“The nearer a man comes to a calm mind, the closer he is to strength,” – Marcus Aurelius.

Hii ni siku nyingine mpya kwetu,
Siku ya kipekee sana kwetu,
Siku ambayo tumepata nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari UIMARA UPO NDANI YAKO…
Inapokuja kwenye uimara katika maisha, watu wengi hufikiri ni kitu ambacho mtu umezaliwa nacho au huna kabisa.
Yaani ni labda umezaliwa ukiwa na uimara kwenye maeneo fulani au umezaliwa huna uimara kabisa.

Lakini hii siyo kweli, siyo kweli kwamba kuna wanaozaliwa na uimara na wengine hawana.
Wote tuna uimara ambayo tayari upo ndani yetu.
Kinachowatofautisha wanaoonekana imara na wasio imara ni utambuzi na kuufikia uimara ambao upo ndani.

Huwezi kutumia kitu ambacho hukijui na hujui kama kipo.
Hivyo hatua ya kwanza ya kuwa imara ni kujua kwamba tayari uimara upo ndani yako.
Hatua ya pili ni kuufikia na kuutumia uimara huo, na njia ya kufikia uimara huo ni kuwa na utulivu wa akili.
Kadiri mtu unavyoweza kutuliza akili yako, unavyoweza kudhibiti fikra na mawazo yako, ndivyo unavyoweza kuufikia na kuutumia uimara wako.

Kama huwezi kutuliza akili yako, na kudhibiti mawazo yako, utaishia kuyumbishwa na kila kila kitu kwenye maisha. Utaishia kuhangaishwa na kila mawazo na hofu za wengine.
Lakini ukiweza kutuliza akili na kudhibiti fikra zako, utaweza kufanya kile unachotaka kufanya.

Kwa mfano, chochote unachotaka kupata kwenye maisha yako, lazima mawazo yako yawe kwenye kitu hicho kuda wote. Lazima kila unachofikiri kiwe ni kuhusiana na kitu hicho. Na lazima uondokane kabisa na mawazo hasi juu ya kitu hicho, mawazo ya kukosa na hofu za kushindwa, hizi ni sumu ambazo kama huwezi kuzidhibiti, zitakuangusha.

Uimara unaoutaka kwa ajilo ya mafanikio yako tayari upo ndani yako, utaweza kuufikia kwa kuwa na utulivu wa akili na udhibiti wa fikra zako, vitu ambavyo tayari vipo ndani ya uwezo wako. Anza kuvitumia sasa.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuufikia na kuutumia uimara uliopo ndani yako kwa kuwa na utulivu wa akili na udhibiti wa fikra zako.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha