Mpendwa rafiki,

Maisha unayoishi sasa ni maamuzi yako mwenyewe uliyochagua kuyafanya bila kushikiwa fimbo. Hivyo basi, hata unapoishi maisha yako jaribu kuishi kwa kuangalia wewe unataka nini na siyo watu wanataka nini. Kama una ishi kwa lengo la kuwafurahisha watu hapo utakuwa unajidanganya mwenyewe.

Kama umeingia katika maisha ya ndoa kwa kufosiwa kwa sababu ya umri umeenda sana, watu watakuonaje tayari umeshaanza kutokuwa na mamlaka juu ya maisha yako, wako ambao wanaingia katika maisha ya ndoa kwa kuongozwa na hisia na hawa ndiyo watu wengi sana, wengi leo wanajuta kwanini walifanya maamuzi fulani kwa sababu ya kutumia hisia kufanya maamuzi badala ya kutumia akili.

urafiki kwenye ndoa

Rafiki yangu, hakuna kitu chenye nguvu kubwa katika maisha ya ndoa kama upendo. Upendo katika maisha ya ndoa unaweza kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi kwa kila mmoja. Upendo huwa una nguvu katika kila eneo la maisha yetu na ukitaka maisha yako ya ndoa yaende vizuri basi tumia falsafa ya upendo, hakuna mtu aliyetumia upendo akabahatika kupewa chuki.

Kwanini upendo? Kwanza upendo huvumilia yote, ukiwa na upendo mtachukuliana, kila mmoja atabeba madhaifu ya mwenzake, mtabebana lakini kama maisha ya ndoa hayana upendo basi ni mzigo mkubwa lakini kama umeingia kwenye ndoa kwa upendo, kwa gia ya kwenda kutumika na siyo kutumikiwa utakuwa na maisha bora ya ndoa.

SOMA; Fedha Inayonunua Kila Kitu Katika Maisha Ya Ndoa

Wengi wanaingia au waliingia kwenye maisha ya ndoa kwa lengo la kwenda kutumikiwa ndiyo maana kwa sasa wengine wameshindwa kwa sababu wamekutana na mambo tofauti na vile walivyotarajia. Ndoa bora inabadilisha familia na kuwa familia bora, vivyo hivyo familia bora inabadilisha jamii na kuwa bora.

Kama tunataka tubadilishe familia zetu basi tuanze kubadilisha kwanza ndoa, hakuna familia itakayokuwa bora kama hakuna ndoa iliyosimama.

Hatua ya kuchukua leo; tumia falsafa ya upendo kung’arisha ndoa yako. upendo utabadilisha kila kitu kwenye ndoa jaribu ufaidike.

Kwahiyo, usisubiri wahisani waje wabadilishe maisha yako ya ndoa, anza wewe kubadilisha maisha yako ya ndoa kwani ni yako na ni wajibu wako kuwajibika kwa kila kitu. Hujaazima ndoa bali ulifunga mwenyewe hivyo ni wajibu wako kuweka ndoa yako katika mkao mzuri na unaweza kama ukiamua, kama unaweza mengine na hili nalo utaweza.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki yangu.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com , kessydeo@mtaalamu.net

Unaweza kutembelea tovuti yangu kwa kujifunza zaidi kila siku na kupata huduma mbalimbali kama vile vitabu, kwa kutembelea tovuti  hii  hapa  www.mtaalamu.net/kessydeo .

Asante sana na karibu sana !