Rafiki yangu mpendwa,

Juma jingine la mwaka huu 2018 limeshamalizika, ni juma namba 40 na hivyo tumebakiwa na majuma 12 pekee kwenye mwaka huu ambao tuliuanza kitambo siyo kirefu na kupanga makubwa sana kwenye mwaka huu.

Ni matumaini yangu kwamba kadiri majuma yanavyokatika, ndivyo na wewe unavyotekeleza mipango uliyojiwekea kwenye mwaka huu. Na kama unalitumia kila juma vizuri, kama ambavyo tunajifunza na kushirikishana, basi utakuwa unapiga hatua kubwa sana.

Karibu kwenye tano za juma, mkusanyiko wa mambo matano muhimu ninayokuwa nimekuandalia wewe rafiki yangu. Kwa kujifunza mambo haya matano na kuchukua hatua, unajiweka kwenye nafasi ya kuweza kufanikiwa zaidi.

Na kwenye tano za juma hili, nakwenda kukupa nafasi ya kipekee kabisa, ya kujifunza falsafa itakayokuwezesha kuwa na furaha wakati wote wa maisha yako, hata kama umepoteza kila kitu.

KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO

Karibu kwenye tano za juma, fungua akili yako kwa ajili ya kujifunza kisha kuwa tayari kuchukua hatua kufanyia kazi yale uliyojifunza.

Na hizi ndizo sindano tano muhimu za juma namba 40 kwa mwaka huu 2018.

#1 NILICHOJIFUNZA; JUMA LA USTOA NA MISINGI KUMI YA MAISHA YA FURAHA.

Juma la kwanza la mwezi Oktoba kila mwaka, taasisi zinazojihusisha na falsafa ua ustoa, zimelifanya kuwa juma la ustoa. Hili ni juma ambalo watu wanajifunza kuhusu falsafa ya ustoa na kujaribu kuishi kwa falsafa hiyo kwa juma zima na kuona kama falsafa hii inayafanya maisha yao kuwa bora zaidi. Kama unajiuliza huo ustoa ndiyo nini, usiwe na shaka, nitakueleza kwa lugha rahisi kabisa kuelewa.

Lakini kabla sijakueleza kuhusu ustoa nikuambie kwamba nilikutana na falsafa hii ya ustoa kama miaka mitano imepita sasa, na imeyafanya maisha yangu kuwa bora sana. Licha ya kukutana na changamoto mbalimbali kwenye maisha yangu, sijawahi kutetereka kwa sababu falsafa hii imenipa msingi muhimu sana wa kuyaendesha maisha yangu, kwa kutokutegemea chochote cha nje na kuwa imara ndani.

Juma la ustoa mwaka huu 2018 nilitumia nafasi hiyo kuwashirikisha wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA tahajudi na tafakari za kila siku, na wengi wameeleza kunufaika sana na falsafa hii. Na sasa nakwenda kukushirikisha wewe rafiki yangu misingi kumi muhimu ya kuendesha maisha yako kwa falsafa ya ustoa na uweze kuwa na furaha wakati wote bila ya kujali nini kinaendelea kwenye maisha yako.

Lakini kwanza tuanze na kukuelezea maana ya ustoa;

Ustoa ni falsafa ya matendo, ni falsafa ambayo imelenga kumwezesha mtu kuwa na maisha bora, kwa kufikiri sahihi na kuchukua hatua sahihi kwenye maisha yake. Falsafa ya ustoa siyo kama falsafa nyingine za kubishana na kutaka kuonekana unajua zaidi, badala yake ni falsafa ya kufikiri sahihi na kuchukua hatua sahihi. Falsafa ya ustoa inalenga kudhibiti hisia zetu na kuishi kulingana na asili. Kwa njia hiyo, tunakuwa na maisha bora wakati wote.

Falsafa ya ustoa ilianzishwa na Zeno wa Citium miaka ya 301 K.K na baadaye kupokelewa na kukuzwa na wanafalsafa Cato, Seneca, Epictetus na Marcus Aurelius. Hawa wote ni wanafalsafa walioishi zaidi ya miaka 2000 iliyopita, wakati wa utawala wa Roma.

Kuhusu Juma la ustoa;

Taasisi ya MODERN STOICISM imekuwa ikiweka juhudi katika kufundisha na kusambaza falsafa ya ustoa katika nyakati hizi.

Taasisi hii imekuwa inaandaa mafunzo na matukio ya kistoa kila mwaka. Na mwezi oktoba kila mwaka wamekuwa wanaandaa juma la ustoa, ambapo kwa juma zima, watu wanaishi kwa misingi ya ustoa na kuona kama itawasaidia kuyafanya maisha yao kuwa bora zaidi.

Kwenye juma la ustoa, kunakuwa na Kauli mbiu ya juma, mwongozo wa siku na tafakari za kila siku, asubuhi, mchana na jioni.

Kauli mbiu ya mwaka 2018.

Kauli mbiu ya juma la ustoa mwaka 2018 ni KUISHI KWA FURAHA.

Kuishi maisha ya furaha ni moja ya misingi muhimu sana ya ustoa. Kwenye juma la ustoa mwaka huu 2018, tumeweza kuishi kwa msingi wa maisha ya furaha kwa juma zima.

Kauli ya Seneca kuhusu kuishi kwa furaha;

“What is a happy life? It is peacefulness and lasting tranquillity, the sources of which are a great spirit and a steady determination to hold fast to good decisions. How does one arrive at these things? By recognizing the truth in all its completeness, by maintaining order, moderation and appropriateness in one’s actions, by having a will which is always well-intentioned and generous, focused on reason and never deviating from it, as lovable as it is admirable.” – Seneca, Letters, 92.3

Seneca anauliza maisha ya furaha maana yake nini? Ni maisha ambayo yana amani na utulivu, ambayo chanzo chake ni imani kuu na maamuzi ya kushikilia maamuzi sahihi. Na je mtu anawezaje kufikia hili? Ni kwa kugundua ukweli kamili, kwa kuenda kulingana na mipango, kuwa na kiasi katika matendo na kuwa na nia njema na ukarimu, kuongozwa na fikra sahihi na kutokupotoka.

MISINGI KUMI YA MAISHA YA FURAHA KUTOKA KWENYE FALSAFA YA USTOA;

MSINGI WA KWANZA; TEGEMEA KUKUTANA NA WATU WABAYA.

Huwa tunazianza siku zetu tukitegemea kutekeleza yale tuliyopanga na kufanya mambo makubwa sana. Lakini siku zetu zimekuwa haziendi kama ambayo tumepanga, yamekuwa yanatokea mambo ambayo hatukutegemea yatokee, hasa kwa wale ambao tulitegemea wafanye vitu fulani na wasifanye.

Hili limekuwa linawanyima wengi furaha, lakini kwa falsafa ya ustoa, hupaswi kukosa furaha kwa mambo kama hayo, kwa sababu unapaswa kuyategemea yakitokea kabla hata hayajatokea.

Mstoa Marcus Aurelius ana hili la kutuambia pale tunapoianza siku yetu;

“Say to yourself first thing in the morning: I shall meet with people who are meddling, ungrateful, violent, treacherous, envious, and unsociable. They are subject to these faults because of their ignorance of what is good and bad.” (Meditations, 2.1)

Jiambie unakwenda kuianza siku ambayo utakutana na watu wachafu, wasio na shukrani, wenye fujo, wasaliti, wenye wivu na wasiojali mambo ya wengine. Na wanafanya mambo hayo kwa sababu hawajui mazuri na mabaya.

Kwa kuianza asubuhi yako kwa tafakari yenye nguvu namna hii, hakuna chochote kitakachokutokea ambacho kitakushangaza, maana ulishakitegemea.

MSINGI WA PILI; IPIME KILA SIKU YAKO KABLA YA KULALA.

Kila siku tunayoishi ni nafasi nzuri kwetu kuwa bora zaidi, kwa sababu kuna mengi tunakutana nayo ya kujifunza, kuna makosa tunayoyafanya na yapo mazuri tunayafanya pia. Wengi wamekuwa wanakosa nafasi ya kuzitumia siku zao kuwa bora zaidi kwa sababu hawapati muda wa kutafakari kila siku yao.

Kupitia Ustoa, tunashauriwa kuipima na kutafakari kila siku yetu kabla ya kulala. Na hapa ndipo tunapata nafasi ya kujifunza na kujiandaa kuwa bora zaidi kwenye siku inayofuata.

Jioni unapoimaliza siku yako, usikimbilie tu kulala na kuona siku imeisha, badala yake unahitaji kuwa na tahajudi ambayo utaipitia siku yako yote.

Kwenye tahajudi hii, pitia siku yako nzima, kwa kufikiria kila ulichofanya kwenye siku yako, kila uliyekutana naye na mawazo na hisia ulizokuwa nazo siku nzima.

Kisha jiulize na kujijibu maswali haya matatu;

Moja; vitu gani umefanya vibaya? Katika yale uliyofanya kwa siku nzima, je vitu gani umefanya kwa ubaya au kwa njia ambazo siyo sahihi?

Mbili; vitu gani umefanya vizuri? Katika vitu vyote ulivyofanya kwa siku nzima, vipi ambavyo umevifanya kwa uzuri, ni kwa namna gani umeishi misingi na tabia za ustoa?

Tatu; Vitu gani utakwenda kufanya tofauti? Ni vitu gani unahitaji kuvifanya kwa utofauti ili kuweza kuishi kulingana na msingi na tabia za ustoa?

Kwa kujiuliza na kujipa majibu ya maswali hayo matatu, utaweza kujipima kwa kila siku yako, na pia kujiandaa vyema kwa siku inayofuata. Pia utaepuka kurudia makosa uliyofanya kwa siku husika.

Kauli ya Epictetus kwenye tahajudi ya jioni;

“Allow not sleep to close your wearied eyes, Until you have reckoned up each daytime deed: “Where did I go wrong? What did I do? And what duty’s left undone?” From first to last review your acts and then Reprove yourself for wretched [or cowardly] acts, but rejoice in those done well.”

(Discourses, 3.10.2–3)

Anasema usikubali usingizi ufumbe macho yako kabla hujahesabu kila tendo ulilofanya kwenye siku yako. kipi umekosea, kipi umefanya vizuri na kipi ambacho hujakamilisha. Kuanzia tendo la kwanza mpaka la mwisho, jikaripie kwa yale uliyofanya vibaya na jisifie kwa yale uliyofanya vizuri.

MSINGI WA TATU; FANYA KILICHO SAHIHI, LAKINI USITEGEMEE CHOCHOTE.

Moja ya sababu zinazopelekea wengi kukosa furaha ni kufanya vitu ambavyo wanajua siyo sahihi, lakini kwa sababu wengine wanafanya au wanawategemea wafanye, basi wanafanya ili kuwaridhisha wengine. Hatari nyingine kubwa ni watu kufanya kitu wakitegemea matokeo fulani yatokee. Yaani unachukua hatua, ukitegemea matokeo fulani ili uwe na furaha. Hii ni njia ya kujitengenezea kushindwa na kujinyima furaha.

Cicero ana haya ya kutuambia kuhusu kufanya na kutegemea;

The wise person does nothing that he could regret, nothing against his will, but does everything honourably, consistently, seriously, and rightly; he anticipates nothing as if it is bound to happen, but is shocked by nothing when it does happen …. and refers everything to his own judgement, and stands by his own decisions. I can conceive of nothing which is happier that this. – Cicero, Tusculan Disputations 5.81

Mtu mwenye hekima hafanyi chochote atakachoweza kujutia, hafanyi chochote kinyume na matakwa yake bali anafanya kila kitu kwa heshima, msimamo, umakini na usahihi; hategemei chochote kitatokea kwa yeye kufanya, lakini pia hashangazwi na chochote kinachotokea, na anarejea kila kitu kwa maamuzi yake mwenyewe na kusimamia maamuzi hayo. Hakuna kitu chenye furaha kama kuishi kwa namna hii.

Kama ambavyo Cicero anatuambia, furaha siyo kitu unachokipata kutokana na kupata vitu fulani au kuwa kwenye hali fulani kama wengi wanavyofikiri.

Bali furaha ni matokeo ya maisha unayoishi na namna unavyofanya mambo yako. Kama unafanya kile kilicho sahihi mara zote, ukawa na msimamo na kufanya kwa umakini na usahihi, utapata matokeo mazuri. Na kama hufanyi ukitegemea matokeo mazuri, matokeo yoyote yatakayotokea hayatabadili chochote kwenye furaha yako, kusudi lako wewe ni kufanya kwa usahihi na siyo kulazimisha matokeo unayotaka wewe. Fanya maamuzi yako na yasimamie kwenye maisha yako, hili litakupa furaha kuliko kuhangaika na kukosa msimamo.

MSINGI WA NNE; JIJENGEE TABIA NJEMA.

Tabia njema ni moja ya misingi muhimu sana kwenye falsafa ya ustoa. Kadiri unavyojijengea na kuishi kwa tabia njema, ndivyo unavyojitengenezea maisha bora na yenye furaha wakati wote. Tabia njema ndiyo zao la furaha. Kwenye ustoa, tabia njema ni pale unapoishi na kusimamia yale yenye maana kwako na kwa wengine, na kuachana na yale yasiyo na maana.

Kwenye ustoa kuna tabia njema kuu nne;

HEKIMA; Ubora katika kufikiri na kufanya maamuzi.

UJASIRI; Uwezo wa kukabiliana na hatari kwa usahihi.

HAKI; Ubora katika mahusiano yetu na wengine.

KIASI; Uwezo wa kudhibiti hisia na tamaa.

Marcus ana haya ya kutuambia kuhusu tabia njema;

If you can find anything in human life better than justice, truthfulness, selfcontrol, courage […] turn to it with all your heart and enjoy the supreme good that you have found […] but if you find all other things to be trivial and valueless in comparison with virtue, give no room to anything else, since, once you turn towards that and divert from your proper path, you will no longer be able without inner conflict to give the highest honour to what is properly good. It is not right to set up as a rival to the rational and social good anything alien to its nature, such as the praise of the many, or positions of power, wealth, or enjoyment of pleasures. – Marcus Aurelius, Meditations, 3.6

Kama unaweza kupata kitu bora kwenye maisha ya mtu zaidi ya haki, ukweli, kujidhibiti na ujasiri, kishikilie sana kitu hicho. Lakini kama utakuta vitu vingine ni visivyo na maana ukilinganisha na tabia njema, usitoe nafasi kwa kitu kingine bali tabia hizo njema. Kwa sababu utakapoacha njia yako sahihi hutaweza tena kuzingatia yale ambayo ni mazuri kwako. Siyo sahihi kuleta upinzani kati ya fikra sahihi na vitu vya nje kama sifa kutoka kwa wengine, nafasi za madaraka, utajiri na kufurahia raha.

MSINGI WA TANO; MAHUSIANO BORA.

Sisi binadamu ni viumbe wa kijamii, hatuwezi kuishi kwa kujitegemea wenyewe kwa kila kitu. Hivyo mahusiano yetu na wengine ni moja ya vitu muhimu sana kwetu ili kuweza kuwa na maisha bora.

Falsafa ya ustoa inatufundisha jinsi ya kutengeneza mahusiano bora na wale wanaotuzunguka kwa kuimarisha mahusiano yetu na ushirikiano kwenye mambo mbalimbali.

Njia bora ya kuimarisha mahusiano na ushirikiano ni kuangalia tabia nzuri zilizopo ndani ya wengine badala ya kuangalia mabaya pekee. Pia kuangalia namna ya kushirikiana na siyo kupingana.

Marcus ana maneno mazuri ya kutuambia kuhusu mahusiano;

Say to yourself first thing in the morning: I shall meet with people who are meddling, ungrateful, violent, treacherous, envious, and unsociable. They are subject to these faults because of their ignorance of what is good and bad. But I have recognised the nature of the good and seen that it is the right, and the nature of the bad and seen that it is the wrong, and the nature of the wrongdoer himself, and seen that he is related to me, not because he has the same blood or seed, but because he shares in the same mind and portion of divinity. So I cannot be harmed by any of them, as no one will involve me in what is wrong. Nor can I be angry with my relative or hate him. We were born for cooperation, like feet, like hands, like eyelids, like the rows of upper and lower teeth. So to work against each other is contrary to nature; and resentment and rejection count as working against someone. – Marcus Aurelius, Meditations, 2.1

Jiambie hili kitu cha kwanza asubuhi: Leo nakwenda kukutana na watu ambao ni waovu, wasio na shukrani, wenye fujo, wasaliti, wenye wivu na wasiojali. Watu hao wako hivyo kwa sababu hawajui kipi kizuri na kipi kibaya. Lakini mimi natambua asili ya uzuri na nimeona kipi sahihi na asili ya ubaya na kuona kipi kisicho sahihi na asili ya wanaofanya ubaya na kuona wana uhusiano na mimi, kwa sababu wana damu sawa na yangu na tunashirikiana mawazo yetu. Siwezi kuumizwa na yeyote kwa sababu hakuna anayeweza kunihusisha kwenye ubaya wake. Pia siwezi kuwa na hasira au kumchukia ndugu yangu. Sote tumezaliwa kwa ushirikiano, kama miguu, mikono, kope za macho, meno ya juu na ya chini. Hivyo kufanya kazi kwa kupingana ni kinyume na asili na chuki na kukataana ni kufanya kazi kinyume na wengine.

MSINGI WA SITA; DHIBITI HISIA ZAKO.

Moja ya changamoto kubwa zinazowapelekea wengi kushindwa kwenye maisha ni kuendeshwa na hisia badala ya wao kuendesha hisia zao. Wote tunajua kwamba pale tunaporuhusu hisia zitutawale, tunakuwa tumeondoa kabisa uwezo wetu wa kufikiri. Kwa sababu hisia kali na fikra haviwezi kukaa pamoja.

Kupitia falsafa ya ustoa, tunajifunza kwamba hisia ni kitu ambacho tunakitengeneza sisi wenyewe na hakuna anayetupa, hivyo tunaweza kuchagua kutoruhusu hisia zitawale maamuzi yetu.

Epictetus ana maneno mazuri ya kutuambia kuhusu hisia;

It isn’t the things themselves that disturb people, but the judgements that they form about them. Death, for instance, is nothing terrible, or else it would have seemed so to Socrates too; no, it is in the judgement that death is terrible that the terror lies. Accordingly, whenever we are impeded, disturbed or distressed, we should never blame anyone else but only ourselves, that is, our judgements. It is an act of a poorly educated person to blame others when things are going badly for him; one who has taken the first step towards being properly educated blames himself, while one who is fully educated blames neither anyone else nor himself. – Epictetus, Handbook, 5

Kinachotusumbua siyo kile kinachotokea, bali tafsiri yetu kwa kile kinachotokea. Kwa mfano kifo, siyo kitu cha kutisha, kama ingekuwa hivyo wanafalsafa kama Socrates wangekiogopa. Ni tafsiri yetu kwamba kifo ni kitu kibaya ndiyo inatusumbua. Hivyo hivyo, tunapokuwa tumekwazika, tumesumbuka au kupata msongo, hatupaswi kumlaumu mtu yeyote bali sisi wenyewe, kwa sababu hivyo vinatokana na tafsiri zetu wenyewe. Kwa asiyekuwa na elimu, huwalaumu wengine pale mambo mabaya yanapomtokea, anayeanza kujifunza hujilaumu mwenyewe wakati yule aliyeelimika hamlaumu yeyote wala hajilaumu yeye mwenyewe.

MSINGI WA SABA; KUWA MSTAHIMILIVU.

Maisha siyo rahisi, hakuna chochote kwenye maisha yako kitaenda kama ulivyopanga. Utakutana na magumu na changamoto ambazo zitakuangusha na kujaribu kukukatisha tamaa. Ili uweze kufanikiwa, ili uweze kupata chochote unachotaka, unapaswa kuwa mstahimilivu, unapaswa kuwa mgumu, unapaswa kuwa kinga’ang’anizi na unapaswa kutokujua kabisa msamiati unaoitwa kushindwa au kukata tamaa.

Falsafa ya ustoa inatujenga tuwe wastahimilivu kwa kutuandaa kukutana na magumu na hata kuweza kuyavuka bila ya kukata tamaa.

Ili kuzuia mabaya yanayotokea yasituvuruge, tunapaswa kuwa na maandalizi ya mabaya na magumu yanayoweza kutokea.

Kama wastoa tunaweza kujiandaa na magumu kwa njia mbili. Njia ya kwanza ni kuishi magumu yenyewe, kujiweka katika nyakati ngumu hata kama hujafikia ugumu huo. Kufanya kama vile huna kitu fulani, hata kama tayari unacho. Kwa njia hii, hutashtushwa pale kile ulichokuwa unategemea kitakapokuwa hakipatikani.

Njia ya pili ni kujijengea taswira ya magumu kabla hayajatokea. Unapopanga chochote, usiangalie tu yale mazuri unayotegemea yatokee, bali pia jenga taswira ya mabaya yanayoweza kutokea. Jiulize kipi kibaya kabisa kinachoweza kutokea, kisha pata picha kwamba kitu hicho kimetokea na ona utawezaje kukabiliana nacho. Zoezi hili la kujijengea taswira ya mabaya linakufanya usipatwe na mshangao pale unapokutana na magumu, kwa sababu ulishapata picha ya magumu hayo. Pia kwa sababu  hutapata magumu makubwa kabisa, utajiambia ulishaona magumu zaidi ya uliyokutana nayo, hivyo hayakusumbui.

Marcus anatuambia;

Be like the headland, on which the waves break constantly, which still stands firm, while the foaming waters are put to rest around it. ‘It is my bad luck that this has happened to me.’ On the contrary, say, ‘It is my good luck that, although this has happened to me, I can bear it without getting upset, neither crushed by the present nor afraid of the future.’ This kind of event could have happened to anyone, but not everyone would have borne it without getting upset. – Marcus Aurelius, Meditations, 4.49

Kuwa kama ukingo wa mto au bahari ambao unapigwa na mawimbi ya maji kila mara lakini unaendelea kusimama imara na kuyatuliza mawimbi ya maji. Chochote kibaya kinapotokea, usijiambie nina bahati mbaya hiki kimetokea kwangu, badala yake jiambie nina bahati nzuri hiki kimetokea kwangu kwa sababu nitaweza kukikabili bila ya kukasirika au kuumizwa nacho kwa sasa au wakati ujao. Kitu kama hicho kingeweza kutokea kwa yeyote, lakini siyo kila mtu anaweza kukipokea kwa utulivu.

Pia Seneca anatukumbusha kuishi kila siku yetu kama ndiyo siku ya mwisho kwenye maisha yetu;

Glad and cheerful, let us say, as we go to our rest: ‘I have finished living; I have run the course that fortune set for me’. If God gives us another day, let us receive it with joy. The happiest person, who owns himself more fully, is the one who waits for the next day without anxiety. Anyone who can say, ‘I have had my life’ rises with a bonus, receiving one more day. – Seneca, Letters, 12.9.

Kila unapoimaliza siku yako jiambie kwa furaha na uchangamfu nimemaliza kuishi, nimemaliza mwendo ambao asili imenitengenezea. Kama Mungu atanipa tena siku nyingine, nitaipokea kwa furaha. mtu mwenye furaha anajimiliki yeye kwa ujumla, anaisubiri siku nyingine bila ya wasiwasi. Yeyote anayejiambia nimeyamaliza maisha yangu, anapata zawadi ya siku nyingine tena ya kuishi.

MSINGI WA NANE; ISHI KULINGANA NA MISINGI YA ASILI.

Huwa tunayaona maisha yetu ni magumu na tuna mengi ya kukabiliana nayo, lakini hebu fikiria jinsi ulimwengu unavyojiendesha. Fikiria jinsi ambavyo sayari yetu ya dunia inalizunguka jua mwaka mzima, na kutupatia majira ya mwaka. Fikiria jinsi sayari hii inajizungusha kwenye mhimili wake kila siku na kutupatia usiku na mchana. Asili imeyapangilia mambo yake ambayo yanajiendesha vizuri.

Sisi pia tunapaswa kuishi kwa msingi wa asili, kujua kile ambacho tunapaswa kufanya, kujipanga kukifanya na kukifanya kwa ubora na msimamo kama ambavyo asili inafanya mambo yake. Kwa kuishi kulingana na asili, hata matatizo yetu yanayotusumbua yanaonekana ni madogo sana ukilinganisha na jinsi ulimwengu mzima unavyojiendesha.

Marcus ana haya mazuri kutuambia kuhusu asili;

The works of the gods are full of providence, and the works of fortune are not separate from nature or the interweaving and intertwining of the things governed by providence. Everything flows from there. Further factors are necessity and the benefit of the whole universe, of which you are a part. What is brought by the nature of the whole and what maintains that nature is good for each part of nature. Just as the changes in the elements maintain the universe so too do the changes in the compounds. — Marcus Aurelius, Meditations, 2.3

Kazi za Mungu ndiyo zinatupa sisi riziki, na kazi za asili hazitofautiani na asili yenyewe. Kila kitu kinatokana na asili. Kila kitu ambacho ni muhimu na kinachohitajika na ulimwengu mzima kinatokana na asili. Kila kinachotokana na asili na kila kinachoitunza asili ni kizuri kwa kila sehemu ya asili. Mabadiliko ya kipengele chochote kwenye asili, ndiyo yanaufanya ulimwengu kuwa kama ulivyo.

MSINGI WA TISA; JUA YALIYO NDANI YA UWEZO WAKO NA YALIYO NJE YA UWEZO WAKO.

Sisi binadamu huwa tunasumbuka na mambo mengi sana, lakini tukianza kuyaangalia mambo hayo, mengi tunajisumbua nayo bure, kwa sababu yapo nje ya uwezo wetu, hakuna chochote tunachoweza kufanya tukayabadili au kuyaathiri.

Mambo yote yanayotokea kwenye maisha yetu tunaweza kuyagawa kwenye makundi mawili, yaliyo ndani ya uwezo wetu, haya ni yale ambayo tunaweza kuyaathiri, tunaweza kuyafanya kuwa bora zaidi. Na kuna yale ambayo yapo nje ya uwezo wetu, ambapo hatuna cha kufanya.

Kwa vyovyote vile, hupaswi kusumbuliwa na chochote, kwa sababu kama kitu kipo ndani ya uwezo wako basi unahitaji kuchukua hatua, na kama kipo ndani ya uwezo wako huna hatua ya kuchukua hivyo kubaliana nacho kama kilivyo au kipuuze.

Epictetus ana njia nzuri ya kugawa yaliyo ndani ya uwezo wetu na nje ya uwezo wetu;

Some things are up to us and some are not up to us. Our opinions are up to us, and our impulses, desires , aversions-in short, whatever is our own doing. Our bodies are not up to us, nor are our possessions, our reputations, or our public offices , or, that is, whatever is not our own doing. The things that are up to u s are by nature free, unhindered, and unimpeded; the things that are not up to us are weak, enslaved, hindered, not our own . – Epictetus, Encheiridion.

Baadhi ya vitu vipo ndani ya uwezo wetu na vingine vipo nje ya uwezo wetu. Vilivyo ndani ya uwezo wetu ni maoni yetu, fikra zetu, maamuzi yetu na matendo yetu, kwa kifupi yale yote ambayo sisi tunayafanya. Vitu vilivyo nje ya uwezo wetu ni miili yetu, mali zetu, sifa zetu na nafasi nyingine tunazopewa, kwa kifupi chochote ambacho hatufanyi sisi moja kwa moja, kipo nje ya uwezo wetu. Vitu vilivyo ndani ya uwezo wetu ni bure, huru na visivyo na ukomo, vilivyo nje ya uwezo wetu ni dhaifu, visivyo huru, vyenye ukomo na visivyo vyetu.

MSINGI WA KUMI; UNA MUDA WA KUTOSHA KUFANYA YALE MUHIMU.

Moja ya kisingizio cha watu wengi kwenye kushindwa kufanya yale wanayotaka kufanya kimekua ni muda. Muda unaonekana kuwa mfupi sana na mambo ya kufanya yakiwa mengi. Hivyo tumekuwa tunatamani kama masaa ya siku yangeongezwa ili tuweze kufanya zaidi.

Lakini ukweli ni kwamba, masaa ya siku hayataongezeka, ni yale yale 24. Na wale wanaofanikiwa sawa sawa na wanaoshindwa, wana masaa hayo hayo kwa siku. Sasa kwa nini wachache wafanikiwe kwenye muda huo, wakati wengi wanashindwa na kuona hawana muda?

Seneca analo jibu zuri sana kwetu kuhusu muda;

Life is long enough, and a sufficiently generous amount has been given to us for the highest achievements if it were all well invested. But when it is wasted in heedless luxury and spent on no good activity, we are forced at last by death’s final constraint to realize that it has passed away before we knew it was passing. So it is: we are not given a short life but we make it short, and we are not ill-supplied but wasteful of it. Just as when ample and princely wealth falls to a bad owner it is squandered in a moment, but wealth however modest, if entrusted to a good custodian, increases with use, so our lifetime extends amply if you manage it properly. – Seneca, On The Shortness Of Life.

Maisha ni marefu vya kutosha na muda wa kutosha tumepewa kwa kufikia yale makubwa kama tutauwekeza muda huo vizuri. Lakini tunapopoteza muda huo kwa anasa zisizo na maana na kushindwa kufanya yale mazuri, tunakuja kustuka tumepoteza muda na maisha yetu pale tunapofikia kifo. Hivyo basi, siyo kwamba tuna maisha mafupi, bali tunayafanya kuwa mafupi, siyo kwamba muda ni mdogo, bali tunao mwingi mpaka tunaupoteza. Kama ambavyo utajiri ukiwa kwenye mikono ya mtu asiye makini unapotea na ukiwa kwenye mikono ya mtu makini unakua, ndivyo maisha yetu yalivyo, yanakua kama yataendeshwa vizuri.

Rafiki, chagua kuishi kwa misingi huu kumi ya ustoa na utakuwa na maisha bora na yenye furaha wakati wote. Hakuna chochote kitakachotokea ambacho kitakushtukiza kwa sababu ulishajua utakutana na magumu na mabaya pia. Kadhalika utaweza kujua yaliyo ndani ya uwezo wako na kuyafanyia kazi, na yaliyo nje ya uwezo wako na kuyakubali au kuyapuuza. Mwisho kabisa, wekeza muda wako vizuri kwa yale ambayo ni ya muhimu kwako, na kuachana na yale yasiyo muhimu, yasiyostahili muda wako.

Kama utapenda kujifunza zaidi kuhusu falsafa hii ya ustoa, falsafa nzuri sana kwa maisha ya mafanikio, karibu sana ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA.

#2 MAKALA YA JUMA; HATUA ZA KUCHUKUA PALE UNAPOSHINDWA KWENYE KILA UNACHOFANYA.

Wapo watu hakuna wanachojaribu kikafanikiwa. Kwanza wanasumbuka sana kupata kazi, wakiipata haidumu, wanakazana sana kuanza biashara lakini mwishowe inashindwa, na hata wanapoingia kwenye mahusiano, matatizo hayakomi. Watu hawa huwa rahisi kuamini kwamba labda wana bahati mbaya au dunia imewatenga.

Juma hili niliandika makala kuhusu hatua za mtu kuchukua pale ambapo kila unachofanya unashindwa. Kama umewahi kushindwa kwenye chochote, hakikisha unasoma makala hii, kuna mengi sana ya kujifunza. Makala ni hii hapa; USHAURI; Hatua Za Kuchukua Pale Unaposhindwa Kwenye Kila Unachofanya Kwenye Maisha Yako.

Pia kama unakazana kukuza kipato chako bila ya mafanikio, kama kipato chako kimedumaa na hakikui tena licha ya kuchukua hatua mbalimbali, nilikushirikisha makala hii ya njia moja ya uhakika ya kuongeza kipato chako. Isome hapa; Njia Moja Ya Uhakika Itakayokuwezesha Kuongeza Kipato Chako Bila Ya Kubadili Unachofanya Sasa.

#3 TUONGEE PESA; UTAJIRI NA FALSAFA.

Kwenye falsafa ya ustoa, mambo yote yanagawanyika kwenye makundi matatu;

Kundi la kwanza ni mambo ambayo ni mazuri, na haya yanajumuisha zile tabia nne nzuri kwenye ustoa, yaani hekima, ujasiri, haki na kujidhibiti.

Kundi la pili ni mambo ambayo ni mabaya, haya ni kinyume na yale ambayo ni mazuri, hivyo mabaya ni upumbavu, woga, udhalimu na tamaa.

Kundi la tatu ni mambo yasiyo na tofauti, haya ni mambo ambayo siyo mabaya na wala siyo mazuri. Hapa kuna afya, utajiri na sifa.

Hivyo kwenye ustoa, fedha inaingia kwenye kundi la tatu, kundi la vitu ambavyo siyo vizuri wala siyo vibaya. Hivyo kama mstoa, fedha siyo msukumo mkubwa kwako, lakini pia hakuna ubaya ukiwa na fedha, kama unaishi misingi ya ustoa.

Mwanafalsafa Seneca alisemwa sana kipindi chake, kwa sababu alikuwa mwanafalsafa wa ustoa, lakini pia alikuwa tajiri mkubwa sana. Hivyo watu walimwona kama anaishi kinyume na mafundisho yake ya falsafa.

Lakini Seneca alisema hili, fedha haipo kwenye yaliyo mazuri wala yaliyo mabaya, lakini ukiambiwa uchague kati ya kuwa na fedha na kutokuwa na fedha, utachagua kuwa na fedha. Lakini pia kama utapoteza fedha zote ulizonazo, hupaswi kuumia wala kulalamika, kwa sababu fedha haipo kwenye yale ambayo ni muhimu.

Seneca alikuwa na haya ya kusema pale watu walipomsema kwa utajiri wake;

So stop forbidding philosophers to have money. No one has sentenced wisdom to poverty. The philosopher will have ample wealth, but not wrested from anyone or dripping with another’s blood, and acquired without any harm to anyone or any fi lthy profiteering. Its exit will be as morally good as its entry, and no one except a stingy person would mourn for it. Pile it up as much as you wish: that wealth is morally good in which, even when there are many things that each person might wish to be called his, there is nothing that anyone can rightly call his. – Seneca, On The Happy Life.

Anasema acheni kuwanyima wanafalsafa wasiwe na fedha. Hakuna aliyehukumu kwamba hekima ni umasikini. Mwanafalsafa anaweza kuwa na utajiri mkubwa ambao hajaiba kwa wengine wala kuwaumiza wengine katika kupata utajiri huo. Pia wakati wowote atakuwa tayari kuachia utajiri huo uende bila ya yeye kutetereka.

Mwisho Seneca anatuambia kama mwanafalsafa mwenye utajiri, anaweza kufungua milango yake na kuwaambia watu mwenye chake na achukue. Hii ina maana kwamba utajiri wake anakuwa ameupata kwa misingi sahihi, hajamdhulumu wala kumwibia yeyote, hivyo hakuna anayeweza kumdai chochote.

Hivyo fedha ni muhimu kwa mambo yote yanayohusu fedha, na hakuna ubaya kuwa tajiri kama ukiwa mwanafalsafa, hasa falsafa ya ustoa.

#4 HUDUMA NINAZOTOA; KAMA BADO HUJACHUKUA HATUA HII, UNAKOSA NAFASI BORA SANA KWAKO KWA MWAKA HUU 2018.

Rafiki yangu mpendwa, kama ulikuwa hujapata taarifa au kama umesahau nachukua nafasi hii kukuarifu na pia kukukumbusha ya kwamba lile tukio letu kubwa, linalotokea kwa mwaka mara moja, mwaka huu linafanyika tarehe 03/11/2018.

Tukio hili ni SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018. Hii ni semina ya kukutana ana kwa ana, ambayo huwa nafanya mara moja kwa mwaka. Hii ndiyo nafasi pekee ya kukutana pamoja, kuweka mipango, kujifunza, kuhamasika na kwenda kuweka juhudi zaidi ili kuweza kufanikiwa zaidi.

Ada ya kushiriki semina ya mwaka huu ni tsh 100,000/= ambayo inapaswa kulipwa mpaka kufikia tarehe 31/10/2018. Namba za kufanya malipo ya ada ya semina ni 0755 953 887 au 0717 396 253, majina ya namba hizo ni AMANI MAKIRITA.

Sasa hatua muhimu sana ninayotaka wewe uchukue leo ni hii, kudhibitisha ushiriki wako, hata kama ada hutalipa leo. Maandalizi ya tukio hili la kipekee yanaendelea, hivyo napenda kuwa na idadi kamili ya watakaoshiriki semina hii. Hivyo kama unatarajia kushiriki, nitumie ujumbe kwenye namba 0717396253 wenye majina yako na namna ya simu. Tuma ujumbe huo leo hata kama hutafanya malipo leo. Kwa kudhibitisha kushiriki, unatuwezesha kufanya maandalizi bora kabisa.

Hivyo tuma ujumbe leo wa kudhibitisha kushiriki, kisha panga kulipa ada yako kabla ya mwezi huu wa kumi haujaisha.

Karibu sana kwenye tukio hili kubwa la mwaka huu 2018, karibu tukutane pamoja kwa ajili ya kujifunza na kuhamasika ili tuendelee kufanya makubwa zaidi.

#5 TAFAKARI YA KUFIKIRISHA; USIFUATE NJIA, TENGENEZA NJIA.

”Do not go where the path may lead, go instead where there is no path and leave a trail.” – Ralph Waldo Emerson

Watu wengi wamekuwa wanashindwa kwenye maisha kwa sababu hawathubutu kufanya vitu vipya, badala yake wanaangalia kile ambacho tayari kimeshafanya na wao wanafanya. Hii ni kufuata njia, sasa unapochagua kufuata njia fulani, jua utafika kule ambapo njia hiyo imeelekea. Kama utafanya kile ambacho wengine wanafanya, utapata matokeo ambayo wanayapata.

Njia pekee ya kufanikiwa zaidi, ni kufanya mambo mapya, kufanya yale ambayo hakuna mwingine anayefanya, kutengeneza njia mpya, pale ambapo hakuna njia. Hili linatisha, kwa sababu unakuwa huna uhakika, nafasi ya kushindwa ni kubwa, lakini pia nafasi ya kufanikiwa ni kubwa zaidi.

Kwenye chochote unachochagua kufanya, acha kuangalia wengine wanafanya nini ili uige, badala yake angalia kipi muhimu kinachopaswa kufanya kisha kifanye kwa njia ambayo ni sahihi kwako kufanya na kwa wale unaowahudumia. Kwa namna hii utatengeneza njia mpya na wewe kama kiongozi wa njia hiyo utanufaika zaidi.

Rafiki, sindano za leo zimekuwa ndefu na kali, lakini kama utazifanyia kazi, hutabaki hapo ulipo. Sina kingine cha kuongeza zaidi ya kukukumbusha kanuni yetu muhimu ambayo ni MAARIFA SAHIHI + KUCHUKUA HATUA KUBWA = MAFANIKIO MAKUBWA. Maarifa ni hayo, kazi kwako kuchukua hatua ili ufanikiwe.

Makala hii imeandikwa na Kocha Dr Makirita Amani.

Dr. Makirita ni Daktari wa binadamu, Kocha wa mafanikio, Mwandishi na Mjasiriamali.

Dr. Makirita anaendesha mafunzo ya mafanikio kwa wale waliojitoa hasa kufanikiwa kupitia program ya KISIMA CHA MAARIFA.

Kama bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma sasa ujumbe wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA kwa njia ya wasap namba 0717 396 253 (tumia wasap tu)

Kupata huduma nyingine za ukocha tembelea www.amkamtanzania.com/kocha

Kupata vitabu vizuri vya kusoma tembelea www.amkamtanzania.com/vitabu

Usomaji