Mpendwa rafiki,

Sisi wote hapo mwanzo tulikuwa ni watoto na baadhi ya misingi ambayo tunaishi huenda tuliipata kutoka kwa wazazi wetu kama vile mchungaji anavyochunga kondoo wake vivyo hivyo mzazi anapaswa kuwachunga watoto wake.

Viumbe vinavyopata shida katika karne hii ni watoto kwa sababu ni dunia ambayo ina kila kitu na watu wako huru kufanya kile wanachotaka na wanachojisikia hata kama siyo sahihi kwao. Watoto wako katika hatari hivyo sisi kama wazazi tusipochukua jumuku la malezi ya watoto kama wajibu wetu ni wazi tunaanda matatizo zaidi.

Ukienda hospitali ukitembelea wodi nyingi za watoto utakuta mambo mengi waliyofanyiwa watoto ni kwa sababu ya uzembe wa mzazi na mtoto kukosa ulinzi kutoka kwa mzazi wake. Mtoto mdogo mpaka anaenda anaenda jikoni na anaungua na maji ya moto hii ni wazi kabisa mzazi alikosa umakini kwa sababu ya uzembe.

raising positive kids

Wazazi wengi hawana misingi ya maisha wanaishi ili mradi siku ziende je kama mzazi hana msingi wowote anaosimamia je mtoto itakuwaje? Wazazi wengi siku hizi wamekuwa na malezi kama ya bata, si unamjua bata rafiki? Anafungwa karibu nyumba nyingi  hivyo bata mara nyingi yeye huwa anawalea watoto vibaya hana muda nao kwa mfano yeye akitembea anakuwa mbele na watoto nyumba hivyo hajui hata nini tena kinaendelea huko nyuma. Tunatakiwa tujifunze hata kwa kuku jinsi anavyojitoa kisadaka kwa vitoto vyake anivilea vizuri ili wasipatwe na kudhurika dhidi ya kitu chochote kile.

SOMA; Neno Pekee La Kumfundisha Mtoto Karne Ya 21 Ili Kumletea Mafanikio Makubwa

Siku hizi jukumu la malezi ni la wasaidizi wa kazi, na wazazi wako bize na kutafuta maisha watu wako radhi kupata muda wa kuingia kwenye mitandao ya kijamii lakini utasikia amekosa muda angalau hata nusu saa ya kukaa na familia yake nyumbani na kuongea hata na mtoto kujua anaendelea , na changamoto anapitia au anakutana nazo. Usipoipa muda familia yako ni lazima itaharibika ni sawa na mali bila daftari hupotea bila kujua.

Hatua ya kuchukua leo; mlee mtoto wako vizuri usipomlea vizuri na kumfundisha nidhamu na misingi dunia itakuja kumfundisha kwa adhabu na riba. Usimlee mtoto kwa kumpa kile anachotaka bali mfundishe kukosa hata kama unacho na kipo ndani ya uwezo wako mfundishe kukosa.

Hivyo basi, jukumu kubwa la wazazi katika familia ni kulinda familia zao, baba na mama wanaalikwa kulinda familia zao, walinde watoto wako, kiakili, kiroho na hata kimwili. Familia yako ni wajibu wako.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki yangu.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com , kessydeo@mtaalamu.net

Makala hii, imeandikwa na Deogratius Kessy,Unaweza kutembelea tovuti yake kwa kujifunza zaidi kila siku na kupata huduma mbalimbali kama vile vitabu, masomo ya kila siku, ushauri nk kwa kutembelea tovuti  hii  hapa  www.mtaalamu.net/kessydeo .

Asante sana na karibu sana!