Kama bado hujawa mwanachama, unapaswa kulipa ada ya mwaka ya KISIMA CHA MAARIFA, ambayo kwa sasa ni shilingi elfu hamsini (50,000/=). Hii ni ada ya mwaka mzima, ambayo inakupa nafasi ya kuendelea kujifunza kila siku kwa mwaka mzima tangu ulipolipia.

Ili kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma ada, tsh 50,000/= kwa MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/ AIRTEL MONEY 0717 396 253 majina yatakuja AMANI MAKIRITA.

Ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye majina yako kamili na email yako kisha utaunganishwa kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA na kuendelea kupata mafunzo.

Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii, inabidi uwe umejiunga na KISIMA CHA MAARIFA kabla ya tarehe 05/07/2018. Hivyo mwisho kabisa wa kujiunga ili unufaike na semina hii vizuri itakuwa tarehe 03/07/2018

Karibu sana kwenye semina ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, uondoke na vitu vya kwenda kufanyia kazi kwenye biashara yako ili iweze kukua kwa kiasi kikubwa na uweze kufikia malengo makubwa uliyojiwekea kwenye maisha yako.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Rafiki, kama ungependa kujifunza zaidi kupitia mafunzo ninayotoa, karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA. Hii ni blog maalumu inayoenda na kundi maalumu la wasap ambapo kila siku unajifunza na kuhamasika, kila wiki kuna madarasa ya mafanikio na kila mwaka kuna semina tatu nzuri sana kwa mafanikio yako.

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA tuma ujumbe wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA kwa wasap kwenda namba 0717396253 au fungua hapa;  www.kisimachamaarifa.co.tz/kujiandikisha

Kupata huduma za Ukocha; www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha

Kujiunga na Kundi la kusoma vitabu; www.amkamtanzania.com/kurasa

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

Usomaji